Elections 2015 Kama hii ni kweli, then serikali yetu ni serikali dhalimu na haramu? Hukumu ya karma ijuu yake!

UKAWA hawana kura za kuibiwa.

wakubali matokeo waingie bungeni ,wajiandae kwa uchaguzi wa serikali za mitaa 2019.

Na CCM ya Magufuli sijui kama itakuwa kama CCM ya Kikwete.Wasubiri mwingine atakayekatwa 2024.
 

Mkuu uko sahihi kabisa na kila siku tuwakumbushe hawa watanzania milioni 6 waliompigia kura kuwa walitaka kutupeleka pabaya!
 
hakika malipo mikononi mwa kikwete na genge lake,na magufuli anayedai ameokoka mungu atajibu tu kwa kuwa haki ya mtu haidhulumiwi hapa duniani
 
yan mkuu Pasco uwa nakusalute sana ila leo umekuwa mnafiki.Mwanzoni unasema "Kama ni kweli" kwa manaa kwamba huna uhakika na lililosemmwa na Edward,lakini baadae unashindwa kuficha hisia zako na kutoa hukumu na kusahau kabisa kuwa umesema "Kama ni kweli".

Kwa mfano unasema wale wote wanaoshangilia ushindi dharimu.etc na wenyewe wataadhibiwa na Rhe law of Karma,hapo inaonyesh tayari kuwa na wewe unaamini kuwa kulikuwa na figisu halafu unajidai "Kama ni kweli",Huo ni UNAFIKI, PASCO HAPO UMEKUWA MNAFIKI na wewe pia na Wanafiki kama wewe hiyo Law of Karma haitawaacha pia.
 
Ni lini wapinzani waliwahi kukubali matokeo nchi hii?Hizi ngonjera zilitegemewa tu na wala siyo habari tena.CDM wenyewe demokrasia kwenye chama chao imewashinda huo ujasiri wa kuinyoshea vidole NEC wametoa wapi?Hivi kama demokrasia isingelawitiwa ndani ya CDM huyu mzee angegombea kupitia chama hicho?Bora akae kimya tu maanake hata yeye mwenyewe kagombea kwa demokrasia hiyo hiyo iliyopigwa mtungo.
 
Mkuu uko sahihi kabisa na kila siku tuwakumbushe hawa watanzania milioni 6 waliompigia kura kuwa walitaka kutupeleka pabaya!
Tusilaumu sana,najua ni nguvu ya Fedha na kumbuka jamaa ameanza muda mrefu sana.Kahonga makanisani na misikitini.Yaani kuna waumini nilikuwa nakutana nao hususani wa Gwajima wanamwona Lowassa kama mtume vile.Fedha ni kitu cha ajabu mkuu.
 
Mm nimeshaanza KUFUNGA KWA MAOMBI....!!! Kama ni ushindi wa haki, MUNGU hatatoa ADHABU...!!!

Kama ni USHINDI wa DHULUMA, MUNGU ataangamiza watu, hadi wakome...!!! Narudia, Mungu ataangamiza wahusika hadi wakome...!!!

In Jesus name...!!!

Umechelewa sana, ulitakiwa kufunga na kuomba kabla ya kampeni hazijaanza ila kwa sasa it's too late
 
Huyu jamaa mnafiki kitambo,huwa anataka aonekane hana upande ilhali maandishi yake yote yana upande.Pasco,huzuiwi wala hutashitakiwa kwa kuwa na upande unaouamini,issue ni unafiki siyo deal WOTE HUMU TU WATU WAZIMA mazee.
 

Hapa ndo udhaifu wa mwafrika ulipo. Hatukubali matokeo. Tunatafuta kila sababu ili tu tuonekane tumeonewa ili tuwaridhishe washabiki wetu.

Washabiki wote wa Lowasa lazima wawe wakweli na mmwambie ukweli Edward Lowasa kuwa Kura hazijatosha. Hizo kura million 10 anazosema amepata wekeni tu mfano wa majimbo matano ya kuonesha tofauti ya kura zilizohesabiwa na kusainiwa majimboni na zile zilizosomwa na tume ya Uchaguzi.

Wakati matokeo ya Ubunge majimboni yakisomwa hakuna hata mmoja aliyekuja na mfano hata mmoja. Zimekuwa zikitengenezwa tofauti za kuumba (Tunduma na Bumbuli) ambazo zote zimekuwa debunked na rekodi sahihi za tume na majimboni.

Kama EDO anajua kuna wizi na anajua ulivyofanyika; aje na mifano ya rekodi, siyo sweeping statements kwamba alipata kura million 10. Kampeni za mijini tu kwenye wapiga kura 30% na kununua media (TV na Magazeti) haitoshi. Unahitaji wapiganaji on the ground. Hakuna vita ambayo imeshawahi kushindwa kwa kutumia air power na pyschological warfare peke yake. You need ground solders. Hao maeneo mengi ya nchi hawakuwepo; ukiachana na mikoa miwili ya Arusha na Kilimanjaro pekee.

Edo is dangerously polarizing na hilo ni mojawapo ya matatizo yake makubwa. Wakati ana win hardcore supporters, methods zake vile vile zinafanya apate hardcore opponents. Si mkusanyaji, ni mtawanyaji. Challenge ya kwanza kuunganisha Upinzani alishindwa and he nearly killed Ukawa.

