Bufa
JF-Expert Member
- Mar 31, 2012
- 12,599
- 26,263
Kweli kabisa, mie niliondoka bongo mwaka mmoja tu baada ya kumaliza UDSM, nipo huku kwa Biden na sijutii. Niliondoka na lengo langu moja tu kuja kuishi huku, sio kurudi tena afrika. Bongo uwa nakuja kusalimia maana nina mijengo yangu huko miwili na huku nina mjengo wangu wa mortgage, sitaki kurudi huko kwa sasa. Bongo bila connection au kua kwenye circle ya ccm ni kweli hutoboi , ila tatizo ninaloliona wabongo wengi ni waoga wa maisha sio kama wakenya au waganda na west africans ambao wamejaa huku wanapambana haswa.
Sidhani kama ni waoga ila hawakua na sababu ya msingi ya kuondoka nchini. Bongo ilikua tambarare miaka hiyo, mtu ulikua na uhakika wa kupata kazi hata kama ni ndogo, nyumba na shamba. Wakarelax. Sasa hata kazi ya kujitolea hupati.
Nchi ulizozitaja kwao game tight toka miaka ya uhuru. Nigeria kila siku mapinduzi na vita toka 60s, Uganda na Kenya njaa kila siku plus vita. Bongo there's none of that. Watu hawakua na sababu ya msingi kukimbia nchi. Wengi walikua wanazamia just for fun na yakiwashinda wanarudi home ambako ilikua tambarare.
Ni kama leo ni nadra sana kukutana na raia wa South Africa, Namibia au Botswana wanaishi nje ya ya nchi zao permanently, nchi zao zina mazingira yote ya kukufanya ubaki pale.