Kama kweli Yesu aliteseka msalabani kwaajili yetu ili tusamehewe dhambi zetu, sisi tunatubu ili iweje?

Tabia ya Mungu au niseme utaratibu wa Mungu ni kwamba ukitenda dhambi lazima ufe, damu imwagike kabisa. zamani hizo wanadamu wakitenda dhambi ilitakiwa wamwage damu walau ya mnyama, kwa niaba ya dhambi ile waliyoitenda. meaning, ukitenda leo utamwaga damu na ile damu inahudu dhambi hiyo tu, haihusu dhambi utakazofanya keshokutwa au mwakani, hizo zitahitaji umwagaji damu wake. waisrael wamekuwa wakimwaga damu za kondoo, mbuzi, ng'ombe, na njiwa kwa namna hiyo kwa ajili ya upatanishi, ama la wao ndio wangekufa. mnyama unayetoa sadaka hiyo ya dhambi alitakiwa awe msafi, asiye na madoadoa wala uchafu wowote.

katika Agano Jipya, Mungu akaleta utaratibu mpya, ipatikane Damu ya mtu ambaye hana hatia kabisa yaani hajawahi kutenda dhambi, mtakatifu na msafi, ili afe kama sadaka ya kuchukua dhambi badala ya ng'ombe na mbuzi kuchinjwa kama sadaka. hakuna mwanadamu yeyote wa kawaida ambaye angeiweza hiyo kazi kwasababu wanadamu woote wana asili ya udhaifu wa dhambi, hata wale wanadamu waliopaa mbinguni kama kina Eliya, walishatendaga dhambi. hivyo, Mungu yeye mwenyewe akafanyika mwili (akaingia kwenye mwili wa mwanadamu ili auvae mwili huo kwa kuzaliwa kama mwanadamu), aishi kama mwanadamu, asitende dhambi yeyote, na asiwe na mbegu (sperm) ya mwanadamu ili Damu isiwe ya kibinadamu bali Damu ya Kimungu, aishi maisha ya kibinadamu, ashinde dhambi zote, halafu auawe kama kafara la dhambi za wanadamu wote. huyo ndiye Yesu Kristo aliyezaliwa pale Bethlehem.

kwa kifo chake, ukitenda dhambi, badala ya kuchinja ng'ombe, unatubu kwa kumwamini yeye, unasamehewa bila gharama yeyote nyingine, imani tu. wapo wachungaji manabii wa uongo wamejitokeza siku hizi wanasema kwasababu Yesu alikufa, hatutakiwi kutubu tena na watenda dhambi hawataenda motoni kwasababu Yesu aliichukua dhambi yetu yote. NO, ukitubu leo Yesu anakusamehe dhambi uliyotubu, ukitenda dhambi kesho baada ya kutubu, hiyo mpya haitasamehewa hadi utubu na kuacha, ama la utaenda nayo motono.

kwahiyo, kile kitendo chetu cha kutubu kwa specific dhambi, ni sawa na kwenda zizini na kuchagua mnyama wa kuchinja badala ya dhambi uliyoitenda. Yesu alichinjwa badala yako hivyo ukitubu kwa Jina lake, unasamehewa specific dhambi uliyotubu. hausamehewi zile utakazotenda kesho na keshokutwa, ndio maana kutubu kutakuwepo kila siku, unapaswa kujitakasa kila siku ukijua mwanadamu ana madhaifu kila iitwapo leo.

na sio dhambi tu, Yesu Kristo aliyachukua hata magonjwa yetu, aibu yetu na huzuni zetu. Isaya 52 na 53 inaeleza kwamba, jinsi alivyoishi awali, alikuwa mtu anayedhaniwa ni dhaifu, aliyedharauliwa hadi watu walitema mate wakimwona, alikuwa mtu wa huzuni nyingi mno na masikitiko, Yesu hakuishi maisha ya furaha. kwa kifupi, ili wale watakaomwamini waishi maisha ya furaha, yeye alibeba huzuni/aliishi maisha ya huzuni muda wote na masikitiko, aliposulibiwa aliumizwa mwili kwa mijeledi na kipigo ili kwa kupigwa kwake sisi tupone miili yetu isipate maumivu, hata tukipata anao uwezo kuyaondoa kwasababu aliyashinda na alilipa garama hiyo, alimwaga damu ili kwa Damu yake iwe kafara la dhambi za dunia nzima, meaning, yeyote ulimwenguni akija kwake kumwamini na kutubu, dhambi yake inalipika/inasameheka kwasababu alilipa deni la dhambi yeyote itakayofanywa na wanadamu wowote wale waliokuwepo na walioendelea kuzaliwa, deni lililipwa.

