Kama Dangote kafunga mitungi ya gesi kwenye malori yake, Mimi ni nani hata nisibadili mfumo wa nishati ya gari yangu?

Kama Dangote kafunga mitungi ya gesi kwenye malori yake, Mimi ni nani hata nisibadili mfumo wa nishati ya gari yangu?

Zipo nyingi hadi daladala kwa siku anatumia gass ya 30000 analaza hesabu ya 200000 na hapo ushatoa posho ya kon
Uber na bolt ndo zinaongoza kwa kutumia gasi ktk hizi gari ndogp
 
@

Bado sana watu kuwa wengi...

Hadi sasa gesi asili inafikika mikoa minne tu Mtwara, Lindi, Pwani na Dar...

Na katika mikoa hiyo si wilaya zote bali zile zilizo pembezoni mwa bomba la gesi asilia...

Bahati mbaya sana sera za CCM juu ya gesi asilia zipo kwenye makaratasi tu, mfano ukifuatilia domestication ilivyo fanyika utaona ni nyumba chache tu zinazofaidi kwenye kutumia gesi hiyo kupikia majumbani...

Sehemu pekee ambapo umma wote umefaidika ninkwenye uzalishaji umeme...
Hii gesi nchi nyingine ingekuwa imeshasambaa kila mkoa na watu wanafaidi matunda ya nchi yao,, afrika tunakosea wapi?
 
Kutuuliza sisi ni kutuonea......ilitakiwa uwaulize hukohuko chamani kwenu mdo wanaweza kukupa jibu stahiki
Mkuu, katika vitu tunafeli waafrika ni kutegemea kila kitu toka kwa wazungu!

Sioni kama selikali yangu ya ccm inafanya juhudi zozote kuhakikisha hii gesi inawanufaisha wanachi kama ilivyo kwa waarabu na mafuta,.
 
Tatizo sio kwamba nimeshindwa kununua petroli, tatizo wanufaikao na too za petroli ndio adui zangu.
KWENYE petroli tunatozwa Hadi Kodi za kuwastarehesha wakurugunzi
Sawa sasa nimekupata vyema kabisa.
 
Gesi ni kama sola. Gharama ni kubwa sana mwanzoni katika kuweka mifumo yake. Ukishaweka unaenjoy maisha mpaka itakapopata hitilafu na kuhitaji repair. Ila ni chaguo zuri sana.

Nashauri ufanyike uwekezaji mkubwa kwenye vituo vya kujazia na utengenezaji wa mitungi bora hapahapa nchini.

Halafu kabla sijasahau, tuliambiwa gesi ya mtwara itakuwa ikitumika majumbani mwetu kipitia mabomba kama ilivyo maji ya DAWASA, hii plani imeishia wapi? Au ilikuwa danganya toto ya wanasiasa?
Mbona inatumika tayari
UDSM, Mikocheni maeneo mengine miundombinu bado
 
Mafuta yanapanda Bei Kila kukicha, kipato kinapungua kila kukicha.

Nimepita Ubungo, kituo cha kujaza natural kwenye magari (sheli, tuite hivyo ili nieleweke) nimekuta kg 1 ni shilling 1550.
Gharama za kubadili mfumo ni kama milioni moja na kidogo.

Jumamosi naipeleka gari ikabadilishwe mfumo, sitaki ujinga mimi
Kuna vituo vingapi vya kujaza gesi nchini kwa dar mie nakijua cha ubungo tu

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom