Kama hujajipanga vizuri usichokoze ujenzi

Ulichosema ni kweli kabisa, huu upuuzi niliukataaa, fundi akinipa hesabu, ikipungua nakuwa mkali zaidi ya pilipili, sema sijengi kwa stress
 
Ndugu uko moro mjini? Kama uko moro mjini naomba uniunganishe nanhuyo fundi wako maana nami nataka nilianzishe
 
Hapo kwenye tofali 5000mbona nyingi sana mkuu bungalow hilo!??
Hapo ndio watu wanapoliwa, ukitaka kujenga kwanza jifunze ujenzi kidogo ili uwe na idea ya idadi ya tofali, mifuko ya cement na nondo, hapo utaibiwa kidogo sana. Mm ninapojenga huwa napiga estimates zangu za tofali, cement na nondo, fundi akija na estimates tofauti namuuliza kulikoni
 
Well said
 
U r wromg ndugu, idadi ya tofali za kuchoma haiwezi kuwa sawa na tofali za block, nyumba ya tofali 2000za block inaweza kula tofali 10,000 za kuchoma
 
Usitufokee.
Huyu hajafoka ameongea ukweli, tatizo letu tunajenga nyumba ambazo hatuna uwezo nazo, ndio maana mafundi ujenzi, mama ntilie, madereva wanaweza kujenga kwa sababu wanajenga nyumba wenye uwezo nazo, wewe mtu mshahara 1.5m unataka kujenga gorofa, kweli? Ukijenga nyumna ambayo inaendana na kipato chako stress zitakuwa kidogo
 
Hapa ndo nipo site napambana,tutavuka tu hakuna cha kuogopa kikubwa ni kuomba Mungu atupe pumzi na mafanikio tu mengine yataji-set.

Nataka niende nayo mpaka kwenye paa kisha nikimbie kwanza.
 

Attachments

  • MVIMG_20220823_095333.jpg
    1.7 MB · Views: 64
  • MVIMG_20220823_101804.jpg
    1.3 MB · Views: 61
Hapa ndo nipo site napambana,tutavuka tu hakuna cha kuogopa kikubwa ni kuomba Mungu atupe pumzi na mafanikio tu mengine yataji-set.

Nataka niende nayo mpaka kwenye paa kisha nikimbie kwanza.
View attachment 2332118
room ngapi hii boss ? paa inakula bati na mbao kiasi gani ? upo hatua nzuri ,natarajia mwezi ujao Mungu akijaalia na mi ntafika hapo
 
Hapo fundi maiko kahusika kwa asilimia [emoji817] ila hongera mkuu
 
room ngapi hii boss ? paa inakula bati na mbao kiasi gani ? upo hatua nzuri ,natarajia mwezi ujao Mungu akijaalia na mi ntafika hapo
Rum tatu moja master choo kimoja na bafu na sitting room pamoja na baraza mbili,tofali 1,700 cement mifuko 61 fundi alipima bati ni za Mita tatu 72 pcs na za kofia 7pcs.

Kwenye lintel nondo 19pcs 12mm 7pcs 10mm 12pcs,Mbao 2x2 120pcs na 3x2 80pcs mkanda wa msingi nimezungusha senyenge.
 
Mtu ukishajenga nyumba ikakamilika unaweza kumwelewa yule mzee aliyebomoa nyumba baada ya mtoto wake kumfungia chumbani ili afe kwa lengo la kurithi mali za baba yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…