Kama hujajipanga vizuri usichokoze ujenzi

Kama hujajipanga vizuri usichokoze ujenzi

Siyo kwamba unakuwa huna akiba
Fundi anakuja anakwambia kwa kuanza leta matofali buku yatatosha kwa mfano, nunua na cement mifuko 50 wewe unanunua kila kitu
Wanaanza na hela yao ushAbageini mpak kwenye level flan

Hiyo level haijafikiwa tirio linaisha labda cement au tofali mfano
Kibongo bongo ndo pale tunapojikuta tumeitumia na akiba kwa sababu makadirio ya mafundi wengi hayako realistic na wengi wanapenda kupunguza vitu ili umpe kazi uko mbele sasa unaambiwa ogeza hiki, ongeza kile dah ni huzuni kwa kweli
Ulichosema ni kweli kabisa, huu upuuzi niliukataaa, fundi akinipa hesabu, ikipungua nakuwa mkali zaidi ya pilipili, sema sijengi kwa stress
 
yeah , kama walivyoshauri wadau huipaswi wakati unajenga kutumia mbaka pesa ya akiba inabidi uende taratibu.
- mwaka jana nilianza kumwaga mawe , nikaja msingini na kujenga kiti .nikatulia
View attachment 2323760
- Mwaka huu , mwezi watu nikaanza simamisha kuta nusu nikatulia ilipofika mwezi wa sita nimemalizia kozi zilizobaki, kwasasa nimetulia napiga hesabu namna ya kupiga linta sina presh maana still plan zangu zipo ndani ya muda

- incase mungu akinijalia uzima kufikia mwezi wa kumi na moja ntakuwa nishamaliza na linta na kumalizia kozi za juu zilizobaki . Ila mbaka mwakani mwezi wa saba najua ntakuwa nishapaua kabisaa.
View attachment 2323760
- hii picha chini inaonesha nilipokwamia kwa sasa najua ntatoboa tuu lazima nimiliki mjengo wangu lazimaaa
Ndugu uko moro mjini? Kama uko moro mjini naomba uniunganishe nanhuyo fundi wako maana nami nataka nilianzishe
 
Hapo kwenye tofali 5000mbona nyingi sana mkuu bungalow hilo!??
Hapo ndio watu wanapoliwa, ukitaka kujenga kwanza jifunze ujenzi kidogo ili uwe na idea ya idadi ya tofali, mifuko ya cement na nondo, hapo utaibiwa kidogo sana. Mm ninapojenga huwa napiga estimates zangu za tofali, cement na nondo, fundi akija na estimates tofauti namuuliza kulikoni
 
Endeleeni kukatishana tamaa... Mtaani mama ntilie, muuza matunda, mwenye genge, machinga, fundi viatu hawa wote wanajenga nyumba nzuri tu... Mnaishia kuwaita wachawi freemason majambaz, wakat ukweli ni kwamba wakipata 10,000 basi 6,000 wanaitunza kwajili ya kununua matofali au cement...
Wengi mnasema kujenga ni kugumu kwasabab hamjui nini maana ya ramani, hamjui nini maana ya kiwanja, hamjui nini maana ya materials, hamjui kufanya utafiti wa bei za materials, bei za mafundi wazur wenye uzoefu, hamjui kukaa chini na kumpa masharti fundi (akiyashindwa aache kazi au atakosa malipo), fundi anekuambia zinahitajika cement mifuko 30 kazi ipo katikati anakuambia ongeza mifuko 20 unamchekea chekea tu lazima akuone fala akuchezee akili, kuna watu mnaokota raman hujui ina ukubwa gani [emoji23] hujui lolote unamwambia fundi wew jenga tu ilimradi nyumba ifanane na hii ramani, ktk mazingira haya lazima uone ujenz ni gharama...
Wewe kijana una biashara yako nzuri au una kazi nzuri ya uhakika miaka inazid kwenda upo umepanga chumba kimoja au chumba na sebule kazi yako kumlipa kodi mwanaume mwenzako are you stupid..? Bad enough ukute upo na Familia ktk nyumba ya kupanga... Kujenga ni jambo la kujitambua tu, haina haja kisa unajenga eti ushindwe kunywa bia kula vzuri au kununua nguo... Ni mpumbavu tu anayeweza kuogopa ujenzi mtakufa masikini ktk nyumba za watu...
Well said
 
Uzi wa matajiri huu, majobless hawagusi huku kwa moto[emoji23][emoji23].

Anyway, before ujenzi hakikisha kabisa unajua nn unataka kufanya.

Usikurupuke ktk ujenz.

First of All juwa unahitaji nyumba ya aina gan, una bajeti gan in your hand, pia jua gharama kuanzia msingi mpaka finishing.

Hakikisha unamtafta mtahalamu wa ujenzi akupe full information ya ujenzi kuanzia aina ya ramani, eneo la ujenzi, vifaa vya ujenzi na bei zake, pia gharama za mafundi na ubora wao, bila kusahau muda muafaka wa kukamilisha ujenzi kwa mafundi wanapopewa kazi.

