Kama ilivyokuwa kwa Diamond Platnumz, Joti naye achukuliwe hatua...

Kama ilivyokuwa kwa Diamond Platnumz, Joti naye achukuliwe hatua...

♦️ Hawajaingia kwenye nyumba yoyote ya ibada inayotumiwa na dini yoyote

♦️ Hawajatumia kitabu kitakatifu kinachotumiwa na dini yoyote

♦️ Hawajanukuu aya ya kitabu cha dini yoyote

♦️ Mavazi waliyoyavaa sio icon ya dini fulani bali ni mavazi ya kijadi kwa jamii za asia hata wasio na dini huvaa hivyo hivyo ila kuna ka utofauti tu wa mfumo.wa.uvaaji kutoka nchi moja kwenda nying
ine, wahindi wanavaa , wachina wanavaa, wayahudi wanavaa nk

♦️ Sioni tatizo hapo bali ni comic video tuu isio taja dini ya mtu. Wakristu wa uarabuni wapo na mavazi yao ni hayo hayo, wapagani wa uarabuni wapo na mavazi yao ni hayo hayo. WAHAYA wa Tanzania wapo, na mavazi yao ya harusi ni hayo hayo na ni ya mila enzi na enzi bila kujali dini zao. Hivyo asiibuke mtu akadhani ana hati miliki na mavazi ya kanzu
 
Sioni Kosa lolote hapo kwa Joti na ukiona Umekwazika na Jambo fulani jua Sindano imefika Mfupani. Hongera mno Joti kwa Ulichokifanya.
Kama ulichukizwa na kitendo alichikifanya diamond kwenye nyimbo yake inatakiwa usimame wa kukemea na hapa pia ,kama hauoni tatizo basi tukibaliane nyimbo ya diamond Haina tatizo.
 
Hivi joti huwa anaigiza kama shoga linalovaa nguo za kike?? Au anaigiza kama mwanamke?? Kama anaigiza kama shoga basi waislam wanapaswa kumkaripia hapa.

Lakini Kama huwa anajifanya mwanamke basi hamna shida na tusimsumbue joti eti kisa amekosa nyeti za kike.

Ni sawa tu na mtu anapoigiza daktari, kwahyo bodi ya madaktari imshukie mtu aliyeigiza daktari kwakuwa hana vyeti?
Suala sio kuigiza kama mwanamke Hilo waislamu walisha liongea Kuna sheikh alimpa ushauri joti miaka ya nyumba kuwa sio vizuri mwanaume kujifananisha na mwanamke lkn hayo ni maisha yake binafsi aliyochagua mbona Kuna yule dogo dulivan anaigiza kama mwanamke na ni muislamu lkn waislamu hawajatoa makasiriko zaidi ya kumuusia kwamba kidini haifai.

Hoja iliyopo hapa Kuna kwenye hio video Kuna sheikh anaonyeshwa anafungisha ndoa wanaume, na wakati ushoga ni uasi mkubwa katika uislamu afu kingine video ya diamond ilizua taflani ikidaiwa inadhalilisha ukiristo

Sasa na hii inatakiwa ichukuliwe hatua kama video ya diamond
 
Nafikiri kuna kukuza tu haya mambo, Joti hapo ameigiza kama mwanamke na wala sio shoga aliyevaa nguo za kike!
Ila Diamond kuimbia Kanisani ilikua sio kukuza mambo kwa kulalamika kwenu? Ule pia ni wimbo tu na sio uhalisia ila mbona mlitokwa povu?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Asante kwa link mkuu nimechekaa sana Kiboga Binti Mbaruku

Utulushie link nyingine mkuu ikiwa unaziona JOTI Mjinga sana [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ila Diamond kuimbia Kanisani ilikua sio kukuza mambo kwa kulalamika kwenu? Ule pia ni wimbo tu na sio uhalisia ila mbona mlitokwa povu?
Ndugu Icebreaker ni vyema ukaepuka kujumlisha mambo...mimi sikutoa maoni yangu kuhusu wimbo wa Diamond katika mandhari ya kanisa, na ukifuatilia michango yangu humu JF hasa inayohusiana na dini utaelewa kuwa mimi sio wa imani unayoninasibisha nayo! vinginevyo uelewe tu kuwa huo ni mtazamo wangu kama binadamu wa kawaida na wala hauna uhusiano na imani yangu ya dini!
 
Huu Ni udhalilishaji dhidi ya uislam,
Waislam hawana utaratibu wa ndoa za jinsia moja.

Hii Ni kesi Kubwa,
Asipokua Makin itamsumbua sana joti
We jamaa ndio maana ule mchepuko unakuchezesha kadanse sasa hapo kosa liko wapi au huoni kama joti ameigiza kama mwanamke hapo?
 
Pale wameigiza ndoa ya jinsia moja??
Mbona unakua mbumbumbu ndgu yako. Wewe mwenyewe umesema "issue ni KUIGIZA", hivi unajua maana ya kuigiza??
Wale jamaa ni mashekhe kweli?? Mbona hujataka uhalali wa wale wanaogungisha hiyo ndoa kama ni waislamu kweli au lah??

WANAIGIZA sio kweli ila WANAIGIZA sijui unaelewa maana ya kuigiza??
Wewe kweli ni hamnazo,akili zako umeamua kuziweka kwenye mfuko wa shati na kutembea na kichwa tu ili kukamilisha kiwiliwili,

Mlivyotokwa povu kwa Diamond kuimbia Kanisani ulikua usingizini?

Ficha upumbavu wako kwa kupiga kimya.
 
Wakuu salaam,

Siku kadhaa zilizopita msanii Diamond alifungiwa wimbo wake kwa maelezo kwamba unadharirisha imani ya watu fulani. Watu walienda mbali zaidi wakasema jamaa kwanza ni muislamu hivyo ule wimbo angerekodia kwenye mazingira yanayomhusu na sio kanisani.

Sasa leo Joti kaachia kazi yake ya sanaa ambayo pia inadharirisha imani fulani. Kwamba anachodepict kwenye hii video ni kwamba uislamu unaozesha watu wa jinsia moja.

Joti anafahamu kabisa kua katika uislamu kujifananisha na jinsia tofauti ni kosa na hairuhusiwi (wakati akiwa orijino komedi walienda kwa sheikh wa mkoa sheikh alhad akawaambia hilo suala). Na pia Joti yeye ni mkristo so hiyo video angeenda kurekodia kanisani.



Sijaona sehemu yoyote walipo kashifu Dini ya mnyanzi Mungu
 
1. Nachukizwa mwanaume kuigiza kama mwanamke..inatia sana kinyaa. Tena kuna aina ya uigizaji inakirihisha; mfano kama hii ya Joti.

2. Kuhusu ile video ya Diamond naona tu wakristo walikaza fuvu. Wao si huwa wanasema wao wako poa hawana mihemko wala sijui nini. Ukiangalia kuna video kibao zina scene za kanisani mfano ya Zoba - Banana. Lakini hakukuwahi kuwa na makelele.

3. Kwenye hili sijaona kama Joti kautukanisha Uislam sababu kaigiza kama mwanamke na si kama mwanaume tata (shoga).

4. Waafrika tusizibebe hizi dini kiasi zinatuweka mbali na identity ya Uafrika wetu. Binafsi, naona dini zinatuondolea identity yetu ya uafrika kwa kasi kila uchwao. Hii inatufanya tunakua waendao ovyo kama vipofu.
 
Kuna watu mnachukulia vitu siriaz sana, dini Ni cover tu la nje.
Imani unayo mwenyewe ndani yako. Hivi vitu Ni cheap sana kulalamika.
 
Back
Top Bottom