sio nimekataa. Bali nimekataa kuukubali uwongo kwa kuitetea fact ambayo yeyote mwenye uwezo wa kujua kusoma akipewa hiyo aya ataweza kuelewa ni nani aliyesema yale maneno
Sasa nacho kiona hapa wewe hutaki kukubali kuwa pale ulikurupuka tu hukumakinika eidha kwasababu hukusoma verse yote hivyo unataka tuache kuzungumzia jambo hilo kiaina tu kwa kuingizia mada zingine katikati kwa lengo la kunitoa kwenye reli
mwanzo 22:11 Lakini malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwita kutoka mbinguni, “Abrahamu! Abrahamu!” Naye akaitika, “Naam, nasikiliza!” 12Malaika akamwambia, “Usimdhuru mtoto wala usimfanye lolote! Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwani hukuninyima hata mwanao wa pekee.
kwa aya hiyo kama kweli yalikua ni maneno ya Mungu ilikuwaje Mungu amwambie abraham kwamba sasa najua unamcha Mungu wakati yeye ndiye Mungu?
mwanzo 22:15 Malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwita Abrahamu mara ya pili kutoka mbinguni, 16 akamwambia, “Mwenyezi-Mungu asema hivi: Nimeapa kwa nafsi yangu kwamba kwa kuwa umefanya hivi, wala hukuninyima mwanao wa pekee
Hapo malaika ananukuliwa kwamba anamuita abraham kwa mara ya pili maana yake hapo awali malaika alimuita abraham, sasa unaweza ukasema hapo mara ya kwanza malaika alipomuita malaika alimuambia nini abraham?