Elections 2015 Kama hii ni kweli, then serikali yetu ni serikali dhalimu na haramu? Hukumu ya karma ijuu yake!


Kwenye karma hakuna jema na baya,concept ya wema na ubaya ni concept ya mafundisho ya kimungu.

Unajitahidi kuandika,lakini bias inakufanya ujisahau/ujichanganye.Labda nikuulize;

Unaonaje kama KARMA hiyohiyo ndio inahusika kumfanya Lowassa akose urais kutokana na matendo yake yaliyopita?Think about it.

ANGALIZO:
Mimi siegemei upande wa chama chochote,bali huwa napenda watu wapate elimu sahihi kwenye nyanja mbalimbali za kielimu ikiwamo elimu hii ya siasa.Sipendi watu wawe washabiki pasipo kuelewa msingi wa jambo.
 

Nakukubali sana Deception kimsingi upo sahihi kabisa...
 

Umenena vema
 
Mkuu uko right, karma inafuata mising ya cause and effects, na ukiishamaliza kulipa, unakuwa set free!, mimi niliamini Lowassa aliishailipia bad karma yake kwa wema alioutenda na kidogo iliyobakia ndio hiyo anayoendelea kuilipa kwenye hali ya afya yake!, hivyo by the time anagombea, he is a clean man out of bad karma!, ila pia it is possible maovu yake yalikuwa yamepitiliza hivyo ameyafidia kwa kuukosa urais!. With karma!, no one can tell, ndio maana nimemaliza kwa kauli hii
Ila pia, endapo tuhuma hizi ni za uongo, ni za kupika na ni uzushi, then John Pombe Magufuli, ndiye chaguo la Mungu la rais wa Tanzania aliyetangazwa mshindi siku yake ya kuzaliwa!, hivyo atasimama test in time, of which time will tell!.

Pasco


 
hamna ukweli wowote katika kijitamko cha lowasa, kashindwa uchaguzi kwa sababu zilizo wazi kabisa ambayo kubwa ni yeye aliwekeza zaidi katika viini macho vya mafuriko na maigizo, wakati CCM wao walikazia nguvu zao kuwasaka wapiga kura walipo.
Tunamtaka atulie kashashindwa atulie watu tuendelee na kazi zingine.

 
Wizi haujafanyika this time, na hii ni kutokana kwamba wale wezi wa kura akina Kingunge na Matson Chizi kuajiriwa upande mwingine kwa kazi hiyo

hata kwa kumbukumbu za uchaguzi uliopita, kulikuwa na tuhuma za wagombea wengi kununuliwa na hata mbunge aliyepita wa Arusha alithibitisha kutaka kununuliwa na kuachia jimbo. sasa tuhuma hizi za sasa labda ni kwa kuzidiana akili
 
Anaesema serikali ya awamu ya tano haramu, basi yeye ndiye haramu, huwezi kutukana Rais ayechaguliwa na Watanzania wengi kwa manufaayako

Watu wenye hofuya serikali ya Magufuli ni
1. Wala rushwa
2. Wazembe
3. Wababaishaji
4. Wakwepa kodi
5. Wakumbatia wafisadi
6. Maslahi binafsi
Hivyo wanajaribu kufanya propaganda ili wale wasiojilewa vizuri wafikirie kuna ukweli katika uongo wao
 
Kama 10,268,795 ni kweli za Lowassa basi jibu la watu kutokuwa na Bwembwe za Ushindi kwa sababu waliowengi wamepokwa haki zao

Inakuwaje watu washinde halafu wanazunguka wachache na tena wanaonekana wamepewa chochote?
 
Mkuu sana Pasco, kwanza hongera kwa "chama chako" kutangazwa kimeshinda uchaguzi mkuu.

Ingawa ushindi huu kwangu mimi ni kukataa agizo halali la Mungu.

Rejea maneno haya "Lakini neno hilo likawa baya machoni pa Samweli, waliposema, Tupe mfalme atuamue. Naye Samweli akamwomba BWANA. BWANA akamwambia Samweli, Isikilize sauti ya watu hawa katika kila neno watakalokwambia; kwa maana hawakukukataa wewe, bali wamenikataa mimi, ili nisiwe mfalme juu yao."(1 Samweli 8;6-7)

Mkuu wangu sana Pasco, wana wa Israel walifika kipindi Cha Uchaguzi. Mwamuzi wao( Aliyekuwa akifanya kazi za kifalme) Samwel ilikuwa ndiye asimikwe kuwa Mfalme. Lakini wana wa Israel walimkataa Samwel. Wakataka wamchague wanaye mpenda wao. Mungu akasema Waache waendelee kuchagua, wamenikataa mimi(Mungu).

