Kama kilichoripotiwa na CAG ni Kweli, basi Magufuli alikuwa sahihi mara 3...

Kama kilichoripotiwa na CAG ni Kweli, basi Magufuli alikuwa sahihi mara 3...

Mnajitahidi kupaka rangi kaburi lakini kilichomo ni uozo mtupu.

“Nilibaini kuwa wakala wa ndege za Serikali ililipa bilioni 3.92 Kama gharama za matengenezo makubwa ya ndege. Baada ya ziara nilibaini ndege ilikuwa haifanyi kazi toka 2015.” CAG.
Kwa hiyo na ww umemeza kama ilivyo.....
hizo political manouvers zinazochezwa huko nyuma unazijua!!.??
 
Ukisoma mitandao ya kijamii hasa twitter utafikiri kweli hii nchi imeibiwa kila kitu na hakuna kitu kimeachwa, kumbe sio kweli.

Watu wanajifanya kushangaa ATCL kupata hasara, hivi mtu mwenye akili timamu unaweza kushangaa atcl kupata hasara? By the way, ni shirika gani la serikali linalopata faida? Lipi? Mashirika yote ni hasara kila mwaka kuanzia Tanesco, TPDC, TTCL, ATCL, NHC na mengine yote, kwa nini shida iwe kwa ATCL?

Halafu watu wanataka kusema Magufuli ange eliminate rushwa ama wizi wa mali za umma 100%, hilo jambo halipo Duniani. Duniani kote, kuanzia China ambapo kosa la rushwa unaweza kuuwawa ama Marekani ambapo mifumo iko strong bado watu wanaiba na kula rushwa, tusimsingizie Magufuli kwa kila kitu.

Kuna kikundi ama kingenge cha wahuni sijui kinalipwa na nani kutaka kumchafua Magufuli na report ya cag
Well, kama ndivyo mashirika yote hayo yalikuwa yakiendeshwa kwa hasara, a funny thing happened kwamba baadhi yao yalitoa dividend!
Ndugu zangu, je nasema uwongo?

Sent from my TECNO BC1 using JamiiForums mobile app
 
Ww utakuwa mzoga team sio bure you can't even reason!!???
MATAGA safari hii kama vipi muhame nchi maana chini ya mama yetu Samia lazima mtawekwa hadharani kwa madudu ya hovyo mliyo yafanya ya ufisadi ulio kubuhu.
 
Ukiwasikiliza wapinzani ni kwamba chama tawala alikuwa Magufuli na sasa Magufuli katoka hivyo wamefanikiwa kuitoa ccm madarakani.
 
Ni ujinga kuamini mtu anaejenga miradi mikubwa hawezi kufanya Ufisadi. Ufisadi ni zao la mfumo. Watu wenye akili wanakushangaa kwa kuhoji taarifa za ufisadi kisa kuna maendeleo yanaonekana kwa macho!

Hivi hatuwezi kuleta maendeleo bila kufanya ufisadi?
Wenye hekima walijua nini kinaendelea. Nguvu kubwa ilotumika kujaribu kuua upinzani, kuminya uhuru wa habari, kuminya haki za Raia kupewa taarifa kupitia sheria mpya ya takwimu, kuondoa matangazo mubashara ya Bunge, ilitosha kwa mwenye akili yeyote kujiuliza kinafichwa kitu gani kisijulikane.

Hila zilizotumika kumwondoa Prof. Assad kwenye majukumu yake ilitosha kwa mwenye akili yeyote kujiuliza kinafichwa kitu gani kisijulikane.

Hakuna Mwizi anayependa kupigiwa mayowe.

Niliwahi kuandika hapa siku za nyuma kwa kusema Tanzania bila shaka ni Taifa lenye wajinga wengi sana miongoni mwa Mataifa yanayoishi leo.

Kama marehemu hapaswi kukosolewa, basi historia haina maana.
Nguvu kubwa mnayotumia kufuta legacy ya JPM ina ajenda nyuma yake na tumeshawastukia. Kama mna lengo jema, na nia yenu si ovu, si muiwajibishe serikali ya JPM kuanzia waziri mkuu wake, makamu wake wa rais, mawaziri na watendaji wake wote? Mbona bado wapo wapo serikalini? Ni uhuni tu, na bado muendelee kusisitizwa, JPM kaacha jeshi kubwa nyuma. Furaha yenu ni ya muda tu.
 
Nguvu kubwa mnayotumia kufuta legacy ya JPM ina ajenda nyuma yake na tumeshawastukia. Kama mna lengo jema, na nia yenu si ovu, si muiwajibishe serikali ya JPM kuanzia waziri mkuu wake, makamu wake wa rais, mawaziri na watendaji wake wote? Mbona bado wapo wapo serikalini? Ni uhuni tu, na bado muendelee kusisitizwa, JPM kaacha jeshi kubwa nyuma. Furaha yenu ni ya muda tu.
Mnajidanganya sana nyinyi sukuma gang.
Mjiandae maana mtakamatwa mmoja baada ya mwingine na team zenu zote maana hamuwezi kumkwamisha rais wa nchi.
 
