LGE2024 Kama lile ndio Daftari la kujiandikisha kupiga kura, Professor Assad yuko Sahihi kuwa hatapiga kura

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Sasa kuna haja gani ya kujiandikisha kabla ya uchaguzi?? Si watu wangesubiria tu siku ya uchaguzi unapiga kura kisha unajiandikisha hapo hapo kwa wakati mmoja.
Ni kweli utaratibu wa kujiandikisha ni mwepesi. Lakini, kwa utaratibu wa sasa wa kupiga kura za siri. Lazima vifaa viandaliwe vya kupiga kura kulingana na idadi ya watu. Hivyo. Itakuwa vigumu kuunganisha kazi hizi mbili siku moja ( kuandikisha na kupiga kura)
 
CCM ndiyo wanataka hivyo, nadhani tushiriki kwa wingi na kuwadhibiti kwa njia zote ikiwezekana hata kwa kutumia waganga wa jadi
Tatizo la upinzani wanahamishwa na matukio mara katiba mpya mara tume huru, mara bandari , wange simama na kimoja ungekuta mfumo umebadilika na kuleta hamasa kwa sisi wapiga kura , kwa kinachoendelea kwa sasa bila kupepesa macho ni njaa ya madakara tu kwa pande zote mbili.
 
Uongozi imara unaanzia chini, hatuwezi kusema hili ni sawa kisa ni ngazi ya chini
Ni kweli usemacho. Viongozi wanatuona wananchi mafala sana. Na waandikishaji nao wanaamka asubuhi kwenda kufanya hiyo kazi. Wanachotaka ni kukatisha tamaa watu wasiende kupiga kura. Lakini wamenoa
 
Tatizo la upinzani wanahamishwa na matukio mara katiba mpya mara tume huru, mara bandari , wange simama na kimoja ungekuta mfumo umebadilika na kuleta hamasa kwa sisi wapiga kura , kwa kinachoendelea kwa sasa bila kupepesa macho ni njaa ya madakara tu kwa pande zote mbili.
Huwezi kubeza mchango wa wapinzani, hawa watu wamesaidia sn taifa letu vinginevyo hali ingekuwa mbaya zaidi, sema kupambana na mifumo dhalimu kama ya CCM ni kujitoa mhanga, kufungwa, kutekwa na kuuawa, kufilisiwa na maovu yote yale, mimi wapinzani nawaheshimu sn wanapitia matatizo makubwa sn hata kwa usalama wa familia zao, juzi mke wa Mbowe kakamatwa anaenda kazini hospitali tena daktari bingwa wa watoto na hahusiki na siasa + mtoto + baba, siyo mchezo kuwa mpinzani ni bora uwe gerezani.
 
Jana nilienda kujiandikiasha ili kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa. Nikakuta kumbe unataja majina yako matatu, unaweka sahihi, msimamizi nae anaweka sahihi halafu ndio imetoka hivyo.

Yaani Nikajiuliza na kucheka tu, ni Watu wangapi wataingizwa ambao ni fake? Waandaaji wameshindwaje hata kutumia akili za kawaida Tu nyingine kuchukua tahadhari ya Watu wasiostahili kutokuingizwa au kuandikwa?

Kwa muktadha huu, Watu WA CCM wataenda kujifungia na hili daftari na kuandika majina yoyote kwa idadi yoyote ile na HAKUNA kitu kitatokea.

Nishauri Tu kuwa, ni muhimu sana kutumia akili zetu KULIKO SIASA kwenye kitu muhimu kama hiki.
.
Daftari gani huulizwi hata unaishi wapi, huulizwi kitambulisho, huulizwi taarifa zozote zile zaidi ya kutaja jina na kusaini?

Leo nitaenda kujiandikisha kituo kingine tena na nitawapa mrejesho na mniambie kama kuna umuhimu WA uchaguzi wa kipumbavu namna hii
Yes,
nawe kaa nyumbani kwako kwa kutulia sasa na usilete kimbelembele na kubweka bweka baadaee, sijui eti ng'weee ng'weee nini, sawa?🐒
 
Uongozi imara unaanzia chini, hatuwezi kusema hili ni sawa kisa ni ngazi ya chini
Tena ni uongozi muhimu sn kwenye taifa kuliko hata mbunge au diwani, Mwenyekiti wa mtaa tupo naye masaa yote siku zote tofauti na Mbunge anaonekana kwa vipindi.
 