Maisha kadiri yalivyokuwa yakienda ikaja kugundulika kuwa Sauli ni Mfalme wa hovyo kuliko wafalme waliowahi kuwepo katika zama hizo. Kwanini? Mungu aliwaacha.

Naliona hili Tanzania. Nimeanza kuliona hili tangu 2006-2015 NA LITAENDELEA HIVI HIVI HADI 2025. Kwa nini? Tumeidharau sauti ya Mungu! Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu. Laana huja baada ya kuikataa sauti ya Mungu kwa kutotenda HAKI.

Biblia inasema HAKI HUINUA TAIFA...Bali dhambi ni aibu kwa watu wote. Tutegemee aibu kama hizi tuzipatazo sasa,deni la taifa, uchumi kuzorota, kutumia mabavu kisiasa, kuiba fedha kama Escrow na mengineyo mengi. Kwa nini? Tumeikataa sauti ya Mungu.

kaka Pasco, Miaka ya mwanzoni Sauli alifanya vizuri. Miaka iliyofuata ilikuwa ya laana. kila vita wanashindwa, mambo hayaendi hadi alipopatikana Daudi "kwa mbinde" nchi ndipo ilianza kuneemeka.

Hata sisi, ni hadi tutakapompa uongozi Daudi, tutaacha kulia. Kwangu mimi Magu ni Sauli.

NB:Out of Topic: Vipi usalva ndio ushapeperuka? "Au home boy atakufikiria?"
 
Last edited by a moderator:
Hivi nafsi yako inajisikiaje pale unapoongoza watu wasiokuhitaji na hawakukuchagua,shame!
 
Kila jambo lina mwanzo na mwisho wake,

"Power tends to corrupt, and absolute power corrupts absolutely. by John Emerich Edward Dalberg Acton, first Baron Acton (1834?1902).
 
Unaweza kutoa uthibitisho hadharani?

Hat kipofu anaweza. Na tume wanalijua hilo. Ndiyo maana wakaharakisha kumtangaza mshindi. UKAWA tunazo fomu zilizosainiwa na mawakala nchi nzima ambazo zilitakiwa kutumiwa na tume kutangaza matokeo.
 
ni maneno mazuri sana pasco ya kutuasa.ila pia tuupe muda nafasi!!!i still don't believe mambo yanayoendelea baada ya uchaguzi huu.ni kama tupo vitani wanajeshi na polisi wametanda kila mahali!!!
 

Post zako nyingi sana zina mashiko,lakini inanisikitisha sana kwamba kuna jambo moja ambalo linafanya yote hayo unayozungumza yakose tija.Jambo hili lisingekuwapo,basi yale unayozungumza yangekuwa na maana na tija kubwa kwa watanzania.
-Jambo hili ndilo lililonifanya nisipoteze muda kujiandikisha kupiga kura kwa muda mrefu sasa ingawa wengi wanaonifahamu walinipinga.
-Jambo hili ndilo linalofanya mchakato wa katiba mpya usifanikiwe.
-Jambo hili ndilo linalofanya hata baadhi ya vifungu katika katiba ya sasa visifuatwe.
-Jambo hili ndilo linasababisha mambo mengi machafu yasiyo na idadi kiasi cha kushindwa kuyaweka yote hapa ubaoni.

Jambo hili ni 'watu wanaotuongoza nyuma ya pazia' au naweza kusema 'dark government'/serikali isiyoonekana.Watu hawa si ule mfumo wa CCM kama wengi wanavyofikiri na wala si usalama wa taifa.Hawa ndio wanaomuweka rais wamtakaye madarakani,na hata wakimuweka rais aliyechaguliwa na wananchi basi lazima afuate matakwa yao kwenye mambo mazito mazito yanayohusu uchumi.Watu hawa wana elimu ya juu zaidi kuliko sisi.

Jambo hili wengi hulidharau na kulichukulia kama ni hadithi za Abunuasi kujenga nyumba angani.Ndio maana hatufanikiwi kwa muda mrefu sana katika masuala ya kisiasa na uchumi kutokana na kilema hiki tulichonacho cha kutojua ukweli huu.Cha msingi ni kujua kiini cha tatizo,halafu ndio tujue jinsi ya kulitatua tatizo.Sina maana kwamba hatuwezi kushindana na watu hawa,bali elimu na ujuzi wa kiini cha tatizo ndio msingi wa utatuzi,sisi hatujui kiini cha tatizo,tunagusa juu juu tu.

