Kama kijana nifanye vipi sasa kabla muda haujanitupa mkono?

Kama kijana nifanye vipi sasa kabla muda haujanitupa mkono?

Kingine nilichokiona binafsi baada ya kuhitimu chuo kikuu, ni kuwa alama nzuri zinaweza kukusaidia kwenye kutafuta fursa ama kujiendeleza zaidi kwenye profession yako haswa kama utahitaji kujiendeleza kupitia scholarships na katika kupata kazi zinazoanzia kuchuja watu kwenye ufaulu. Hata hivyo, ni muhimu kuelewa kuwa sio kila kitu kinategemea na alama zako. Kuna mambo mengi yanayoweza kukuwezesha kufanikiwa katika maisha, kama vile uhusiano na watu.

Ni kweli kuwa uhusiano wako na watu una jukumu kubwa katika kufanikiwa kwako. Unapata fursa nyingi katika maisha kwa sababu ya uhusiano wako na watu, na unapata msaada wa kihisia, kitaalamu, na kifedha kutoka kwa watu ambao unao uhusiano mzuri nao.

Lakini pia ni muhimu kufanya kazi kwa bidii na kujifunza kadri uwezavyo. Kujifunza kwa kina katika masomo yako na kufanya kazi kwa bidii kutakusaidia kugundua mambo ambayo unavutiwa nayo na kupata maarifa na ujuzi unaohitaji ili kufanikiwa katika kazi yako.

Ni muhimu kuwa na dira ya kile unachotaka kufikia na kuzingatia kile kinachokuvutia. Unapopata fursa ya kufanya kazi kwenye jambo ambalo unapenda na unavutiwa nalo, utafurahi sana na utafanya kazi yako kwa bidii zaidi.

Kwa hiyo, ni muhimu kuwa na mbinu mbalimbali za kufikia mafanikio katika maisha. Kujifunza kwa bidii, kuwa na uhusiano mzuri na watu, na kufanya kazi kwenye jambo ambalo unapenda ni mambo muhimu katika kufikia mafanikio yako.
 
Kijana mwenye malengo
1.Elimika(simaanishi uwe na Phd)
2.Jali afya yako(ya mwili na akili)
3.Jenga mahusiano(kuwa na marafiki wa faida)
4.Kuwa imara Fuata ndoto zako (kelele , za ujana zitakuchanganya Kama hauna utulivu wa akili)
5.Kubaliana na mabadiliko (The world is changing day to day)
 
Mshilikishe Mungu yaan mpe yesu maisha yako , okoka
Changamoto lazima upitie ili ujue au uwe sharp minded, kwenye maeneo flan flan,

Mtoto mdogo anapojifunza kutembea, ni lazima aanguke,
Sasa sio kila shimo lazima uangukie mfano,
Kubet
Wanawake
Pombe

Hayo unayaona kbsa Ila angukia kwenye vitu positive ambavyo ukipata changamoto unakua umejifunza
 
Kaka maisha ya siku hizi ni kisonga front na kile unacho kiamini.
Ckuiz mambo ya nidhamu yamepitwa na wakati wewe fanya kazi kwa bidii ila usiibe wala usi zulumu.
Ukiwa na nizam nyingi huta move mana watu watakuchukulia poa kua mkali jiamini.
Ahsante sana.
 
Mshilikishe Mungu yaan mpe yesu maisha yako , okoka
Changamoto lazima upitie ili ujue au uwe sharp minded, kwenye maeneo flan flan,

Mtoto mdogo anapojifunza kutembea, ni lazima aanguke,
Sasa sio kila shimo lazima uangukie mfano,
Kubet
Wanawake
Pombe

Hayo unayaona kbsa Ila angukia kwenye vitu positive ambavyo ukipata changamoto unakua umejifunza
Kama vipi hivyo vitu positive?
 
Kijana mwenye malengo
1.Elimika(simaanishi uwe na Phd)
2.Jali afya yako(ya mwili na akili)
3.Jenga mahusiano(kuwa na marafiki wa faida)
4.Kuwa imara Fuata ndoto zako (kelele , za ujana zitakuchanganya Kama hauna utulivu wa akili)
5.Kubaliana na mabadiliko (The world is changing day to day)
6.Pray to god kwa staili tofauti kila siku....
 
Back
Top Bottom