usijichanganye tunaposema Yesu alilipa deni, hii haimaanishi deni lilishalipwa hivyo tufanye tu dhambi hatutaadhibiwa kwasababu alilipa, NO, inamaanisha, ukifanya dhambi, badala ya kugarimia ng'ombe au kondoo, yeye alishamwaga Damu yake badala ya mang'ombe na makondoo, atakusafidha dhambi yako (ile tu unayotubu sio zile za kesho na keshokutwa hizo zitahitaji kutubu kupya).

na hakuna njia nyingine ya kusamehewa dhambi, wanadamu wote wasiopitia njia hii wataenda motoni moja kwa moja, meaning, waislam,wabudha na kadhalika wote imani yao haitawaokoa, ni watu wa motoni.
 
Kwa maneno mengine ni kwamba alikua anafanya maigizo?
 
Mbona unanichanganya KRISTU au KRISTO yupi ni yupi?
 
VP kuhusu Kwa wasabato na wengine ?
 
Tatizo kila viashiria vipo vya Mungu hayupo vipo na vya Mungu yupo vipo
 
Kuna mambo hayaingii akilini;

1. Kwamba Mungu alieumba dunia yote na vyote vilivyomo, ili akusamehe dhambi alihitaji damu ya ng'ombe, mbuzi nk la sivyo unakufa! Hii ina tofauti gani na ibada za mizimu walizokua wanafanya babu zetu???

2. Kwa maelezo yako, hakuna mwanadamu yeyote wa kawaida ambaye angeiweza hiyo kazi kwasababu wanadamu woote wana asili ya udhaifu wa dhambi. Kama wanadamu wote tumerithi dhambi kwa KUZALIWA na mwanadamu, iweje YESU nae azaliwe na mwanadamu yuleyule alierithi dhambi? Hii haimfanyi nayeye kurithi hiyo dhambi?

3. Hili suala la kwamba MUNGU alilazimika kujifanya mwanadamu, akateswa, akafa, akafufuka, ili MUNGU huyo huyo aweze kutusamehe dhambi tulizotenda KWAKE, ni kizungumkuti!

4. Umesema YESU alichukua sio tu dhambi zetu, bali na magonjwa yetu. Sasa kama ni hivyo mbona bado tuna magonjwa na tunatakiwa kutubu dhambi. Ina maana YESU alikufa kwa ajili gani..? Yaani maisha ya mwanadamu wa kabla ya YESU na baada ya YESU yamebadilika vipi kutokana na ujio wake, kama kila kitu kipo vile vile??
 
Ukiweza kujijibu hili swala utakua umeelewa pakubwa sana..

Dhambi ziliumbwa na nani?
 
Mimi ninavyoona haya mambo ya Mungu sisi wanadamu tunayajua kwa umbali sana sana yaani ni kama kipunje Cha ulezi ndo tunajua. Ila Kuna Mambo makubwa sana Kuhusu Mungu hatuyajui bado. Sasa hapa Kikubwa Wacha tuamini kwenye kakiwango hako hako kama kapunje ka ulezi. Mengine tutayajua Yesu akija au tukienda kukutana nae tutamuuliza maswali naamini atatujibu na atatuonesha Shetani na pia tutapata Fursa ya kumuuliza Shetani maswali chini ya usimamizi wa Yesu mwenyewe.
 
Huo ni mchongo tu ndio maana Wayahudi wenye akili mpaka leo hawaamini. Ila waliochonga nafikiri walitumia ulimwengu wa roho.
 
Inawezekana pia hatuyajui kabisa, hata hicho tunachodhani tunajua huenda hatujui na hatujui kama hatujui.
 