Hili ni suala pana sana,linanipa uvivu kuandika kila kitu.Lakini tutake tusitake,ukweli ni kwamba rais wetu akiwa na urafiki na watu hawa lazima awe adui na wananchi wake,vinginevyo,rais wetu akiwa rafiki wa wananchi wake,basi lazima awe na uadui na watu hawa.Ukiwa na urafiki na watu hawa,kamwe huwezi kushitakiwa na kuhukumiwa kwenye ile mahakama ya kimataifa bila kujali kama umeua watu wangapi nchini kwako.Watu hawa wakisema wanamtambua Lowassa kama rais basi atakuwa rais,wakisema wanamtambua Magufuli kama rais basi atakuwa rais.Wananchi hawana maamuzi juu nchi yao.(Rejea statement ya Joseph Stalin wa Urusi ya zamani kuhusu wananchi na uchaguzi).

Tuko gizani,ukombozi pekee tulionao sasa ni elimu sahihi kuhusu kiini cha tatizo,na si ushabiki.Tusidanganyike kwamba eti serikali yetu inasaini mikataba mibovu,ukweli ni kwamba serikali inasainishwa mikataba mibovu,haisaini kwa ridhaa yake.Nani anaijua mikataba ya madini mfano gesi na urani?Mkiijua mtalia sana,ni bora msiijue ili muishi kwa amani rohoni mwenu.Nani anajua kwanini Kiwete alikwenda sana Marekani kabla ya uchaguzi?Sehemu kubwa sana za muhimu katika nchi hii zimeshauzwa na nyingine tumesainishwa mikataba inayodumu kwa zaidi ya miaka 80 au 90?Kiini cha tatizo ndio mpango mzima.

Huwezi kutatua tatizo kwa kutaka katiba mpya bila kujiuliza kwa nini hata ile iliyopo haitekelezwi.Kama watu wanakiuka hata mafundisho ya Mungu wao kwenye misaafu,itakuwa katiba iliyoandikwa na binadamu?

Mifumo katika sekta ya elimu,afya,madini,kilimo na viwanda imekamatwa kisawasawa na watu hawa.Huwezi kuboresha sekta hizo nilizozitaja kama una urafiki na watu hawa.Wapo waliowahi kupingana na watu hawa lakini hivi sasa hawapo kwenye uso wa dunia.Najua pia kwamba kuna udhaifu binafsi wa viongozi ambao hauchangiwi na watu hawa,lakini ukweli unabaki palepale kwamba watu hawa ndio wameshikilia sehemu kubwa muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu.

Huu ndio mfumo/utawala ulio nyuma ya pazia/dark government ambao ndio unaathiri hatua yoyote ya kimaendeleo nchini kwetu.Kikwete alijiamini sana kwamba CCM watashinda kutokana na kuahidiwa na watu hawa.

Mambo yaliyojificha yanayoonesha kwamba hawa viongozi wetu wana ujamaa na watu hawa;
1.Angalia Kikwete jinsi anavyosalimiana na Obama,halafu linganisha na Kikwete jinsi alivyo grip mkono wake na Magufuli jana.

2.Angalia Uhuru Kenyata jinsi alivyosalimiana na Obama na John Kerry.

3.Fautilia Kikwete jinsi alivyosalimiana na Uhuru Kenyata.

Haya ni kwa uchache tu.Watu wanaweza kuona kama ni maigizo,lakini haya yanaashiria kuna nguvu kubwa inayotutawala,tusipopata elimu sahihi kuhusu jambo hili tutaendelea kutawaliwa milele huku tukibaki kufanya ushabiki wa vyama vya siasa kama ilivyo kwenye soka.
 
Mkuu The Boss, siku nilipokujibu bandiko hili, sikumbuki kama nilijibu hoja yako ya triple vowels, it's not just a coincidence but it has something to do with numerology, japo nimeisoma kidogo na astrology na palmistry nilishindwa kwenda deep kutokana na imani yyangu kwenye Christianity.

Paskali
 
Mkuu The Boss, siku nilipokujibu bandiko hili, sikumbuki kama nilijibu hoja yako ya triple vowels, it's not just a coincidence but it has something to do with numerology, japo nimeisoma kidogo na astrology na palmistry nilishindwa kwenda deep kutokana na imani yyangu kwenye Christianity.

Paskali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…