Kama huna elimu ya juu mafanikio utayasikia tu kwenye tv

Tumuulize Lizer kwanza ana PHD ngapi na ni KWANN ni billionare?
 
Acha kuaminisha watu uwongo..wenye elimu ndo hao wanasota mtaan

Me na ufundi cherehan wangu nina mafanikio kuliko hao waliosoma

naomba nfundishe ufundi cherehan
 
Mfano, anaecheza mpira, hata kama hana elimu ya msingi atatoboa, namalizia! "life is a game, play it "
 
Nina ofisi za ushonaji sehemu 3 nmefungua.nimeajiri vijana 30

Frem ni zangu sijakodi
Nina nyumba za kupanga room kama 10 nimekodisha

Nina bar kama 2 nasimamia mwenyew

Nanimeishia darasa la saba.una lipi lingine la kusema
Aiseeee
 
Yah nikweli kabisa mkuu
Mfano Upo kwa ;
Prf.LIPUMBA Na
S.S.BAKHALESA
 
Nyie ndio mkikosa njia za kutoboa kimaisha huwa mnajinyonga kabisa

Nakufundisha katika kufanikiwa kimaisha hatuangalii kuwa na elimu ya juu au ya chini

Kuna mambo meng yanayo onekana na yasio onekana kuwa uwone maisha yalivyo changamoto zikupige utakapoenda kukopa kwa mtu asie hata na elimu ya darasa 7
 
We soma ili uwajiliwe sie tunapiga kazi niko na vibiashara vyangu vijumba na maeneo kazaa bado napigisha jembe huko shambani.sasa sasa sijui unazungumzia maaendeleo yapi manana huo mshahara wako 1.2m nakusanya ktk kamisheni vya tigo Mpesa.wewe endelea kusoma uje kuajiliwa ujengi mpaka uchukue mkopo
 
Kiongozi njoo privet, siku upange nikifuate popote ila iwe hapa Dar, nikuonyeshe hao unaowaita wasomi ninaofanya nao kazi mimi nikiwa CEO wao. Na nauli ya kuurudi kwako nakupa.
kaka mkubwa mbona unanitisha sasa???.

mimi wala sijataka tufikishane huko unako kutaka.

lkn niseme neno moja tu;-

kama ni kweli kabisa unachokisema kinaukweli,basi Mungu akuzidishie.

labda tu kama nilikukwaza naomba unisamehe kwa sababu mazingira ya ile comment yako ya kwanza,niliona kama kuna utata mahala
 
Guys maisha yana siri kubwa, elimu ni mwanga tu maadam uko hai kutoboa ni jitihada zako binafsi.
 
Acha kuaminisha watu uwongo..wenye elimu ndo hao wanasota mtaan

Me na ufundi cherehan wangu nina mafanikio kuliko hao waliosoma
Ila unatumia nguvu sana kupata pesa raha ya kisomo unashusha mizigo tu
 
Mafanikio kutangaza Nia?
 
Kwenye orodha ya matajiri duniani MAPROFESSOR & MADOCTOR ni wachache sana.
 
Kusema kwamba kuuza mali kwa ajili ya kusomesha watoto ni vibaya, ni pointless. Una upeo mdogo wa kufikiri. Kwani ukiumwa anaekutibu ni nani , si daktari? Angekuwaje daktari bila ya kusoma. Au ww kujua kusoma na kuandika ungejuaje bila kufundishwa na mwl, na huyo mwalimu angepataje uwalimu bila ya kusoma? Hata huyu wa Jamii Forums ambae sasa hivi ametuunganisha tunachat, ingewezekana vp bila ya kusoma? Smartphones, magari, ndege, internet n.k vingewezekana vipi bila ya watu kusoma? Cha msingi elewa kuwa kuna elimu ya kutoa ujinga (scholastic education, la kwanza hadi form six) na kuna elimu za taaluma (professional education) na kuna elimu ya fedha (financial education). Elimu zote hizo zina umuhimu wake na hakuna ya kubeza, hata daraja haliwezi kujengwa bila ya kuwepo na kibarua (ingawa kuna mhandisi)
 
Haswaaa, tunategemeana. Hakuna kubeza waliosoma na hakuna kubeza ambao hawana elimu za taaluma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…