Aliweka upatanisho, nafasi ya kupata msamaha. Vinginevyo ilikuwa "One mistake, one goal"
 
Mi naona hao Wanafunzi wa Yesu na Mitume wengine kama Muhammad, hawakututendea haki, walipaswa kuuliza maswali magumu kabisa yanayohusu Mungu na uumbaji. Walipaswa kuuliza maswali mengi kabisa mpaka kusiwepo na Mashaka yoyote. Anagalau Musa aliwahi kuuliza kinachoaminika kuwa Mungu kwamba kwani wewe ni Nani? Akasema "Mimi Niko ambaye Niko" "I am who I am"
 

Kama Baba yako ananunua maji ya kunywa kwa gharama zake na kuweka kwenye fridge, kwa nini ni lazima uchote na unywe? Ina maana akishanunua tu kiu yako inaisha!
 

Mbona mtume Muhammad aliuliza maswali Magumu na Mungu akajibu

Alitaka kujua kama kweli Yesu alisurubiwa na alikufa Mungu akajibu

Quran 4:157
- Na kwa kusema kwao: Sisi tumemuuwa Masihi Isa, mwana wa Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu - nao hawakumuuwa wala hawakumsalibu, bali walifananishiwa tu. Na hakika walio khitalifiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana ujuzi nayo wowote, ila ni kufuata dhana tu. Wala hawakumuuwa kwa yakini.
 
Kanuni ilikuwa kwamba MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI.

Ndio maana wakati wa torati ya Musa, kulikua na sadaka za kuchinja ili kusamehewa dhambi.

Tendo la Kifo cha Yesu ilikua ni kuondoa ile kanuni ya Kifo kwa wanadamu wanapotenda dhambi.

Hivyo kwasasa ukitenda dhambi, badala ya kufa, kile kifo cha Yesu kinafidia hapo, na badala ya kutoa sadaka za kuchinja, Damu ya Yesu isiyo expire, damu ya thamani, inatosha kabisa kutumika kukutasa.

Kuhusu Yesu Kuwa Mungu hili ni jambo hata mimi kama mkristo nalifanyia utafiti kwa kujifunza. Japo maelezo mengi yanakuacha na maswali.

Wengine husema kwakua Mungu ni Roho ili aje ulimwenguni na kufanya hilo zoezi (kusulubiwa,kufa msalabani na kufufuka) ilibidi apitie mchakato wa kuwa na mwili wa damu na nyama (kuzaliwa)...

ukisema Mungu wako hawezi kufanya hivyo, bhasi tayari huyo sio Mungu. Kwani sifa ya Mungu ni KUWEZA YOTE.

Na ukikubali Yesu ni Mungu, Je kwanini alikua akimuomba Baba wa Mbinguni? Ukisema utatu mtakatifu, Biblia haijawahi andika neno utatu mtakatifu Mwanzo mpaka ufunuo hilo neno halipo.

Je Mimi naamini nini?
Naamini Yesu ni Mwana wa Mungu ( haina maana Mungu alizaa, bali ni cheo tu kuonyesha ukaribu wa Mungu na Yesu).

Naamini Yesu alikuja duniani kwa kazi ya kuleta msamaha wa dhambi kwa njia nyepesi zaidi na yenye upendo, na si hasira kama gharika au moto wakati wa sodoma.

Ndio maana mpaka leo, Hakuna Jina Lenye Mamlaka Ya Kiroho kama jina la Yesu. Kwa lugha yoyote inayotumika ilimradi unamaanisha YESU KRISTO, kuna nguvu, mapepo, majini, wachawi, mizimu vyote vinasalimu.

Sihitaji mafuta wala chumvi kushughulikia kazi za giza, nikijua kulitumia Jina la Yesu tu. Am Untouchable.

Ukimuona Muislamu Yoyote anamdhihaki Yesu bhasi jua huyo ni muislamu asie isoma Quran vema, kwani Yesu ambae wao wanamuita nabii Issa Ameandikwa kwa heshima kubwa katika Quran.

Hilo tu linatosha kujua YESU hakua wa kawaida kawaida.


Yesu alieandikwa kwenye Biblia matukio yake ni ya kweli na hakika, kwani timeline yake, imethibitika kupitia nyakati za watawala waliokuwepo wakati huo, ushahidi wa kaburi kuonyesha alikuwepo kweli, na historia za kawaida za wakati huo.

Ushahidi unaomthibitisha Yesu na maisha yake ni mkubwa sana, kuliko unaopindisha.

Asante.
 
Hizo ni story tu za kuibia wajinga!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…