Kama hauna nia ya kumuoa usimpe mimba

Kama hauna nia ya kumuoa usimpe mimba

Kumekua na wimbi la akina dada kuzalia nyumbani hasa hawa wa miaka 19-26. Unakuta kijana anajua hana uwezo wa kuhudumia mimba na kuchukua majukumu kama baba lakini anazalisha tu.

Kuna hawa jamaa ambao wameshaoa, anakuwa na kamchepuko kwa tamaa zake, anakazalisha. Wakati uwezekano wa kumuoa haupo. Hii inachangia sana kujaza single mothers mtaani.

Hivi utajiskiaje kuona dada yako ambaye amezalishwa bila kuolewa na masela, anafika kwenye mwisho wa 20's anapatikana mtu mwenye nia ya kuoa lakini anasitisha kwa kuhofia kuoa single mother (maana single mothers wanalika kirahisi na wazazi wenza).

Vijana tubadilike, kama hauna nia ya kumuoa usimpe mimba.
Kwa uzoefu nilionao mimi, hao akina dada ndio wanategesha mimba, kwa nia ya kuja kuitumia ili kukubana umuoe au uwe unahudumia na yeye afaidikie humohumo, usiwahurumie sana!

Kwanza anatakiwa ajue siku zake vizuri na asifanye mapenzi kabisa kwenye siku hizo kama kweli hataki mimba.
 
Mwisho wa siku hakuna hata huduma ndio wanaachwa tu hivo....
Kwa uzoefu nilionao mimi, hao akina dada ndio wanategesha mimba, kwa nia ya kuja kuitumia ili kukubana umuoe au uwe unahudumia na yeye afaidikie humohumo, usiwahurumie sana!

Kwanza anatakiwa ajue siku zake vizuri na asifanye mapenzi kabisa kwenye siku hizo kama kweli hataki mimba.
Kwanini kia tatizo la mwanamke its mens fault yaani jamii inafanya wao kama mbuzi wasiokua na akili
 
Kwa uzoefu nilionao mimi, hao akina dada ndio wanategesha mimba, kwa nia ya kuja kuitumia ili kukubana umuoe au uwe unahudumia na yeye afaidikie humohumo, usiwahurumie sana!

Kwanza anatakiwa ajue siku zake vizuri na asifanye mapenzi kabisa kwenye siku hizo kama kweli hataki mimba.
Na hata akifanya mapenz ktk siku za hatari kuna vidonge vya P2 wanapaswa kujizoesha kutumia.
 
Sio wanawake wote wapo kwa ajili ya kuolewa.
Na sio wanaume wote ni waoaji.
 
Sijui watu wengine huwa wanachukuliaje, mi kwangu kitendo cha kuzaa naona ni kikubwa sana kikubwaa mnooo yani kuzaa sijawahi kuichukulia kirahisi....nashangaa maamuzi ya watu leo kuzaa na huyu kesho kuzaa na yule kesho kutwa kuzaa kwingine, au kubeba mimba ya mtu na kumsingizia mwingine asee hapana....mabinti sijui wanakwama wapi kwanini uzae zae ovyo ovyo na uone ni kitu cha kawaida
Acha wazae tu dunia ibalance.
Kuna ambao hawana uwezo huo.
Wanasaidiwa na Hawa unaowaita wanazaa ovyo
 
Pia ayo mavidonge wanayotumia uko mbeleni pindi watapokuwa kwenye ndoa kuna uwezekano mkubwa sana kutozaa
Sasa tutafanyaje mkuu?
Na mbususu tunataka kuzichakata?
Ni either tuzae Sasa au asizae mbeleni.
 
Mitaani single mothers wanaolewa kila siku,ni mitandaoni tu ndiyo wanapigwa mawe.
 
Back
Top Bottom