Kama huna pesa hakuna mtu atakuheshimu. Hata wazazi wako watakudharau

Na hii heshima inaongelewa ni kitu gani? Huwa hawakusalimii?

Au unataka kuambiwa matatizo ya watu na kuombwa ushauri?

Na kwanini mtu atake kunyenyekewa?

Seems like it's asking for unnecessary attention.

As much as you'd want to blame them, it's YOU!
 
Ushenzi tu
 
Hapo ndo utakutana na

Hapo ndo utakutana na vibinti vinafiki Mara ooh Ndubwi nimekumisi aggggggggrrr 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Me nkawa nasoma comment nacheka sana.
Wengine hata zawadi watakununulia kwenye birthday yako😆😆😆sijui kama ntaoa mimi maana dah walininyanyapaa sanaa
 
Katika familia ukiwa huna pesa jifunze kujitolea kufanya mambo mengine ambayo hayahitaji pesa.
Kama kuna shughuli piga kazi kuliko wengine, kama kuna mgonjwa wa kuhudumia na una nafasi nenda kahudumie kwa moyo wote. Ni mengi yapo ya kufanya na hakuna anakaye kudharau.
Pesa ni muhimu lakini sio kila kitu.
 
We jamaa huwaga unavituko unaandika mambo ambayo hayana uhalisia
Hakuna binadamu asiyependa recognition kutoka kwa watu wengine
Mfano hapa jamiiforum kuna tuzo wanapewa kupitia member bora au story of change hio yote watu wanafanya ili wapate recognition kutoka kwa watu wengine

Makazin kuna tuzo za mfanyakazi bora hakuna mtu ambaye hafurahii kuwa sio mfanyakazi bora ukiangalia hapo utaona watu tunafanya kazi kwa bidii moja ya sababu ni kuwa recognition

Kwenye michezo kuna prize tofauti tofauti watu wanapewa na angalia ile furaha watu wanakua nayo wanapopewa hizo tuzo hiyo yote ni kutaka kufurahisha watu

Kwenye maisha na (nature) asili kilicho bora kinasifiwa siku zote na ndo raha ya maisha kila mtu anafurah anapofanya jambo linapogusa watu wengine, ukifanya jambo kwa ajili yako huwezi lifurahia

Unaposema ufanye jambo kwa ajili yako mwenye unakuaje motivated
kwa hiyo mkuu mda mwingi unajicontradict sana nyuzi zako nyingi zinapingana zenyewe yaan hujulikan unasimamia kipi

Ukiwa huna hela sio kwamba unadharauliwa kuna mambo ambayo yanahitaji fedha hata ukiambiwa utoe utahisu unadharauliwa ndo maana watu wanakupotezea sasa ukipotezewa usifikiri unadharauliwa ni kwamba huna msaada
 
Hilo haliwezekan dada katika hii dunia
 
Sijui Kwa nini Watu wanapenda kuheshimiwa.[emoji23][emoji23]
Yaani kuendeshwa na Maoni na Mtazamo wa wengine

Kuheshimiwa sio tafsiri yake hiyo.

Ukitaja kujua heshima ina maana gani,subiri siku mtu akutamkie maneno ya fedheha mbele za watu,sababu tu umevaa nguo chakavu au umekosa nauli kamili ndio utaelewa.

Kuna chakula cha mwili(ugali,mananasi,wali,kitimoto nk)halafu kuna chakula cha roho(heshima,upendo,kujaliwa)ukivikosa hivyo lazima usiwe sawa.
 
Nakuunga mkono

Miye unipende usinipende as long as am comfortable with my self I don't care

Huwezi ridhisha Kila mtu

Hauwezi kuwa comfortable for youself,ila una uwezo wa kupuuza yanayokunyima furaha.sababu umekata tamaa kabisa ya kuyapata na uwezekano haupo kabisa.

Ukiwa sehemu pia watu wakapuuza kabisa hali uliyo nayo,hilo pia litakukosesha amani.
 
Hilo haliwezekan dada katika hii dunia
Inawezekana nimeshashuhudia.
Dharau ni tabia mbaya tu za familia. Ikiwa ni familia mliyoishi kwa upendo tangu utotoni hamuwezi kudharauliana.

Nina mama yangu mdogo hana kazi, kiufupi hana kazi lakini ni mtu wa kujitolea sana hasa kwa wagonjwa na anafanya kwa moyo.
Wewe na pesa zako unaweza ukakosa nafasi ya kumuhudumia mgonjwa ndugu yako ya karibu lkn ndugu yako mwingine hana pesa lkn anao muda wa kukaa na mgonjwa. Unaanzaje kumdharau ndugu wa hivyo?

Tatizo la wasio kuwa na hela wanajishtukia sana, kitu kidogo atasema anadharauliwa kwasababu hana pesa.
 
Nakuunga mkono

Miye unipende usinipende as long as am comfortable with my self I don't care

Huwezi ridhisha Kila mtu
You're the same to me .. yaani ukizingatia yanayokuhusu tu hakuna kitu kitakuwazisha.. suala la kufikiria kuridhisha watu ndio mwanzo wa kujipa fikra zitakazokuumiza... Huwa sinaga time na mambo hayo.. ukinipenda it's okay na ukinichukia the same cause nothing else will be added after you love or you hate me..
 
Usipokua na lengo la kutafuta ela siutakua unapuyanga huku dunia jamaa kaongea ujinga
Lengo la kutafuta pesa ni kupata basic needs, as I said, i.e food, shelter, clothing, education, healthcare.

Baada ya kupata na kuwa na uhakika wa kupata basic needs then what?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…