Kama ilipo Israel siyo Israel, Wayahudi wanaotajwa kwenye Quran na Biblia walikuwa wanaishi wapi?

Kama ilipo Israel siyo Israel, Wayahudi wanaotajwa kwenye Quran na Biblia walikuwa wanaishi wapi?

Wayahudi ni kabila miongoni mwa watu waliokuwa wanaishi palestina ila siyo hawa wazungu wazungu waliotoka ulaya kisa wanajua kuongea kiebrania.
Hapo Palestine walipokuwa awali wanaishi kwa sasa panaitwaje ? Najiuliza pia, kama Waisraeli hawapo,, kiebrania kimetunzwaje hadi leo kama lugha yao. Hata kama walienda ulaya Marekani nk kama wakimbizi, hiyo inaondoa uwepo wao na asili yao ?
 
Kwa ivo kwa maelezo yako ni kwamba kosa la Wayahudi ni kutaka kurudi kwao? Kwa ivo pale ni kwao ila waliondoka na sasa wamerudi?
Sio waliondoka, walipateka kwa kigezo wametumwa na Mungu wao wakawapiga wakanaani na kuwahamisha kisha wakasema ni kwao.
Waliishi hapo kwa muda mrefu kisha nao wakavamiwa na kuhamishwa pakamilikiwa na wengine, wengine hao nao wakaja kupigwa pia kama ilivyo desturi ya mwenye nguvu mpishe.
Kihistoria wenye kudai lile eneo ni wakanaani ambao ndio wakwanza kupigwa na wayahudi.
Asili ya wayahudi ni Iraq ya leo ambapo Ibrahim babu wa wayahudi na wapalestina alipakimbia ndio maana nasema ikiwa kila jamii itataka irudi kwenye asili yake, basi tutauana wote tubaki wachache mwisho tujikute tunarudi pale mto Euphrate nchini Iraq kama isemavyo biblia.
Wewe unadhani kwanini sisi wabantu wa Tanzania tusitake kuwapiga wambulu/wairaq na kuwataka warudi kwao Iraq?
Au unadhani kwanini wambulu wasirudi kwao Iraq na kuiacha Tanzania yenye mandhari nzuri ambayo wameridhika nayo huku wakikubali kuishi na sisi tukichanganya vizazi?

Jibu litakuwa sisi sote tuna utu na tunajichukulia hapa duniani tumekutana tu hivyo tuishi kwa upendo bila kubaguana.
 
Caliph Umar aliingia Yerusalem miaka ya 600. Mohammad anatambua uwepo wa wayahudi hapo. Waarabu hawana hoja, wanasumbua makusudi.
Khalifa Umar alipofika Jerusalem aliwakuta Warumi!
Hakukuta hekalu hata Moja la kuabudia mayahudi. Akaigiza watafutwe mabaki yao popote walipo na wapewe uhuru wa kuabudu!
 

Hitimisho​

Kwa kifupi, Wayahudi walikuwa wanaishi kwenye ardhi ya Kanaani (eneo la Israeli ya sasa na Palestina) katika zama za kihistoria. Hata hivyo, mzozo wa kisasa juu ya ardhi hiyo umeleta mgongano wa madai kutoka pande zote mbili. Wayahudi wa Biblia na Quran wanatajwa kupewa ardhi hiyo, lakini migongano ya kisiasa na historia imesababisha hali ngumu ya kiutata kuhusu nani hasa anast
Kanaani hiyo kumbuka kulikuwa na wakanaani hivyo wayahudi wasitake kujiona ndio wamiliki wa pale.
Wawe watulivu waishi kwa amani na majirani zao kama walivyokua hapo mwanzo wakitoka huko ulaya kama wakimbizi. Wapalestina waliwapokea wayahudi wakiwa wakimbizi katoka ulaya ila leo wayahudi wanataka kuwatimua wenyeji ambao ndio waliwasitiri kipindi cha vita vya dunia
 
Ibrahim au Abraham ambaye alimzaa Isaka na Ishmael alikuw mzaliwa wa Uru ya Ukalidayo( ambyo ji Baghdad ya Leo)

Baadae akapewa maono na Mungu wake akahamia nchi ya Kanaani kwenye mji wa Hebron ambao upo had leo kilometer 30 kusini mwa Jerusalem
Kwahyo chimbuko la Waisrael limeanzia hapo Hebron
 
Kuna hoja ipo kuwa pale ilipo Israel kwa Sasa si Ardhi ya waisrael bali wapalestina.

