Kama kweli Mungu yupo, basi hana nguvu

Kama kweli Mungu yupo, basi hana nguvu

Eeh Mwenye Enzi Mungu, nakuomba msahama kwa kwa niaba ya huyu mleta uzi, wewe ni Muweza wa Yote, unayempa umtakaye na kumnyima umtakaye.

Endelea kutuzidishia imani, matumaini na mapendo, tunapoendelea na mwaka huu mpya, ili wewe uweze kudhihirka kwa wale wenye subra na wakutumainiao. AMEN
 
Ukifikiria sana haya maisha sometimes unaweza kufuru,ila yote kwa yote Mungu yupo ila ndo yataka uvumilivu sana,wakati umekata tamaa,akili yako imefika mwisho ndo unaona majibu

Sijui situation unayopitia ila kwenye maisha Kuna kuanguka na kuinuka,usikate tamaa mizimu Ina ghalimu lazima utoe kafara n.k.
 
Ndio shida ya kufanya jambo huku ukiwa na uhakika wa kwamba plan B yake ipo, huwezi kukifanya kwa ufanisi yaani kuingia miguu yote kwa maana unajua ukifeli huko huna pengine pa kukimbilia so uko na option moja tu.

Mambo ya kiroho yanahitaji maandalizi kwanza lakini pia inawezekana unachokiombea tayari kipo kwahiyo ni wewe tu kukifuata.
Mmhh maandalizi tena yaani Mungu mwenye mamlaka na muumba wa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo umfanyie maandalizi tena..
Sasa na waganga nao wasemaje maan kule ndio mambo ya kuku mbuzi ni kawaida.
 
Mmhh maandalizi tena yaani Mungu mwenye mamlaka na muumba wa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo umfanyie maandalizi tena..
Sasa na waganga nao wasemaje maan kule ndio mambo ya kuku mbuzi ni kawaida.
Nenda kasome biblia kitabu kile cha Mwanzo, anzia sura ya kwanza hadi ya sita pale (ishia tu hapo, wala usiende mbali, kisha ukimaliza kaa kwenye utulivu tafakari neno)... Utapata kujua kwanini ufanye maandalizi wakati wa kuomba na kwanini ukiomba maombi hayajibiwi na kadhalika.
 
Habari zenu Wanajamiiforums.
Kwa mda niliotumia kumuomba Mungu na kutokupata majibu yoyote, nahitimisha kuwa nguvu za Mungu si nyingi kama tulivyoaminishwa.

Aisee nataka kuamia Mizimuni, Anayejua namna ya kutambikia Mizimu anielekeze, Mungu aliyeletwa na meli kwenye maisha yangu amefeli (Hana impact yoyote).

Am done.
Mungu yupo na ana Nguvu sana
 
Mmhh maandalizi tena yaani Mungu mwenye mamlaka na muumba wa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo umfanyie maandalizi tena..
Sasa na waganga nao wasemaje maan kule ndio mambo ya kuku mbuzi ni kawaida.
imeandikwa usimjaribu bwana mungu wako kwa chochote hata kwa maombi bali muombe kwa moyo wako wote na kwa akili zako zote utamuona
 
Habari zenu Wanajamiiforums.
Kwa mda niliotumia kumuomba Mungu na kutokupata majibu yoyote, nahitimisha kuwa nguvu za Mungu si nyingi kama tulivyoaminishwa.

Aisee nataka kuamia Mizimuni, Anayejua namna ya kutambikia Mizimu anielekeze, Mungu aliyeletwa na meli kwenye maisha yangu amefeli (Hana impact yoyote).

Am done.
Kabla hujafikiria kumuomba Mungu hakikisha alivyokupa kama akili na afya umevitumia kwa ukamilifu,,,unaweza pia kutumia na akili za wanadamu wengine kupitia USHAURI..

Zaidi ya hapo tafuta sadaka umpelekee Mwamposa.
 
Back
Top Bottom