Kama kilichoripotiwa na CAG ni Kweli, basi Magufuli alikuwa sahihi mara 3...

Nimesoma lakini sijaelewa unataka kufikisha ujumbe gani.
uyo anamtetea Magufuli, na pia anasema turudi kwenye uchaguzi mkuu,SAMIA asigombee, asimamishwe msukuma yoyote kama Chenge, ili wasukuma washike tena hatamu, Tatizo ni uraisi wa Samia hapo,,, mwendazake alikuwa fisadi mkuu
 
CCM haipo, bali inalindwa na jeshi la polisi pale kwenye box la kura
 
Nimekuelewa..lkn unapaswa ujiulize jambo moja, kama Mheshimiwa Magufuli alikuwa na nia njema na Nchi hii kwa nini alizuia sauti mbadala zisiingie Bungeni?
Kwa nini alichukizwa na taarifa za ufisadi wa Serikali yake? Kwa nini alizuia vyombo vya habari kufanya kazi zao kwa uhuru? Kwa nini alizuia Bunge live kwa kisingizio cha kubana matumizi lkn yeye akionyeshwa live hata kwenye shughuli za kuzindua soko?
Huko Bungeni unakokusemea kumejaa watu wengi ambao ni wezi na mafisadi wakubwa kwenye Nchi hii. Wao hutazama maslahi yao tu. Wapo tayari kufanya kazi na yeyote ilimradi ufisadi wao unadumu.
Waliokataa ujenzi wa Bagamoyo leo wanaupigia debe. Walioshangilia ununuzi wa ndege leo wanahoji uendelee ama ukome. Walio apa kumwongezea muda wa kutawala leo wanatetea udhaifu na wizi mkubwa kwenye taasisi za Umma.
Mfumo unaozalisha ufisadi kamwe hauwezi kuondoa ufisadi hata kama ataletwa Malaika kutawala.
 
Kunywa chochote hapo kwa Mangi nakuja kulipa! Huyu mzee nilimuovarate huko nyuma, sikujua kama ni kiazi kwa kiwango hiki. Mahaba niue yake kwa Magufuli yamemshusha kiwango vibaya sana.
MI MWENYEWE SIAMINI KAMA JAMAA MAHABA NIUE UTAFIKIRI HUU UFISADI WAMEFANYA UPINZANI ATAKUWA MSUKUMA HUYU TU UPIGE BIL 3 MZEE ASIJUE MNALETA UTANI NYIE MWIZI NI MWIZI TU HATA UMTETE VIP NDO MAANA ALIBANA UHURU WA VYOMBO VYA HABAR ALIJUA ATAGUNDULIKA WIZI WAKE NA KWA MWENDO HUU JAMMA ALIKUWA HATOKI IKULU
 
Usimwamini NDUNGAI MNAFIKI na huyu Mama ambae hana anachojua zaidi ya mipasho na taarab
Kwa huyu mama bado ni mapema sana ku judge direction anayoenda,tumpe muda kidogo ili tuweze kupata tathmini ya utendaji kazi wake...
 
uyo anamtetea Magufuli, na pia anasema turudi kwenye uchaguzi mkuu,SAMIA asigombee, asimamishwe msukuma yoyote kama Chenge, ili wasukuma washike tena hatamu, Tatizo ni uraisi wa Samia hapo,,, mwendazake alikuwa fisadi mkuu
Aaah wapi..!

Wasukuma Tena??wasahau nchi hii,kama ni gundu,jamaa yao ameshawatia gundu...

RAIS,ni mama SAMIA had 2030..!!
 
Nimekuelewa pia. Sijawahi kusema popote kwamba JPM hakuwa na kasoro zake na miongoni mwa kasoro zake ilikuwa uwezo wake mdogo wa kuhimili kelele kinzani. Kwa nini hakuwa na uwezo huo siwezi kujua, pengine ni kwa sababu high performance individuals hupenda kufanya mambo bila bugudha, bila kelele kinzani. Lakini kasoro yake hiyo haiwezi kutufanya tusione nchi aliikuta wapi na ameifikisha wapi, uthubutu wake, ufanisi wake, na matokeo yake.