Kama hamtaki hameni nchi mrudi kwenu Burundi
Dawa
Yani hawa jamaa ni wa shamba sana walijidanganya Tanzania ni ya kwao!
Wange changanya akili vizuri wange fika mbali sana ila mtu mshamba na mbinafsi hajawahi kuwa na akili!
Wasukuma huwawezi wewe tafuta mlo wako tu, ukiongelea uchumi wa nchi hii unaongelea usukumani ukiongelea ziwa kubwa liko usukumani na samaki wataaaaamu. Kaa kimya ulishwe upate mlo, ningetaja umaskini wa eneo lako lisilo hata na chembe ya madini ya kusingiziwa. Tanzania ni nchi ya pili afrika kwa mifugo na wafugaji ni wasukuma na wamasai. Madini yanayochimbwa nchii kwa sasa yako usukumani na umasaini. KAA KIMYA achana na sukuma gang
 
Nguvu kubwa mnayotumia kufuta legacy ya JPM ina ajenda nyuma yake na tumeshawastukia. Kama mna lengo jema, na nia yenu si ovu, si muiwajibishe serikali ya JPM kuanzia waziri mkuu wake, makamu wake wa rais, mawaziri na watendaji wake wote? Mbona bado wapo wapo serikalini? Ni uhuni tu, na bado muendelee kusisitizwa, JPM kaacha jeshi kubwa nyuma. Furaha yenu ni ya muda tu.
Hakuna cha legacy wala nini zaidi ya ufisadi wa hali ya juu
 
Dawa

Wasukuma huwawezi wewe tafuta mlo wako tu, ukiongelea uchumi wa nchi hii unaongelea usukumani ukiongelea zikwa kubwa liko usukumani na samaki wataaaaamu. Kaa kimya ulishwe upate mlo, ningetaja umaskini wa eneo lako lisilo hata na chembe ya madini ya kusingiziwa. Tanzania ni nchi ya pili afrika kwa mifugo na wafugaji ni wasukuma na wamasai. Madini yanayochimbwa nchii kwa sasa yako usukumani na umasaini. KAA KIMYA achana na sukuma gang
Umesahau na sifa ya ufisadi wa kutisha kama mmluvyofanya safari hii.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Ufisadi uliofanyika wakati wa miaka mitano ya Rais Magufuli tunaambiwa ni mkubwa sana. Kwamba, mabilioni ya fedha yameliwa na wajanja na kuwa fedha hizi zimeliwa na watu walioteuliwa na kusimamiwa na Rais Magufuli. Kwa haraka haraka - kama kawaida naona siku hizi - wakosoaji wa Rais Magufuli (na hapa nawazungumzia wale wa kisiasa) wameruka ruka kwa shangwe wakisema "si tuliwaambia!". Na kinachosikitisha kidogo ni kuwa hata baadhi ya watu ambao wamejitambulisha kuwa ni wapinzani nao wamerukia kwa furaha tu na hata hawajui ni kitu gani wanaandaliwa. Sijui ni nani anayewalengesha hawa lakini kilichofanyika na kinachoandaliwa labda ni cha kutisha zaidi kuliko kilichotokea. Kuna mtu aliuliza (jamaa yangu Philemon Michael) wakati msiba ulipotangazwa maswali ambayo sidhani kama kuna mtu atakuja kuyauliza hadharani au kutaka kuyajibu yaeleweke. Na kuna mtu aliuliza tena wakati CAG amewasilisha Bungeni ripoti yake kwamba je hii ndio ile ile ripoti ambayo kama JPM angekuwa hai angekabidhiwa? Sijui jibu lake... Kama ni ile ile inawezekana hakukuwa na jinsi ripoti hii ingekutana na JPM meza moja... Kama ni nyingine... Magufuli alikuwa sahihi mara ya 1.

Hii miaka mitano tumeshuhudia miradi mikubwa ya kila namna na hata tukajisikia kuwa kuna kifu kinafanyika... lakini leo tunaambiwa lote ni changa la macho. Hizo hospitali hakuna zilizojengwa, hakuna masoko, hakuna vituo vya mabasi, hakuna shule zilizofanyiwa matengenezo makubwa, hakuna hiki wala kile na hata ndege tulizoambiwa zilinunuliwa kwa fedha taslimu kumbe hazikununuliwa... yaani, hata hii SGR na Bwawa la Umeme la Nyerere yote ni geresha tu! Kwamba kote huku watu walikuwa wanakula tu na tunachokiona hakipo na kama hili ni kweli basi Magufuli alikuwa sahihi mara 2.

