Kama Kifo ni mpango wa Mungu basi Mungu wenu atakuwa katili sana, mnawezaje kuwa nae?

Sawa ngoja tuanze mjadala vizuri ili nikupe majibu stahiki kulingana na unavyouliza

Umesema "kwanini hauamini uwepo wa Mungu"

Swali lako lina msamiati ambao ningependa unifafanulie maana sijauelewa

Nini maana ya neno kuamini?
Dah we jamaa

Mimi nataka nijue tu sababu, usianze kuniuliza tena maswali.
 
Kifo siyo kibaya mara zote. Imagine watu kama kina Hitler, Idd Amin, Magufuli, Mobutu wangekuwa wanaishi milele.

Duniani pangegeuka Jehannum
Mmmh wangeishi milele wangekuwa watu wema sana baada ya nguvu za ujana kuisha...
 
Yaani mi inaniuma kitendo cha shetani kuasi akaletwa duniani kwani tulikua hamna sehemu nyingine ya kumpeleka
 
fafanua swali lako kwanza kwa ku define key point ya swali kabla ya kutaka jibu

imani/kuamini ni nini?
Kwani swali langu halijaeleweka?
Au ni wewe tu hutaki kunipa hizo sababu..
 
Nijibu kwanza swali langu kabla hujaniuliza swali.
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, uwepo wake unapingwa na hali halisi ya ulimwengu huu tunaoishi.

Ukitumia logic, utajua kwamba, baba mwenye uwezo, ujuzi na upendo, akiwa anajenga nyumba ya kuishi watoto wake, anaijenga nyumba iwe salama kwa kadiri ya uwezo wake.

Haitegeshei mabomu na mitego ya mishale ili watoto wake walipukiwe na mabomu wafe.

Sasa, imekuwaje Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe ulimwengu ambao mabaya, njaa, matetemeko ya ardhi, vifo, magonjwa, vita, na dhiki nyingi zinawezekana kuwepo, wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayo yote hayawezekani kuwepo?

Jibu moja ambalo napewa mara nyingi ni kwamba, Mungu hakuumba mabaya, ila mabaya hayo yameletwa na uasi/ shetani.

Jibu hili haliridhishi. Kwa kweli ni jibu la mtu ambaye hajaelewa swali.

Mimi nauliza, Mungu, alipokuwa anaumba ulimwengu, alishindwa kuumba ulimwengu ambao uasi hauwezekani kuwapo, shetani hawezi kuwapo na mabaya hayawezekani kuwapo, hata kufikirika tu?

Halafu mtu ananijibu kwamba mabaya yametokana na uasi.

Siyo tu hajajibu swali, hata kuelewa hajaelewa swali.

Sasa na wewe nakuuliza, kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kuwepo, popote, muda wowote, kwa sababu yoyote?
 
Sawa Kiranga nitakujibu,
Ila naomba unijibu kwanza swali langu pale juu.
 
Nimekujibu kwamba siamini kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote yupo, kwa sababu ulimwengu uliopo, kimantiki, unakanusha kuwepo kwa Mungu huyo.

Nimekujibu kirefu, kwa mifano na mantiki.

Hapa hoja si kwamba nikujibu swali lako. Swali limejibiwa kirefu tu.

Hoja ni hii.

Umelielewa jibu nililokupa?
 
Nimekuelewa.
Kwahiyo kuwepo kwa magonjwa na shetani na mabaya ndivyo vinakufanya uamini Mungu hayupo?
 
Shetani naye hayupo, kwa hiyo mtoe kwenye hiyo list.Ni sehemu ya hadithi ile ile ya kuwapo kwa Mungu.

Kuwepo kwa mabaya, matetemeko ya ardhi, magonjwa, ma tsunami, vita, magonjwa na mengine kama hayo, kunaonesha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Kama unasema yupo, kwa nini ameumba ulimwengu ambao unaruhusu mabaya haya yawepo, wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya haya hayawezekani, popote, muda wowote, kwa sababu yoyote?
 
Kwahiyo Kama Ameumba ulimwengu ambao mabaya yapo inamaanisha kwamba hayupo?
 
Back
Top Bottom