Kama kilichoripotiwa na CAG ni Kweli, basi Magufuli alikuwa sahihi mara 3...


Kunywa chochote hapo kwa Mangi nakuja kulipa! Huyu mzee nilimuovarate huko nyuma, sikujua kama ni kiazi kwa kiwango hiki. Mahaba niue yake kwa Magufuli yamemshusha kiwango vibaya sana.
 
Kama leo unaona sio ajabu kwa ATCL kupata hasara.. mbona miaka yote hatukuambiwa. Na kwanini mwaka jana walidanganya wamepata faida na wakatoa gawio kwa serikali la B 23? Kwanini Magu alikuwa anaongopa? Kwanini ofisi ya CAG ilipunguziwa bajeti yake ili isifanye kazi ya kuchimba madudu na Profesa Assad akafukuzwa?
 
Kama Mheshimiwa Magufuli kaacha jeshi kubwa nyuma, basi jeshi hilo linapaswa lipokee ripoti ya CAG inayobainisha mapungufu makubwa katika matumizi ya pesa za Umma na kuyafanyia kazi ili kuendeleza legacy ya JPM na Serikali yake.

Nimesema kwamba kufanya miradi ya maendeleo hakumpi Kiongozi yeyote haki ya kufanya ama kuruhusu ufisadi. Mheshimiwa Magufuli kaacha alama 4 kubwa katika maendeleo ya Taifa hili, hilo halina ubishi, lkn hii haiondoi ukweli kwamba kuna wizi mkubwa umefanyika katika awamu yake lkn alizuia umma usiambiwe.

Kuikosoa taarifa ya ukaguzi uliofanywa na CAG ni ujinga mkubwa.

Ni aibu kujiita Mzalendo huku unatetea wizi wa mali ya Umma.
 
CAG ni kiongozi wa idara ambaye ana technical team, vijana wake wamefanya kazi wanayopaswa ! Labda niulize tunadhani CAG anaweza kuandika vitu ambavyo havipo kwa faida ya nani?
Wana sukuma gang wanachohitaji ni REPORT INAYO MSIFIA MWENDAZAKE KUWA HAJAWAHI KUONEKANA KIONGOZI KAMA YEYE.
 
Bila katiba mpya hakuna kitu utamwajibishaje mwizi ingali wanajua mfumo wao wa kuiba ukoje na njia zake

Kuiba pesa za uma ni mfumo uliopo juu mpaka chini sasa nani wa kumfunga paka kengele ?

-Ukichunguza utajua hii aliyeiba kwenye shirika ameoa kwenye ukoo wa ndugai

Hapo unaanzaje kumkamata mwizi?
 
Binafsi huyu CAG simuamini kamwe.
Usipomuamini CAG utakuwa unafanya makosa makubwa sana. CAG yuko sahihi na ana nia njema sana, lakini pia Hayati JPM naye alikuwa yuko sahihi na akiwa na nia njema sana vile vile, isipokuwa baadhi ya wasaidizi wa JPM ndiyo hawakuwa sahihi na hawakuwa na nia njema!
 

Kwani tulipokuwa tunawalaumu wakoloni kwa kuiba raslimali zetu, ni kuwa waliiba zote? Naona umeishiwa na hoja za utetezi.
 
Ni hivi, mtu dhalimu hawezi kuliliwa kiasi hicho tulichokishuhudia. Hajageukwa na wote waliomzunguka, hiyo ni tafsiri yako. Ni kwa vile tu umesikia kelele na mayowe ya matapeli wanaotaka kutumia kipindi hiki cha mpito kama fursa ya kumchanganya mama afuate nia zao ovu. Uimara wa mama utapimwa hapa.
 
😀😀😀😀 Endelea kuota ata Marekani anachota mafuta hapo Libya na uarabuni
Kaa Kwa kutulia 💺tuku fundisheni ile ikitokea bahati mbaya ingine akili ziwe zime komaa!
Unafikiria USUKUMA wakati sisi tuna fidia kwenda kuwekeza Kongo na sehemu nyinginezo!
Tambua kwa Asilia flani vinasaba vyangu vina USUKUMA pia ila me sio mshamba
 

Hata Kaburu Pieter Botha wa Afrika kusini naye kuna waliomlilia. Kwa taarifa yako hata majambazi wanaouwawa kwenye wizi, kuna watu huwa wanawalilia sana.
 
