Kama dunia inazunguka, kwanini miamba na milima haiporomoki? Na kwa nini bahari isimwage maji yake?


Je ulichoandika ni kile ulichoelewa? au ni tafsiri ya neno kwa neno aka direct tu kwa kiswahili kutoka sehemu?
 

Sio tu dunia ndiyo inayozunguka hata jua linazunguka. Jua na nyota na sayari vyote huzunguka,mzunguko hufanyika kwa nyota na vyote kuzunguka kutokea kizio cha galax. mfano, mzuri ni kama vile unavyoona vumbi la chamchela inavyozunguka tokea kiini cha katikati.Sasa tuchukulie vile vipande vya vumbi ndio nyota

Sasa inakuwaje hatuhisi mzunguko huo? Dunia ni kubwa mno na katika mzunguko huo dunia ina kwenda kwa kasi ya takriban kilometa 110,000 kwa saa julizunguka jua na Jua linatumia takriban miaka milion 250 kuzunguka kiini cha galax. Kasi ya jua kuzunguka kiini cha galax ni kilometa 220,000 kwa sekunde moja. Hii inajenga picha ya namna upana wa galax tuliomo (Milky Way) ulivyo.

Hivyo ukubwa wa dunia hauwezi kutufanya tuone na kuhisi huo mzunguko na pia upana wa eneo la galax yetu hautoifununu ya kuona kasi ya vile tuzungukavyo na dunia yetu.

Aidha,galax ya milky way ni moja kati ya mabilion ya galax.

NB: Mwacheni Mungu aitwe Mungu!
 
Nimekupata sana mkuu thnx
 
Wakuu ahsanteni sana nimewalewa sana sana salute i appriciate to maximum.
 
 
Jaribu kufikiria Sumaku kubwa iliyoganda kwenye vichuma vidogo vidogo!!

Je hiyo sumaku ikizunguka hivyo vichuma navyo vitaanguka? Au vitajiachia kwenye sumaku?

Pia kuzunguka ingawa ni suala la kifizikia (Motion) but lina impact kwenye saikolojia pia (kizunguzungu), sasa mbona hatusikii kizunguzungu kama kweli muda wote tunazunguka? Jibu ni rahisi, kila kitu ni kinazunguka.

Yaani wakati tunazunguka hakuna ambacho hakizunguki kwamba ukikiangalia utaona kiko palepale. Wewe unazunguka na vyote unavyoviona navyo vinazunguka.
 
Mkuu; kwanza nikuondoe wasiwasi kuhusu usahihi wa maana ya tungamo na uzito. Uko sahihi kabisa kuwa Tungamo ni Mass na Uzito ni Weight.
Rejea Kanuni ya pili ya mwendo ya Newton: KANI = Tungamo * Mchepuo wake (i.e Weight = Mass * Acceleration)
Baada ya kuwa nimekuondolea hofu hiyo, ningependa kuongezea maarifa kidogo kuhusu badiliko la uzito wa kitu kiwapo maeneo tofauti.
Ieleweke tu kuwa uzito wa kitu hubadilika kutegemea na kiasi cha nguvu ya uvutano wa dunia (gravitational force) cha mahali kitu kilipo, ama sehemu kwenye uso wa dunia au sehemu mbali na uso wa dunia (ndani au nje).
Kwenye uso wa dunia kiasi cha nguvu hii ki-tofauti katika maeneo ya Ikweta na katika maeneo ya ncha mbili za dunia yaani ncha ya kaskazini na ncha ya kusini (Northern and Southern poles). Hii iko vile kutokana na umbo halisi la dunia lilivyo.
Dunia ina umbo mfano wa boga (oblate structure) ambalo limebonyea katika sehemu mbili zinazokabiliana, ndizo kwenye ncha ya kaskazini na ncha ya kusini. Umbo hili hufanya uso wa dunia kwenye ncha hizi mbili kuwa na umbali mfupi zaidi kutoka kwenye kitovu cha dunia kuliko uso wa dunia kwenye Ikweta na hivyo kuwepo nguvu tofauti ya uvutano, hivyo tofauti ya uzito wa kitu kiwapo kwenye maeneo haya mawili.
Nawasilisha.
 
