Kama kijana nifanye vipi sasa kabla muda haujanitupa mkono?

Kama kijana nifanye vipi sasa kabla muda haujanitupa mkono?

Hongera sana dogo kwa kujitambua.

Chuoni jitahidi usome kwa bidii uwe nondo kwenye proffessional unayosomea.

Ila pia uwe na extra callicular ya kukufanya ujulikane na kukujengea jina kubwa . Hakikisha mpaka unafika 30. Uwe maarufu kwa ujuzi fulani.

Mimi nakushauri kama unatoka ukoo ambao hauna connections maofisini ama biashara kubwa jitahidi wewe kujenga brand kwa njia ya yoyote halali.

Usiwe na aibu.

1. Jifunze kuigiza. Na nenda kaombe chance kwa ma director wa tamthilia za kibongo hata kwa kujitolea tu.

2. Jifunze bongo fleva hata kuimba singeli . Wimbo mmoja tu ukibahatisha uka hit. Ghafla Unapata mtaji wa nguvu

3. Tengeneza content za social media. Tik tok, instagram na youtube.

4. Jifunze U MC wa masherehe

5. Jifunze utangazaji wa habari. Hata kama hujasomea taaluma hiyo. ( taaluma hii inakupa umaarufu na kujenga brand fasta )

Bongo umaarufu unawapa watu connections kali sana. Utakutana na watu wengi wanaoweza kukupa ajira kwenye ulichosomea chuo. Na hata ukuu wa wilaya, ubunge ama uwaziri
Ahsante sana, nimeupokea ushauri huu.
 
Daaaa mwenzio Nina five decade na cjasoma ramani
 
Heri ya siku njema ya leo.
Mimi ni kijana wa miaka 24 naelekea kutimizia 25 hivi karibuni. Ninasoma chuo kikuu mwaka wa nne(wa mwisho).

Nimewaona wengi ambao wangeweza kunishauri vitu vya msingi vya kuwa navyo umri huu kabla muda haujaniacha, ila kwa heshima ya madini yatokayo JF nimeamua kuja humu kwanza kutoa duku duku langu hili.

Humu najua tupo watu tofauti ila wengi ni intellectuals. Naomba mnisaidie fumbo langu hili, kulitafsiri na kuniambia chochote kitu.

Sitaki kujutia kama wengi wa miaka 50+ wanavyojuta, kwa kushindwa kuukomboa wakati. Sitaki yanifike hayo.

Wakati ni sasa, na leo ni leo asemaye kesho ni mwongo. Wakati umeiva!
Ushauri wangu labda ndio utakua wa tofauti sana , Mie nakushauri kama hauna connection yoyote bongo utaishia kua maskini ni bora uondoke tu tafuta chuo US au nchi yoyote ya Ulaya lakini US na Canada ndio rahisi zaidi, uaply chuo kozi uliosomea kama kawaida, kila watachokihitaji lipia, hadi visa au jaribu green card, halafu uondoke bongo huko fika soma kidogo halafu tafuta kozi hizi ambazo zinahitaji watu kwa sasa kama healthy science ambazo zimeathirika na Covid. Ukimaliza hizo kozi hukosi kazi za maana; na mshahara utapata wa kumzidi Mwigulu Nchemba na posho zake. Weka malengo yako basi utafanikiwa.
 
Ushauri wangu labda ndio utakua wa tofauti sana , Mie nakushauri kama hauna connection yoyote bongo utaishia kua kua maskini ni bora uondoke tu tafuta chuo US au nchi yoyote ya Ulaya lakini US na Canada ndio rahisi zaidi, uaply chuo kozi uliosomea kama kawaida, kila watachokihitaji lipia, hadi visa au jaribu green card, halafu uondoke bongo huko fika soma kidogo halafu tafuta kozi hizi ambazo zinahitaji watu kwa sasa kama healthy science ambazo zimeathirika na Covid. Ukimaliza hizo kozi hukosi kazi za maana; na mshahara utapata wa kumzidi Mwigulu Nchemba na posho zake. Weka malengo yako basi utafanikiwa.
Njemba labda atamzidi za wizi wanazohalalisha kwa urefu wa kamba Basi Ila achukue haki yake ama jasho lako hata mie hanigusi ambaye Ni jobless na PhD ya mchongo na utalaamu wangu nilionunua burundi
 
Kama upo chuo anza kujihusisha na siasa hasa uwe upande wa ccm , fanya juu chin jipendekeze , yani tetea serikal ata kama inafanya madudu , utakuja kunishukuru dogo.
 
Ahsante sana
 
Njemba labda atamzidi za wizi wanazohalalisha kwa urefu wa kamba Basi Ila achukue haki yake ama jasho lako hata mie hanigusi ambaye Ni jobless na PhD ya mchongo na utalaamu wangu nilionunua burundi
Utaalamu upi huo
 
Kama upo chuo anza kujihusisha na siasa hasa uwe upande wa ccm , fanya juu chin jipendekeze , yani tetea serikal ata kama inafanya madudu , utakuja kunishukuru dogo.
[emoji38][emoji38][emoji38] haya bhana
 
Put this into consideration seriously. Zamia nje kuishi au kutafuta mtaji ufanye hiyo biashara yako, bongo hutoboi. Huu ndo ushauri pekee chukua.
Kweli kabisa, mie niliondoka bongo mwaka mmoja tu baada ya kumaliza UDSM, nipo huku kwa Biden na sijutii. Niliondoka na lengo langu moja tu kuja kuishi huku, sio kurudi tena afrika. Bongo uwa nakuja kusalimia maana nina mijengo yangu huko miwili na huku nina mjengo wangu wa mortgage, sitaki kurudi huko kwa sasa. Bongo bila connection au kua kwenye circle ya ccm ni kweli hutoboi , ila tatizo ninaloliona wabongo wengi ni waoga wa maisha sio kama wakenya au waganda na west africans ambao wamejaa huku wanapambana haswa.
 
Back
Top Bottom