Nadhani hoja yako ni kulalamika kuwa ndugu yako Magufuli amesalitiwa baada ya kufariki , kwamba alipokuwa hai mbona ufisadi huu haukusemwa ? mbona akina Mkapa na wengine walisemwa wakiwa madarakani ?

Ni hivi , kabla ya Utawala wa Magufuli vyama vya siasa vilikuwa na uhuru wa kufanya mikutano ya hadhara , kwenye mikutano hiyo uchafu wote wa watawala ulianikwa , Magazeti yalikuwa na Uhuru wa kuandika na kufichua uozo wote uliofanywa kwenye miradi , wewe umekuwa mwandishi wa MwanaHalisi kwa miaka yote hiyo na hukuwahi kufikishwa Mahakamani wala hukuwahi kutekwa , kulikuwa angalau na uhuru wa kutoa maoni .

Kabla ya kufanya atakavyo , Magufuli alipiga marufuku mikutano ya hadhara pamoja na harakati zote za kisiasa ili mambo yake yasifahamike , Vyombo vya habari visivyomtukuza vilidhibitiwa , waliojitolea kuokoa nchi kwa kusema uchafu wake hadharani walipigwa risasi , walitekwa na kutupwa kwenye mapori na baharini bila huruma yoyote , akajipa Uungu Mtu , Sasa muda wa kumsema ni huu , na ndio maana unaona alipokuwa hai watu walimsifu kinafiki , hakuandikwa vibaya kwa vile alidhibiti vyombo vya Habari kwa kuwatumia wapambe wake akiwemo Hassan Abbass , tungewezaje kufichua uovu ? Akataka kudhibiti hata hii JF , kamata Melo na kumtia korokoroni , unatarajia watu wangesemea wapi ?

Nakuhakikishia kwamba Magufuli ndio atakayekuwa rais wa hovyo zaidi kuwahi kutokea Tanzania milele na hatakumbukwa kwa wema wowote huko ccm wala Tanzania , Naihurumia familia yake
 
Assad alimchafua Magufuli, kichere nae anamchafua Magufuli, hivi ninyi mnaakili sawa sawa?
 
Wewe unatazama upande mmoja wa ripoti ya CAG, mimi ninatazama pia pande zingine kuanzia bungeni (tuendelee kununua ndege au tuache..?) na kauli kadha wa kadha za viongozi serikalini. Ninachokisoma ni mpango kabambe uliopangwa wa kutaka kufuta legacy ya JPM na kuirudisha nchi kuzimu. Kwani mara ngapi JPM mwenyewe amekuwa akisema kwamba nchi hii inachezewa sana, akiwa rais? Yeye mwenyewe hao aliokuwa akiwatumbua mara kwa mara ilikuwa ni kwa sababu gani kama sio kwa ufisadi? Suala si kufumbia macho ufisadi, suala ni watu waovu sana, mafisadi wa kiwango cha juu kabisa, wanaotaka kupaint picha kwamba JPM mwenyewe alikuwa fisadi nyuma ya pazia. Hilo si kweli na it wont work.
 
Hata Kaburu Pieter Botha wa Afrika kusini naye kuna waliomlilia. Kwa taarifa yako hata majambazi wanaouwawa kwenye wizi, kuna watu huwa wanawalilia sana.
Sasa ieleweke kwako kwamba JPM alililiwa na taifa zima, na bara zima la Afrika. Huyu si mtu wa kumfuta kirahisi.
 
Wapigaji wamerudi kwa kasi ili mambo yao yaende kazi ni moja kuua legacy yote ya mwendazake alafu waanze kupiga kama ilivyoada

Wapigaji hawajarud,walikuwepo tuh,

Infact hawakuwahi kuondoka,ni meko tuh aliamua kuminya uhuru wa habar na ukweli kusemwa,ukweli ndiyo huo unasemwa sasa,yeye si alikuwa hataki kuambiwa ukweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…