Habari zenu wana jamiforum ,hakika hili jukwa linazidi kuwika kila siku maana kila unachohitaji kujifunza kipo hapa .
TWENDEE KWENYE MAADA.
Katika harakati za kufanya biashara yangu ya dagaa nilipata mteja mmoja ambae sijawahi na sikufikiria kuwa inaweza kuwa hivyo maana mambo ya ushirikiana kwenye biashara nikikuwa siamini sana maana ukitoa shule sana sana chuo huamini ushirikiana kwenye biashara ila unaamini kwenye mahesabu tuna na kusema uta chomoka na ilikuwa hivyo kwa muda mrefu tangu nianze hiyo biashara siamini ushirikiana.
Yule mteja alikuja kanunua mzigo vizuri kwangu na kuahidi nitapewa hela baada ya siku nne kunipa hela yangu yote alikuwa ni MCONGO,nikafurahi kweli maana nimepata mteja amechukua mzigo wote kwa haraka kama mnavyo wajuwa wacongo anachukua mzigo mkubwa,Akachukua na kwa wengine mzigo hivyo hivyo kuwa atatulipa baada ya hizo siku,hakuna aliye pata shaka kwa hilo maana imezoweleka hapa wanachukua mzigo na kutoa hela zote akishamaliza kabisa kukusanya mzigo anaohitaji.
Baada ya siku nne kweli huyo mteja alikuja kulipa pesa kwa kila mtu ambae alikuwa anamdai hela ya mzigo mida ya jioni kabsa wanafunga soko ,maana alidai gari yake ya mzigo inaanza safari muda huo kuelekea mipakani kwenda huko congo.,.
Ile hela sasa niliyo pewa ule muda iligeuka kilio kwangu, nikaweka kwenye ule mfuko wa plastic ambayo ishakatazwa na serikali isitumike kwa kipindi hicho bado inatumika na kwenda nyumbani nitunze ili kesho niamke niende kisiwani kufuata mzigo mwingine maana ulikuwa umeisha ofsini.
Asubuhi sasa naamka niende niwahi BOTI kwa huku kanda ya ziwa imezoeleka kama usafiri wa FERRY kuelekea visiwani nikusanye mzigo ,nikachukua ule mfuko ambao nilitunzia hela zangu nikafungua ili nitoe hela nizipange na nyingine nitoe kwa matumizi ya nyumbani .
Sikuamini nichokiona ndani pale ni karatasi tupu mfumo gazeti ndio zimejaa humo tupu laaaa nilidhani naota lakini kumbe ni live bila chenga nilivurugwa tumbo la kuharisha huku jasho inakaribia nayo kwa kasi akili ikiwa inawaza nipige yowe.
Haija kaa sawa simu ikawa inapigwa na moja ya mfanya biashara mwenzagu tulie muuzia yule mteja mzigo anatoa sauti kama ya mtu anaetaka kutoa kilio ,mimi mwenyewe sauti za kilio kama chake ananipa habari kama niliyo ikuta mimi kwenye hela.
Kumbe janga kila aliye chukua hela ya mtu yule na siku ile asubuhi ilibadirika.
Fuatilia ile gari bana wee maana tuliamini haijavuka boda kwa muda ule gari haikupatikana popote pale wala mipakani sijui nayo ilikuwa gari ya mchongo laaaa.
Kama hufanyi au hujaanza biashara huwezi amini ushirikina upo tena kiwango cha juu.
POLE KWA KUSOMA UZI MREFU LAKINI TUNAPEANA MACHANGAMOTO KWENYE KAZI ZETU.
KAMA UMEWAHI PATA CHANGAMOTO YOYOTE INAYOHUSIANA USHIRIKINA KWENYE KAZI ZAKO TUNAOMBA KWENYE COMMENTS HAPO CHINI.
KARIBU MWANZA DAGAA ZIPO KAZI INAENDELEA KAMA KAWAIDA TUSHASAHAU MACHUNGU NI MIAKA MINGI.
0657886964