 

mkuu kijiko

Asante kwa kunikumbusha,mchango wako ni mzuri.Watu wengi hufikiria dunia ni duara kamili lakini sivyo,dunia ipo kama boga na kuna ushahidi wa kutosha juu ya hilo mkuu..

Nashukuru tena.
 
Last edited by a moderator:
Vp kuhusu ndege ikipaa huwa inakuwa wap dunian au wap? , km dunia inazunguka kwa nini ndege huwa azikose lengo wakat zinatua? Na je ni kweli tupo up side down?

swali lako la ndege kukosea halijajibiwa sijui hakuna marubani humu hata mi ningependa kujua please pilot
 
swali lako la ndege kukosea halijajibiwa sijui hakuna marubani humu hata mi ningependa kujua please pilot


Wakuu mdukuzi na MWAMFUPE

Mzunguko wa Ardhi hauathiri kabisa ndege ikiwa inapaa angani au imetua Ardhini, sababu kubwa na muhimu ni mvutano wa Ardhi (Earth Gravity) hufanya kuwa kila kitu kinazunguka pamoja na mzunguko wa Ardhi hata anga nayo inazunguka kwa speedi ya Ardhi.
 

Hapana!! Ukisema "hauathiri kabisa" unakosea na labda hujui hilo, mzunguko wa Dunia unaleta Coriolis effect hivyo kuna athari inayotokana na tofauti ya vitu hivi viwili (Dunia na Ndege) kuwa viko kwenye position tofauti, ingawa athari hii ni ndogo sana kwa kuwa speed ya rotation ya Dunia si kubwa. Ndege haikai katika stationary state inapokuwa angani (ina engines zinazoisukuma) hivyo kama ingekaa katika hali ya kutulia sehemu moja tu kungekuwa na athari zaidi kutokana na gravity na pia coriolis effect kwa kiasi kidogo.

Vitu vyote vinavyoruka angani umbali mkubwa vinaathiriwa na Coriolis effect kwa kiasi fulani na Pilots wa yale madege makubwa wanajua kuhusu hili kwa ufasaha. Ndege haiwezi kuruka mstari ulionyooka kutoka bara moja hadi jingine bila Pilot kuweka sawa njia yake kwa sababu Dunia inazunguka. Ukisema haiathiri kabisa ina maana una ignore physics laws na sayari nyingine zenye rotation ya kasi zaidi ya Dunia huko Coriolis effect ni kubwa zaidi na inaathiri anga maradufu ya Dunia. Vimbuga vya huko hapa duniani hatujawahi kuona.

Wakati Corioris effect iko mahali pake na Earth gravity pia iko mahali pake, Ndege na Dunia vinaendelea kuathiriwa na Gravity pull ya Jua hivyo hata kama ndege itakuwa juu na ikae katika stationary state dhidi ya mzunguko wa Dunia bado ingeendelea kulizunguka jua pamoja na Dunia. Jua nalo liko katika mwendo kuzunguka kiini cha galaxi yetu MilkyWay kama nyota nyinginezo hivyo pia linaathiriwa na mvuto mkubwa wa super massive blackhole katika center ya galaxi.
 

Mkuu tafadhali naomba uandike kwa maneno huo uzito wa dunia ulioainisha hapo juu tafadhali...mim nimeshindwa..!
 

Mkuu kumbe na jua pia huzunguka(galaxy)?? Kwa elimu yangu ya jiografia ya darasa la saba nilijua dunia na sayari zingine ndiyo huzunguka jua..!!
 
Kwa kua hapa ni suala la fikra zaidi na wengine Jiografia ilitupita pembeni, naomba kujuzwa yafuatayo:-

1- Hiyo gravity inavuta vitu kuelekea katikati ya dunia?
2 - Hiyo grafity force ipo kwenye sayari ya dunia tu au kila sayari ina gravity force yake?
3 - Jua nalo linavuta vitu kuelekea kwake, namaanisha sayari zote zinavutwa kuelekea katikati (jua liliko)?

Natanguiza shukrani
 
Kuna swali kauliza bwana mmoja halijajibiwa wakuu"" kama mtu ukiruka na chombo angani ukiwa hapa dar na ukakaa stationary kwa masaa kazaa huko angani atakaporudi ardhini anaweza kujikuta eneo tofauti na dar?"""
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…