Mkuu huu uchaguzi tungetumia mbinu na utaratibu wa uchaguzi mkuu Tu kuliko njia hii ya kuandikisha jina na kuondoka
Nadhani utofauti wa set up ya serikali za Mtaa na serikali kuu ndiyo inaleta utofauti kwenye masuala haya. Hata hivyo, nchi hii ni yetu sote. Kwa hiyo, maoni ya kuboresha uendeshaji wa nchi yanatakiwa kuzingatiwa. Na kwa kuwa Jukwaa hili linapitiwa na wahusika, maoni yako haya yatatazamwa kwa kina.
 
Huwezi kubeza mchango wa wapinzani, hawa watu wamesaidia sn taifa letu vinginevyo hali ingekuwa mbaya zaidi, sema kupambana na mifumo dhalimu kama ya CCM ni kujitoa mhanga, kufungwa, kutekwa na kuuawa, kufilisiwa na maovu yote yale, mimi wapinzani nawaheshimu sn wanapitia matatizo makubwa sn hata kwa usalama wa familia zao, juzi mke wa Mbowe kakamatwa anaenda kazini hospitali tena daktari bingwa wa watoto na hahusiki na siasa + mtoto + baba, siyo mchezo kuwa mpinzani ni bora uwe gerezani.
Ni kweli mimi pia naheshimu hili na nina amini upinzani sio chama ni ideology iliyopo ndani ya mtu kupinga uovu fulani .
 
Ni kweli utaratibu wa kujiandikisha ni mwepesi. Lakini, kwa utaratibu wa sasa wa kupiga kura za siri. Lazima vifaa viandaliwe vya kupiga kura kulingana na idadi ya watu. Hivyo. Itakuwa vigumu kuunganisha kazi hizi mbili siku moja ( kuandikisha na kupiga kura)
Kwani sensa ya mwaka 2022 sio pamoja na kukadiria idadi ya wapiga kura?
 
Jana nilienda kujiandikiasha ili kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa. Nikakuta kumbe unataja majina yako matatu, unaweka sahihi, msimamizi nae anaweka sahihi halafu ndio imetoka hivyo.

Yaani Nikajiuliza na kucheka tu, ni Watu wangapi wataingizwa ambao ni fake? Waandaaji wameshindwaje hata kutumia akili za kawaida Tu nyingine kuchukua tahadhari ya Watu wasiostahili kutokuingizwa au kuandikwa?

Kwa muktadha huu, Watu WA CCM wataenda kujifungia na hili daftari na kuandika majina yoyote kwa idadi yoyote ile na HAKUNA kitu kitatokea.

Nishauri Tu kuwa, ni muhimu sana kutumia akili zetu KULIKO SIASA kwenye kitu muhimu kama hiki.
.
Daftari gani huulizwi hata unaishi wapi, huulizwi kitambulisho, huulizwi taarifa zozote zile zaidi ya kutaja jina na kusaini?

Leo nitaenda kujiandikisha kituo kingine tena na nitawapa mrejesho na mniambie kama kuna umuhimu WA uchaguzi wa kipumbavu namna hii
Hata mimi nimejiandikisha juzi. Makarani hawanijui wala mimi siwajui, hawakuniuliza chochote mbali na majina matatu na umri. Nikaona kabisa naweza kwenda kujiandikisha mtaa mwingine tena. Kuna uwezekano mkubwa wa daftari kujaa majina ya kubumba.

Sintapiga kura.
 
Wewe hutajiandikisha maana kwa ratiba yako Hata muda wa kupiga kura hutaupata.
===
Ndiyo maana Kuna mawakala kuhakikisha anayejiandikisha ni mwanamtaa halali.

Tenga muda ukajiandikishe pitia kwa Mjumbe wako wa Mtaani ujitambulishe atakusaidia kuaminika kwa wahusika wa uhandikishaji. Pia tarehe 27/10/2024 ukapige kura hapo hapo ulipojiandikisha.
wakala anajua watu wote wa mtaa huo?
 
Tuanze na wewe kuacha kutetea huu ujinga kwanza
H ha hahahaha aaa! Mkuu najaribu kuwa objective ili tueweze kusonga mbele, Mkuu. Tukisusa watakula wao tu! Tunatakiwa kula wote njia ya kufanikisha hili ni kushiriki sote kwa umoja wetu kushughulikia masuala yetu kama nchi.
===
Wakuu Asubuhi njema, sitaweza kuendelea kujibu hoja kwa Sasa hadi wakati mwingine. Mbarikiwe.
 
Back
Top Bottom