Kama hila ya Wazungu kupitia chanjo ni kutumaliza, basi tusitie kiburi leo, tumechelewa, tangu utotoni tumechanjwa sana na chanjo zao

Kama hila ya Wazungu kupitia chanjo ni kutumaliza, basi tusitie kiburi leo, tumechelewa, tangu utotoni tumechanjwa sana na chanjo zao

Kama unataka kujua unafiki wa viongozi wa serikali hii, hiyo chanjo ije uone kama hawajaenda kuchanjwa usiku.
 
Hahaha look at you man.. for those who see beyond.
I applied logic.. not random theory.
Logic gan😂😂, tatzo bongo ka mtu kana degree flan kanahis ndo ka genius tz nzima, uzr hi n art ingekuw science tungeshusha calculation na principles hapa tuone anayekula Kona😂😂
 
Logic gan[emoji23][emoji23], tatzo bongo ka mtu kana degree flan kanahis ndo ka genius tz nzima, uzr hi n art ingekuw science tungeshusha calculation na principles hapa tuone anayekula Kona[emoji23][emoji23]
Hahaha kuna mahali nimejiita geniuz.? Kuna mahali nimestate educational background yangu nope.

Dont be delusional man , ku assume character ya mtu wkt humjui unaonekana delusional.
Chill & relax.. si lazima wote tufanane.
 
Injinia soma iyo
Wazungu kwani tumewakosea nini hatu watufute kwenye sura ya dunia?
Walitupeleka utumwani, tukatumika kwa utii mkubwa, walitutawala na kuitumikisha huku wakipora utajiri wetu hatukupinga.
Sasa shida ni juu ya Nini Tena?
IMG-20210129-WA0050.jpeg
 
Hahaha kuna mahali nimejiita geniuz.? Kuna mahali nimestate educational background yangu nope.

Dont be delusional man , ku assume character ya mtu wkt humjui unaonekana delusional.
Chill & relax.. si lazima wote tufanane.
Anyway mengine maybe n mitazamo ya mtu, like religions, ( Christians, Muslims etc)
 
Wasubiri kwanza TUFE ndo waje na chanjo zao kwa Sasa hatuwezi kuwaelewa
 
Una mawazo mazuri ila tambua hofu ya baadhi ya nchi za kiafrika ni kwamba sisi ni nchi ambazo hatujaua wengi kama wao wenzetu na isitoshe kwann hawajaanza kwao ambapo wanaumwa wengi na ugonjwa huo upo kwa kasi! Watuonee huruma sisi kivip?
Lazima wakati mwingne unatakiwa ufikirie mbali hili jamboo kwasababu wazungu sio watu wazur kabisa kwetu uzur wao kwetu ni unyonyaji!
Kwaio mzungu siku zote atakaa na wewe kwaajili ya kitu fulani ila kama unaubongo wa kulala siku zote utajua madhara yake baada ya miaka 10 au 20 !
 
Polio, ndui, kifaduro, pepopunda, TB, nk ni chanjo ambazo wengi wetu tumechanjwa utotoni. Na huenda kupitia chanjo hizo ndiyo sababu ya kuwa hai hadi leo tunapotunisha misuli majukwaani.

Halikadhalika ukienda kwa upande wa Mifugo,kuna chanjo nyingi mifugo yetu huchanjwa kukinga magonjwa mbalimbali. Hivyo chanjo ni kitu muhimu kwa binadamu na wanyama hasa kwa magojwa yale yasiyotibika kwa tiba za kawaida.

Kwa uelewa wangu,zaidi ya 99% ya chanjo hizo za binadamu zimetengenezwa nje ya nchi( hasa ulaya) kupitia uangalizi wa Unicef na WHO. Ni nani aliwahi kuhoji kuhusu usalama wake? Na kama alihoji,ni hatua ,zipi za Serikali zilichukuliwa kupata mbadala wake? Na je, viongozi wa awamu zilizopita wangeamua kusitisha kuziingiza nchini, nini kingetokea?

Tumesikia kwenye vyombo vya habari kuhusu ligi inayoendelea kuhusu chanjo ya Covid- 19 hasa kwa nchi zetu changa kupanga kuikataa. Kuna taarifa zisizo rasmi kuwa, kwa nchi changa, hofu siyo aina ya chanjo bali ni gharama kubwa za chanjo hiyo. Na yawezekana, ingetolewa kama msaada kama zile za Unicef kwa chanjo za watoto tusingesikia haya yote.

Kama ndiyo hivyo yaani kuogopa gharama,viongozi wetu wanapaswa kufahamu kuwa kipaumbele cha serikali yeyote ile kwa watu wake ni kulinda maisha yao! Kenya na baadhi ya nchi zinazotuzunguka wameshashaagiza au kuweka mipango ya kupata chanjo hiyo. Ni rai yangu kuwa,,nasi tuwe kwenye mstari wa pamoja na jirani zetu.