Kama kuna tunachoweza kujifunza kupitia kasoro na mazuri ya JPM ni kwamba tumuombe Mungu kama nchi atuibulie mtu visionary, mzalendo, na results oriented anayeweza kuhimili vishindo vya sauti kinzani. Kitu tusichotamani kitokee tena ni kumpata kiongozi mediocre atakayetaka kumfurahisha kila mtu ikiwemo vyombo vya habari, huku mambo ya msingi ya nchi yanaharibika.
 
[emoji120][emoji120][emoji120]
 
Hii ripoyo imekuja strategically ili kutoa option badala ya restriction ndiyo maana kuna mtu nimesikia akisema .....tuendelee au..!.
Wananchi tunatak kazi iendele ova!...
 
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amepewa mwangaza wa kuanzia. CAG kaweka hadharani changamoto katika usimamizi na matumizi ya pesa za Umma.

Anapaswa sasa arekebishe kasoro zilizopo. Wale wote waliotajwa kwenye ufisadi huu wawajibishwe kisiasa na kisheria.
Miradi yote iliyoanzishwa na Mheshimiwa Magufuli inapaswa iendelee..hasa ile yenye tija kwa Taifa kama Bwawa la Umeme, Ujenzi wa reli ya kisasa, Elimu bure, Ujenzi wa daraja la Busisi, upelekaji wa umeme vijijjini na miradi mingine.

Miradi isiyo na tija kwa sasa inapaswa isimame. Mfano wa miradi isiyo ni pamoja na ununuzi wa Ndege. Zilizonunulia zinatosha, zisimamiwe vizuri, ufanyike utaratibu wa kuongeza mauzo ya ticket za ndege hasa kwa safari za ndani kwa kupunguza ukubwa wa nauli uliopo na pia kuanzisha route mpya ndani ya Nchi.

Ni dhahiri pia Serikali inao uwezo wa kutoa ajira mpya kwa vijana wengi waliomaliza masomo yao na kukosa ajira, hata kama ni kwa hatua. Kiasi cha pesa kinachopotea kwa kuibiwa ama kusimamiwa vibaya ni kielelezo Serikali inao uwezo wa kutoa ajira mpya.
Uzalendo ni pamoja na kukosoa pale penye matatizo. Kushauri na kuelekeza yaliyo sahihi. Uzalendo sio kuwazuia wakosoaji wako. Wote tunajenga Taifa hili... Tunahitaji kukubaliana hata kama mengine yanatufedhehesha.
 
Hivi ulimsikiliza Magufuli wakati anamwapisha Kichere kuwa CAG? Zile bit alikuwa anampiga kuwa asiende kuanzisha mhimili wake ilikuwa kuweka mazingira ya kumtisha CAG asije akafunua maovu ya serikali.

Prof Assad alisema kuna wizi lakini huyu huyu Ndugai alitishia kutofanya naye kazi na kumdhalilisha bungeni kwa kumvua viatu na mkanda hii yote ilikuwa kumtisha.

Magufuli alikuwa corrupt to the core ila alichofanikiwa ni kuwanyamazisha wabaya wake ili uovu wake usijulikane. Na huyu mtu asingelitoka madarakani kwa amani. Ama angeweka mtu wake baada yake au angetawala milele atake asitake kama walivyotuambia kina Ndugai.

Baada ya huu ufisadi wa Serikali ya Magufuli subiri sasa utakuja kusikia wa yeye binafsi. Hapo ndipo mtachoka kabisa nyie wafuasi wa kiongozi wa malaika
 
Umezungumza jambo zuri sana. Changamoto ni hii, je mfumo huu wa kulindana unaweza kuacha nafasi ya Taifa kupata mtu mwenye sifa ulizoziainisha?
 

Mkuu Hakimu Mfawidhi heshima kwako. Naomba unisaidie kidogo mkuu, hivi "Gawio" huwa linalipwa serikalini kutokana na Mapato "Ghafi" au "Faida"?

Ahsante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…