Kama kweli Paroko katajwa kimakosa kifo cha Albino, Polisi Mtawaambia nini Watanzania?

Kama kweli Paroko katajwa kimakosa kifo cha Albino, Polisi Mtawaambia nini Watanzania?

Sasa badala ya kuombeleza kifo cha mtoto na kutaka wote waliohusika wanyongwe ..tutaanza kutetea Imani zetu zisichafuke?..kwani hata akiwa Askofu...si ni yeye binafsi na uovu wake? Imani yake inaingiaje,?
Hata mimi nashangaa mkuu eti wafia dini wanadhani paroko kuhusika ni jambo la ajabu.

Hao hao mapadri, maparoko na maaskofu kila uchwao wana kashfa za kulawiti watoto sasa inashangaza nini paroko kuhusishwa na mauaji?
 
Nalipongeza jeshi la Polisi kwa kuatia nguvuni watuhumiwa wa tukio hilo. Msimamo wangu ni uleile, wasifikishwe Mahakamani.
Kuhusiana na huyo Paroko Msaidizi, kama ni kweli ni sehemu ya waliofanya upunguani huo, basi ni wakati wa Kanisa kuanza kujitathmini. Tumekuwa tukipigia kelele sana mwenendo wa kanisa na Mapadre na waumini. Sasa mdogomdogo athari zinaanza kuleta damage kubwa sana.
Mwisho, apenda kufahamu, huyo Padre Elipidius alihamishwa lini kutoka Parokia ya Rutabo?
 
Km ikibainika sio Paroko Polisi lazima wawajibishwe, Paroko hivi unamjua Paroko wewe Paroko?
Utataka polisi wawajibishwe kwa sababu walisema ni paroko au kwa sababu walimkamata na kumshikilia mtu asiye sahihi bila kujali cheo au dini yake??
 
Huyo wanayesema ni Paroko Msaidizi aliyekamatwa, mara ya mwisho rena mwaka huu alikuwa ni Padre wa Parokia ya Rutabo, siyo huko Bugandika.
Nimeshangaa kuona kwenye taarifa akitajwa kuwa ni Paroko Msaidizi wa Bugandika.
Sasa Polisi ndio watolee maelezo hapo
 
Professionally jeshi la polisi wamekosea sana kuripoti habari ya uhalifu na kutaja cheo au wadhifa wa mtu sababu technically hiyo itamaanisha taasisi nzima imehusika.
 
Huyo wanayesema ni Paroko Msaidizi aliyekamatwa, mara ya mwisho rena mwaka huu alikuwa ni Padre wa Parokia ya Rutabo, siyo huko Bugandika.
Nimeshangaa kuona kwenye taarifa akitajwa kuwa ni Paroko Msaidizi wa Bugandika.
Sasa mbona wakatoliki wengine wanamkataa wanasema alikuwa teja mlevi tu?!
 
Utataka polisi wawajibishwe kwa sababu walisema ni paroko au kwa sababu walimkamata na kumshikilia mtu asiye sahihi bila kujali cheo au dini yake??
Unachafua kanisa alafu unatarajia nini inabidi ulisafishe la sivyo Sheria zifuate mkondo wake yule mropokaji wa Polisi afikoshwe mahakamani kwa kuropokaropoka ovyo bila kijiridhisha km ni kweli au sio kweli
 
Msemaji wa jeshi la polisi kachemka na kwenye hili litamkosti
Aliyekamatwa siyo Paroko msaidizi na wala siyo padre.
Ni mraibu ambaye paroko msaidizi alisoma naye aliamua kumchukua parokiani ili aweze kusaidiwa.
Hivyo kumtaja kama baba padre ni watu kutokutumiza majukumu yao katika kufuatilia mambo .
Paroko anaitwa Deodatus Tibakwasa na msaidizi ni Fr.Mathias.

Inasemekana Padre alimsajilia mtu line kwa kutumia kitambulisho chake hivyo wakati wa upelelezi na kutrack simu zilizotumika ndo akatiwa korokoroni kwakuwa jina lilisoma la kwake. Ndo maana huwa daima ninalia na reporters wetu ktk uandishi wa taarifa.
 
Professionally jeshi la polisi wamekosea sana kuripoti habari ya uhalifu na kutaja cheo au wadhifa wa mtu sababu technically hiyo itamaanisha taasisi nzima imehusika.
Watuhumiwa wote wanapokamatwa na polisi huwa wanatambulishwa kwa kazi zao na ikiwezekana hata vyeo vyao katika taasisi zao, viongozi wa kanisa katoliki sio kundi lenye hadhi maalum kwamba wasitambulishwe kwa utaratibu huo.
 
Back
Top Bottom