Lakini kingine ni kuwa baadhi ya watu ambao waliteuliwa na Magufuli, walifanya naye kazi, na waliimba "maendeleo" "maendeleo" na hata kusifia kuwa tumeachiwa "urithi" kumbe si kweli; tumeachiwa madeni na ufisadi. Na kwa vile hakuna anayejitokeza kuwa na ujasiri wa kutetea walichokifanya kwa sababu kuna mtu anaitwa "Mwendazake" ameende na utetezi wake kumbe watu wamelia bure. Leo wengine (kina Ndugai) wanageuka wazi wazi; kumbe walikuwa wanaunga mkono uongo; walikuwa wanashangilia ulaghai, na walikuwa wanaficha ufisadi.. hapa watanyoshewa kidole wote kuanzia aliyekuwa Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri wote (na wengi wamerudi au kuhamishwa) na kwa kweli inawezekana wabunge wote walioweza kuingia wakisimama nyuma ya Magufuli. Kama hili ni kweli kwamba ufisadi umetokea wakati watu wale wale ambao leo wanatufunulia ufisadi huo walikuwepo basi Magufuli alikuwa sahihi mara ya 3.

Swali kubwa ni usahihi gani ambao ninauzungumzia? Mwenye kusoma na aelewe. Kama kinachodaiwa na kushangiliwa leo ni kweli basi nchi haina kitu kingine cha kufanya bali kurudi kwenye uchaguzi mkuu mapema zaidi (labda Oktoba mwaka huu) kusafisha uchafu huu; ili wananchi wasisubiri kupigwa tena miaka mitano ijayo... Kama kina Majaliwa na wenzake wote hawakubaliani na assessment hii ya kuwa wamekuwa ni serikali ya kifisadi basi Waziri Mkuu aongoze kujiuzulu mara moja ili kumpa Rais nafasi kweli ya kuunda serikali anayoitaka ambamo ndani yake asirudi HATA MMOJA ALIYEKUWA NDANI YA SERIKALI YA MAGUFULI. Ndio maana ya KUWAJIBIKA KWA PAMOJA.

Wakitaka kuendelea bila kuwajibika ni lazima kuna kitu kingine kinaandaliwa. Ajenda ya Magufuli haijafa, haitakufa na kwa hakina haitoachwa ife. Maana, kama ufisadi huu umefanyika kwa kiasi hiki basi inawezekana Magufuli alikuwa ni genius aliyepindukia. Yaani, kama ufisadi kama huu ungefanyika wakati wa Mkapa au JK hii nchi ingekuwa mbali sana!

Subiri uone kama kuna mtu anaweza kutetea mtu dhalimu. Kama aliweza kunajisi uchaguzi kwa kiwango kile, ni nani unataka kumletea hekaya zako? Hakuwa mtu muadilifu hilo halina mjadala, ndio maana hata waliomzunguka ukiacha uoga waliokuwa nao, wameweza kumgeuka haraka sana. Naona umejaribu kutaja miradi mingi katika hali ya upotoshaji, kama vile wote wanasema hakuna kilichofanyika. Acha kuleta hoja ulizochanganya na upotoshaji, ili kuficha ukweli wa kinachozungumzwa sasa. Ni hivi, hakuwa muadilifu hata kama kuna vitu kadhaa vimefanyika.
 
Ok ni haki yako lakini kwa binadamu kamili angehoji je, kwanini aliyeninasibu kuwa msafi mithili ya sufi apende kufanya mambo gizani kiasi kile?
Sio alikuwa ana fanyia gizani hapana alikuwa anafunga na macho kabisa ana piga 💰💰💰 sio sandarusi yeye ni 🚛🚛🚚🛳🛳
 
Sijaelewa ?, Kwamba huenda sio Kweli ?, Kwamba huenda alikuwa sahihi Kuzuia haya yasijulikane na kuminya transparency ili wizi kama huu uendelee bila kujulikana ?

Tukumbuke hata kama mtu alifanya mazuri saba je inamaanisha yale mabaya matatu tusiyaseme ili asichafuke ?

Nilipokuelewa kidogo ni kwamba hawa wanapropaganda waliokuwa wanampigia makofi wajiuzuru ila tatizo hata wakijiuzuru hao waliopo benchi wakiingia huenda ikawa ni yaleyale..., cha muhimu transparency iendelee ili tukipigwa au kama kuna uonzo angalau tusikie harufu sio kipindi cha jamaa badala ya kuoga na kusafisha kikwapa tunapiga perfume tu na kujiona watanashati...
 
Subiri uone kama kuna mtu anaweza kutetea mtu dhalimu. Kama aliweza kunajisi uchaguzi kwa kiwango kile, ni nani unataka kumletea hekaya zako? Hakuwa mtu muadilifu hilo halina mjadala, ndio maana hata waliomzunguka ukiacha uoga waliokuwa nao, wameweza kumgeuka haraka sana. Naona umejaribu kutaja miradi mingi katika hali ya upotoshaji, kama vile wote wanasema hakuna kilichofanyika. Acha kuleta hoja ulizochanganya na upotoshaji, ili kuficha ukweli wa kinachozungumzwa sasa. Ni hivi, hakuwa muadilifu hata kama kuna vitu kadhaa vimefanyika.
Hao tayari washageuka wapinzani
 
Back
Top Bottom