Pia hakikisha unapewa alternative ways za ku avoid gharama za ujenzi, mfano kwa kutumia baadhi ya materials cheap badala ya zile higher price, pia mbadala wa materials mfano kwa baadhi ya mikoa nchin unaweza tumia tofari za udongo za kuchoma badala ya tofali za blocks ambazo ni gharama,

let's say ujenzi wa nyumba mpaka kukamilika ni tofari elfu4, so piga hesabu 1block= 1000Tsh, so 4000blocks will be 4millions[emoji23][emoji23]asee gharama za bati hizi, lkn kama unge avoid kwa njia mkato utanunua tofar za kuchoma zile za 100/200Tsh per one, ambapo kama idadi 4000 basi itakuwa 100×4000 = 400,000Tsh[emoji23][emoji23] ela ndogo sana ambapo unaweza ongezea na zingine za fensi,

Kamwe usijenge kwa kufuata mkumbo, nyumba ni nyumba haijalishi imejengwa kwa tofar gan, lamsingi tutakutana kwenye Finishing[emoji23][emoji23].

Pia hata ktk bati, kama unaona kabisa bajeti haitosh basi usisite kuachana na msouth kamatia bati hiz hizi za kawaida na zipige rangi moja TAAAM ambayo itazuia bati kuchakaa haraka pia kuleta muonekano mzuri.

Mengine jiongeze.
Kamwe usikurupuke kuanza kutafta mafund wakat hujui bei ya siment wala nondo na hujui gharama halali za mafundi ktk level mbalimbali ktk ujenzi.

Na hakikisha huyo mtahalam ama fundi aliyekupa hizi infor hahusiki na ujenzi bali ushauri tu, epuka kupigwa.

Baada ya kujua yote hayo sasa jipange na mahela yako utajua unaanzaje ujenzi awamu kwa awamu kulingana na bajeti yako tena kwa muda sahihi,
U r wromg ndugu, idadi ya tofali za kuchoma haiwezi kuwa sawa na tofali za block, nyumba ya tofali 2000za block inaweza kula tofali 10,000 za kuchoma
 
Usitufokee.
Huyu hajafoka ameongea ukweli, tatizo letu tunajenga nyumba ambazo hatuna uwezo nazo, ndio maana mafundi ujenzi, mama ntilie, madereva wanaweza kujenga kwa sababu wanajenga nyumba wenye uwezo nazo, wewe mtu mshahara 1.5m unataka kujenga gorofa, kweli? Ukijenga nyumna ambayo inaendana na kipato chako stress zitakuwa kidogo
 
Hapa ndo nipo site napambana,tutavuka tu hakuna cha kuogopa kikubwa ni kuomba Mungu atupe pumzi na mafanikio tu mengine yataji-set.

Nataka niende nayo mpaka kwenye paa kisha nikimbie kwanza.
MVIMG_20220823_094934.jpg
 

Attachments

  • MVIMG_20220823_095333.jpg
    MVIMG_20220823_095333.jpg
    1.7 MB · Views: 64
  • MVIMG_20220823_101804.jpg
    MVIMG_20220823_101804.jpg
    1.3 MB · Views: 61
Hapa ndo nipo site napambana,tutavuka tu hakuna cha kuogopa kikubwa ni kuomba Mungu atupe pumzi na mafanikio tu mengine yataji-set.

Nataka niende nayo mpaka kwenye paa kisha nikimbie kwanza.
View attachment 2332118
room ngapi hii boss ? paa inakula bati na mbao kiasi gani ? upo hatua nzuri ,natarajia mwezi ujao Mungu akijaalia na mi ntafika hapo
 
Hapo fundi maiko kahusika kwa asilimia [emoji817] ila hongera mkuu
 
room ngapi hii boss ? paa inakula bati na mbao kiasi gani ? upo hatua nzuri ,natarajia mwezi ujao Mungu akijaalia na mi ntafika hapo
Rum tatu moja master choo kimoja na bafu na sitting room pamoja na baraza mbili,tofali 1,700 cement mifuko 61 fundi alipima bati ni za Mita tatu 72 pcs na za kofia 7pcs.

Kwenye lintel nondo 19pcs 12mm 7pcs 10mm 12pcs,Mbao 2x2 120pcs na 3x2 80pcs mkanda wa msingi nimezungusha senyenge.
 
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787]
Unaweza kufa na nyumba ukaacha hapo, otherwise jenga bila haraka, kwa awamu na taratibu uta enjoy

Ukifikia level vitu vya kingereza uwiiiiii ni stress juu ya stress hasa kama unafosi nyumba kuisha na budget yako ni ndogo

Hongereni watu mnaomiliki mabangalooooo

Hongereni mnaomiliki ghorofa
Mtu ukishajenga nyumba ikakamilika unaweza kumwelewa yule mzee aliyebomoa nyumba baada ya mtoto wake kumfungia chumbani ili afe kwa lengo la kurithi mali za baba yake.
 
Back
Top Bottom