Leonel Ateba Mbinda
JF-Expert Member
- Feb 20, 2023
- 644
- 2,695
Sijaona uwezo wa kocha kabisa na kunifanya niamini kweli Simba inae kocha, tulicheza na Pamba tukashambuliwa hivi hivi Kama sio uhodari wa kipa Camara Leo Bravos alikuwa anatudhalilisha.
Kwanza Fahdu hajui kupanga kikosi kabisa zaidi ya kubahatisha, pili timu inacheza kwa kiwango cha chini mno, Tatu kuna wachezaji anawachukia bila sababu za msingi mfano ni Awesu Awesu, hata akiamua kumpanga basi anampanga kuturidhisha sisi na ndio maana kipindi cha 2 lazima amtoe hata Kama mpira anautaka.
Viungo Ngoma na Okajepha wanapooza sana pale Kati, Mavambo kiwango kimepungua sana, yaan huwezi amini kama ile ni Simba.
Huyu Ahoua ndio usiseme, kazi yake ni kupiga penati tu, hana lolote alilolifanya Leo, Mukwala ndio hamna kitu kabisa
Huwezi kuniambia kuwa unautaka ubingwa kwa kiwango kibovu namna ile