Na kama ipo agenda inayolenga kufafanua madhara yake,tucampaign kwa pamoja kuikataa. Mwl. Nyerere alipogundua IMF inayumbisha nchi maskini, alihamasisha na kuungana na nchi nyingi kuyakataa masharti ya IMF wakiwemo Nigeria ya kina Sani Abacha w, Zambia ya Mzee Kaunda
nk.

Hiyo approach ilifanya Wenye IMF kutikisika na kuanza kufuta baadhi ya misaada. Naamini hata viongozi wetu wa nchi hizi changa wanapaswa kutumia technique hiyo ya umoja pale wanapogundua kuna genuine reason ya kukataa jambo,na hapohapo wawe na mbadala. Covid-19 au 21 ni janga zito na siyo la kuisha leo wala kesho.

Siyo jambo la afya sana viongozi wa nchi zetu changa kuanza matamko ya kukinzana na juhudi yeyote ya awali ya kukabili tatizo la covid kama chanjo kwa staili ya majukwaa mepesimepesi.
Nyakati zinabadilika, mitazamo hubadilika, malengo hubadilika..... Kimsingi watakuwa kuchukua tahadhari kubwa sana kwa sasa. Ongezeko kubwa na la kasi la watu duniani ni tishio kwa viranja wakuu wa dunia. Tusisahau kuna watu wanaiendesha dunia kwa RIMOTI hivyo wanaweza amua chochote....wataumia wao na sisi weusi pia.... Km ndivyo ni mpango wa kidunia hakuna aliye salama ila weusi usalama wetu ni mdogo zaidi ya wao.
 
Wazungu kwani tumewakosea nini hatu watufute kwenye sura ya dunia?
Walitupeleka utumwani, tukatumika kwa utii mkubwa, walitutawala na kuitumikisha huku wakipora utajiri wetu hatukupinga.
Sasa shida ni juu ya Nini Tena?
Fuatilia magazeti na vyombo vya habari vya hao wanaoitwa mabeberu nao hawaitaki chanjo. Wameanza kuipinga kwa nguvu zote wakiamini ni mpango wa nguvu wa kupunguza wingi wa watu duniani.si Afrika pekee
 
Cerelac (food stuff) , yellow fever, measles, ARVs, condoms etc

Lakini wanaoipinga hii chanjo ya COVID sio kwamba hawaitaki kabisa ila wanahoji uharaka wake. Testing & approval processes zimekuwa fasttracked kwa speed ya ajabu na hakuna mwenye uhakika kama hakuna potential long term effects. Harafu zile note kama “not to be used in USA & Canada” zimetisha sana.

Hao wazungu hawasemi kama ukishachanjwa tu then huna haja ya kuvaa barakoa tena na kwamba hutopata tena COVID19

View attachment 1689641
IMG-20210131-WA0003.jpg
IMG-20210131-WA0003.jpg
 
Kwani kwa muda wote uo Africa nzima washindwe ata kushirikiana kutengeza dawa..wasomi wako weng ktk kila nch kwanin wasiungane kukabili majanga ya ghafla kama hya...au ule ushirikiano kama umoja wa Africa na mengine yanadili zaid na nin mambo ya kisiasa tu au nao wanatumika...
 
Nyakati zinabadilika, mitazamo hubadilika, malengo hubadilika..... Kimsingi watakuwa kuchukua tahadhari kubwa sana kwa sasa. Ongezeko kubwa na la kasi la watu duniani ni tishio kwa viranja wakuu wa dunia. Tusisahau kuna watu wanaiendesha dunia kwa RIMOTI hivyo wanaweza amua chochote....wataumia wao na sisi weusi pia.... Km ndivyo ni mpango wa kidunia hakuna aliye salama ila weusi usalama wetu ni mdogo zaidi ya wao
Kama unataka kujua unafiki wa viongozi wa serikali hii, hiyo chanjo ije uone kama hawajaenda kuchanjwa usiku.
Umenichekesha. Nimekumbuka kikombe cha Babu wa Loliondo.
 
Wazungu kwani tumewakosea nini hatu watufute kwenye sura ya dunia?
Walitupeleka utumwani, tukatumika kwa utii mkubwa, walitutawala na kuitumikisha huku wakipora utajiri wetu hatukupinga.
Sasa shida ni juu ya Nini Tena?
Kweli ni Wazungu waliopeleka watu utumwani? Si wafalme na machifu wenyeji waliokamata watu na kuwapeleka utumwani? Halafu kuwauza kwa Waarabu na Wazungu waliowanunua wakiwa watumwa tayari? Na hao kuwapeleka mbali hadi jehenam ya Marekani? (Nikumbushe: walioanza kupinga utumwa walikuwa watu wa wapi??)
 
Back
Top Bottom