Naongelea ufanye kitu kwaajili yako mwenyewe sio kwaajili ya Kupata heshima Kutoka Kwa Watu wengine.
Mfano, unatafuta Pesa ATI ili uheshimiwe, badala ya kutafuta Pesa kwaajili ya mambo yako na familia yako.
Matokeo yake usipopata hizo Pesa unaishi Maisha ya msongo WA mawazo.
Na sio kwamba umefanya Makusudi Bali kazi ulikuwa unafanya.
Au unaenda Kanisani au msikitini ili Mungu na watu wakuheshimu, come on! Huo ni UTUMWA. Fanya kitu kwaajili yako mwenyewe kama kinakufurahisha na kama kinafaida kwako.
Au unakuta Binti analazimisha Aolewe ili apate heshima. Huo ni UTUMWA na upumbavu. Yaani ili uridhishe Watu.
Heshima sio kumridhisha MTU au kundi la Watu.
Heshima ni kufuata na kufanya Haki, ukweli na upendo. Hiyo ndio heshima.
Na Kati ya hayo sijataja Pesa, Gari, nyumba, n.k
Mtu Aishi Kwa maadili Mema, ajipende na kupenda Watu wanaomzunguka, Aishi Kwa Haki, awe Mkweli. Aishi Kwa uhalisia. Hapo atapata heshima ya kweli na inakuja Natural.
Wazazi wanaodharau Watoto wao kisa Hawana Pesa ni majinga, mazuzu, yasiyo na Maadili. Hiyo pia itaenda Kwa Watoto wanaodharau wazazi wao Kwa sababu ya vitu vya kijinga Jinga.
Na wapumbavu na mazuzu ndio huheshimu Watu Kwa sababu ya Pesa, utajiri, na Elimu. Wakati wenye Hekima na Werevu huheshimu Watu Kwa kuangalia maadili Mema wayafanyayo, utu, haki, upendo n.k.
Sisi Watibeli hata huku kwetu tumeshaweka Watu katika makundi mawili tuu, Wenye maadili na wasio na Maadili.
Ukiwa na Maadili Mema Kwa kweli hata kama ni mdogo wangu au mtoto wangu nitakuheshimu na kukupenda, na kukunyenyekea ikibidi.
Lakini ukiwa na Maadili mabaya hata ungekuwa Mama au Baba yangu au Rais au Waziri au tajiri namba moja Duniani, nitakudharau na kukuona kama Mavimavi tuu.
Hukumu hiyo ikitumika kwangu pia ni Haki.
Mimi MTU akinidharau Kwa sababu ya ukosefu WA maadili Kwa kweli ninajisikia vibaya Sana.
Labda nimefanya uasherati alafu MTU akanifumania Kwa kweli hata kama hatasema kitu nitakuwa Duni kwake Kwa muda mrefu.
Sisemi Kuwa Mimi ni mtakatifu kwamba sina Makosa au sina dhambi, nazungumzia heshima na kudharauliwa.
Pole Mchumba Kwa comment ndefu😊😊