Chopa imeanguka hayupo aliyeiona ikianguka, hiyo picha uliyoiweka hapo ni satellite au umeitoa wapi? Pembeni panaonekana kuna ukungu kuonesha hali mbaya ya hewa iliyokuwepo eneo la tukio.
Inawezekana myahudi amefanya jambo lake, kwasababu kama kweli Iran wanaintelijensia wangetakiwa kujua kama wanawindwa na adui, kitendo cha kufeli kutambua hilo kinaonesha Iran bado dhaifu sana kimbinu za kijeshi, hawa hawana uwezo wa kushindana na myahudi.
Sababu ya hali ya hewa iliyotumika inaweza kuwa inatumiwa na Iran wenyewe kuficha ukweli wa kile kilichowakuta, kama waliona hali mbaya ya hewa kwanini wakarusha chopa? hawakujua athari zake?
Hii sababu waliyoitoa kwangu haiingii akilini.