Binafsi nakubaliana na hoja hiyo. Lakini swali la kujiuliza ni kwamba, kama ilipo Israel kwa Sasa siyo nchi ya waisrael, jee pale Mashariki ya kati, waisrael wanastahili kuwepo kwenye nchi Gani?

Quran na Biblia zina hadithi kuhusu wayahudi. Hao wayahudi wanaotajwa kwenye Quran na Biblia, zama hizo walikuwa wanaishi kwenye nchi gani ambayo kwa sasa haipo?
Hao wapalestina ndio waisrael walio tajwa kwenye Biblia. Mtu kakaa Palestina toka wakati wa Yesu hadi leo with Dna proof ya mababu zake kwamba walizikwa hapo, so hawa descendant wa Yesu sio waisrael?
 
Khalifa Umar alipofika Jerusalem aliwakuta Warumi!
Hakukuta hekalu hata Moja la kuabudia mayahudi. Akaigiza watafutwe mabaki yao popote walipo na wapewe uhuru wa kuabudu!
Benzantine empire ( easten roman empire) walikuwa ni wakoloni wa Waisrael so walipotimuliwa wakaja waislam wakoloni wapya. Waliendelea kuwepo hadi vile vita vya crusade.
 
Kuna Waislam Wenye akili pale Mashariki ya Kati wengi tu wanajua ukweli wa uhalali wa eneo la Israel, since historic times. Na ndio maana wako kimya for they know the truth.

Tatizo ni hawa wengine wasio riziki na hata Uislam wao ni WA mashaka mashaka ndio watakuambia Eti Israel ni mvamizi Hana kwake.

Hata vitabu vitakatifu vinatambua Miji ya Israel kwa., Yerusalem, Galilaya, Yudea na mingine Mingi tu. Sasa Miji hiyo Iko Poland?

Kama wa Wana wa Israel walifutika katika uso wa Dunia, kwanini hawakuanza kufutika Wana wa Ishamael ambao ni Wana wa haramu?

Israel shall stand forever.
 
Hao wapalestina ndio waisrael walio tajwa kwenye Biblia. Mtu kakaa Palestina toka wakati wa Yesu hadi leo with Dna proof ya mababu zake kwamba walizikwa hapo, so hawa descendant wa Yesu sio waisrael?
Hao wapalestina ambao ni waarabu wamekuja kipindi Cha utawala wa Ottoman, sawa na waarabu walivyosambaa Afrika kaskazini
 
Hao wapalestina ndio waisrael walio tajwa kwenye Biblia. Mtu kakaa Palestina toka wakati wa Yesu hadi leo with Dna proof ya mababu zake kwamba walizikwa hapo, so hawa descendant wa Yesu sio waisrael?
Hivi wapalestina wa Leo ndiyo wale wafilisti wanaotajwa na Biblia? Kama ndiyo hivyo, kati ya Goliath na Daudi nani alikuwa ni myahudi?
 
Hii ndio tofauti kubwa pekee ni sawa leo watokee wa Catholic waseme kwao ni Vatican sababu ndio nyumbani kwa wa Rome lakini sababu Vatican hapatoshi tuchukue Rome pia. Wayahahudi ni dini na wanaweza kuwepo popote kuna waarabu wengi tu na ni mayahudi hakuna shida. Hawa wazungu waliotoka sijui Poland na nchi za ulaya mashariki ndio shida kubwa. Netanyau halikuwa jina lake alitoka Poland baada ya wao kuhamia Israel na jina akabadilisha Nentanyau.
Tofautisha jews na Judaism. Jews ni watu ila Judaism ndio dini. Kuna mzee wetu mmoja tumetoka kumzika wiki iliyopita nae alikuwa Judaism. Halafu pia kuna jews na zionisim so somen kidogo au tembelea nchi yao uweze kujifunza kwa kuona kuliko kulishwa stor za vijiwen.
 
Back
Top Bottom