Magufuli hakuhitaji wizi wa kura kushinda huu uchaguzi, wala CCM haikuhitaji wizi wa kura kushinda majimbo mengi. Walichohitaji ni Ukawa iliyokosa mwelekeo. Hakuna mtu hata mmoja aliyeweza kusimamia hoja ya katiba ya warioba na kuielezea vizuri. Hiyo inaonesha kwamba, kampeni ya Edo ilijaa wadandiaji, si watu original waliokuwa wakijua Ukawa inasimamia nini. Matokeo yake walipoteza mwelekeo wakafanya kampeni ya kutoa ahadi; kampeni ambayo haikuwatofautisha na CCM. Wananchi wengi wanajua kuwa hizo ahadi ni uongo na nyingi hazitekelezeki.

Wananchi walitaka kusikia alternative thinking. Edo alitegemea Mbowe, Sumaye na Kingunge kuwa ndo wasemaji wakuu. Ni vigumu sana kuwashawishi watanzania wengi kuwa Sumaye na Kingunge ni watu tofauti na wale waliokuwa CCM. Mbowe watanzania walishamkataa mwaka 2005.

Tulitarajia Lowassa aongozane na Kina Lissu, Mnyika, Mwalim, Lema, Mdee ili kuwaonesha wanachadema wa siku zote kuwa Lowasa ni Chadema. Hilo halikutokea. Watu hao wote walijichimbia majimboni kwao kupigania uhai wao Bungeni.

Kwa kufanya uchambuzi makini usio na chembe ya unafiki, ni wazi hizo kura million 10 anazodai kuzipata Edo ni za kupikwa na washabiki wake wanaotaka kuendelea kufaidi mfuko wake.

Ataheshimika sana hata akikaa kimya tu. Kura milioni kumi akiulizwa ushahidi uko wapi itakuwa kichekesho!
 
Ila Pasco Mungu hatukubalii kukaa tu tuombe bila ya kuitafuta haki yako, Hata kama mtu unamdai unaambiwa umwambie na umkumbushe Mara kadhaa deni lako.

Maombi yawepo na haki itafutwe kama ukiamini umedhulumiwa, zipo njia nyingi zenye kheri za kutafuta haki na uziepuke zenye shari
 
Edward Lowassa ni nani?

Wewe Pasco nnakusihi kaa kimya na ukubali matokeo.

Amini.
sijawahi kuona maajabu ya dunia kama safari hii, kweli dunia inautawala wa shetani, dunia ni ngome ya shetani kuiba haki ya wengi kiasi hiki ni ajabu sana, na huyu si mwingine mwenye roho ya shetani ni huyu huyu Mkuu wa n..c...h...i aibu.
 

Mkuu hizi ni tuhuma tuu na hazina uthibitisho ndio maana nimesema kama ni kweli, ila sijatoa hukumu, nimesema kama ni kweli, then, hao wanaoshangilia haramu, pia nao watakuwa na sehemu yao ya hukumu ya karma!. Yaani kunauwekano kabisa kuwa John Pombe Magufuli is not a part kwa huo udhalimu, ni NEC na CCM ndio wamecheza game yote, kuna Watanzania mamilioni kwa mamilioni wamemchagua Magufuli kwa ridhaa zao na kwa kura halali, hivyo hawa hata wakishangilia ushindi, kwao ni shangilio la haki, bila wao kujijua kumbe ushindi huo umechangiwa na haramu!. Karma iki act, inafuata haki bin haki, unaweza kukuta kwa vile Magufuli hajui kilichofanyika, na yeye anashangilia sweet victory genuinely, karma inaweza kumspare na kuwa strike wale maingeneer wa hii kitu!. Unaweza kukuta masikini hata Jaji Lubuva hajui chochote kuhusu the games people play!, he is very honest and very genuinely anatangaza matokeo aliyoletewa aiamini ndio ya kweli kumbe ni cooked!. Then hata yeye karma itamspare!, tatizo la karma, when it strikes, haitoi reference inastrike kwa lipi, kazi yake ni kutoa tuu hukumu ya haki kwa mapigo humu humu duniani. Yaani kila mtenda mema, atalipwa mema, na kila mtenda maovu atalipwa maovu!. Huku sio kuhukumu bali kuwaeleza Watanzania wenzangu, pia tujiweke tayari kwa matokeo ya karma!.

Na niliposema kama ni kweli sikuishia hapo, jee uliosoma huu mstari
Ila pia, endapo tuhuma hizi ni za uongo, ni za kupika na ni uzushi, then John Pombe Magufuli, ndiye chaguo la Mungu la rais wa Tanzania aliyetangazwa mshindi siku yake ya kuzaliwa!, hivyo atasimama test in time, of which time will tell!.
Pasco
 
Badala ya kukaa chini mrekebishe kasoro zenu mnaanza kutafuta wa kutupia LAWAMA.CCM YA KIKWETE SIYO CCM YA MAGUFULI.2020 MTALALAMIKA TENA PALE MAGUFULI ATAKAPOPETA KWA 85%
 

Amen........
 
Hivi inaingia akilini mtu awe anahutubia mikutano ya kampeni kwa dakika 4 halafu aseme ameibiwa kura! is it logic kweli, tufikie mahali tuwe wakweli tu

Kama kuhutubia dk nyingi ndo kupata kura basi mama Mghwila angepata nyingi kuliko wengi wote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…