Kama Kifo ni mpango wa Mungu basi Mungu wenu atakuwa katili sana, mnawezaje kuwa nae?

Hayo yote majanga, magonjwa hayakuepo kabla ya uasi. Matatizo yalikuja baada ya kuasi,kwa hiyo kama kusengua na uasi kusingekuwa na mambo yote mabaya uliyotaja
Wewe hata swali hujalielewa.

Nakuuliza, Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao hauwezi kuwa na ubaya wowote, pamoja na uasi? Maana uasi nao ni ubaya.

Wewe unanijibu, hayo yote hayakuwepo kabla ya uasi.

Hujaelewa swali.

Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao hauruhusu uasi?
 
Dah yani watu wanakomalia huyu mungu alieletwa na meli Africa kama vile ni wakwao, yani wao ndio wanajua story zake mwanzo mpaka mwisho [emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787]

Buda kitabu kinachoitwa bibilia kilichoandikwa huko ulaya kilipakizwa kwenye mashua kikaletwa mpaka pwani ya africa mashariki kwa msaada wa upepo za Mansoon

Mkajengewa makanisa moafundishwa kitu kipya kitaalamu tunakiita “introduction of new religion” mkaiva kisawa sawq leo mnajiona eti mnamjua mungu wa wazungu kikweli kweli kuliko wao
[emoji23][emoji23][emoji23] stupid kweli

Katafute kwanza historia ya babu wa babu yako aliitwa nani? Alifia wapi na ujana wake alijishughulisha na nini sio kutetea dini ambayo kina Scars mnashindwa kuwajibh maswali yao
 
Wewe hata swali hujalielewa.

Nakuuliza, Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao hauwezi kuwa na ubaya wowote, pamoja na uasi? Maana uasi nao ni ubaya.

Wewe unanijibu, hayo yote hayakuwepo kabla ya uasi.

Hujaelewa swali.

Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao hauruhusu uasi?
Hajashindwa,lakini kama kusingekuwa na sheria ungemjua muumbaji? Mfano mwingine. Hivi barabarani kusingekuwa na sheria kwa ajili ya usafiri,hivi tungeweza kuendesha kweli?
 
Kwani kuwa na ulimwengu usiokuwa na mabaya, matetemeko ya ardhi, ma tsunami, magonjwa, vifo, njaa, uasi ni kuwa na ulimwengu usio na sheria?

Mbona hata huo msingi wa "ulimwengu usio na mabaya" ni sheria tayari inayokataza mabaya?

Unataka kusema Mungu wako alishindwa kuumba ulimwengu ambao hauna mabaya na wakati huo huo watu wanamjua muumbaji?
 
Wasingejua,hapo ulipo tu una kiburi sababu hauna tatizo. Je kusingekuwa na matatizo?
 
Hujajibu swali langu.

Unataka kusema Mungu wako alishindwa kuumba ulimwengu ambao hauna mabaya na wakati huo huo watu wanamjua muumbaji?

Kuhusu kuwa na kiburi kwa sababu ya kukosa matatizo, tatizo lako ni elimu ndogo.

Ungesoma maisha ya Primo Levi, usingesema ujinga huo.
 
mimi hata nikiona uovu wangu haisaidii kitu maana siwezi kubadilika tofauti na alivyopanga yeye. Kwa hiyo hata point ya kusema mitihani ni kwa ajili yangu bado ni insanity
mkuu huku nilikuwa swali ila umekimbia?
labda nikuulize swali hivi kuboresha huduma za afya kunapunguza idadi ya vifo?
 
Swali gani ambalo nimekimbia?
Kama wewe ni msomaji mzuri kachunguze kisa cha Abrahamu na Isaka kwa makini!

Abraham anaambiwa akamtoe isaka, wanaenda mlimani na Abraham anafunga isaka ili amchinge .....
Sasa ona Mwanzo 22:12 Kisha akasema: “Usimdhuru mvulana huyo, wala usimtendee lolote, kwa maana sasa ninajua kwamba unamwogopa Mungu kwa sababu hukuninyima mwana wako, mwana wako wa pekee.”

Niambie hilo neno "kwa maana sasa ninajua" linamaanisha nini kwa wakati uliopita?
 
Kwanza unaelewa hayo maneno ya huo mstari yamemnukuu nani?

Hayo maneno yaliyosema kkwa maana sasa ninajua" unaweza kuniambia ni nani ambaye alikua akiyasema?
 
Back
Top Bottom