Wewe kubali tu kuwa Mheshimiwa Makonda ndiye mwenezi wetu wa CCM Taifa na Anaendelea kuchanja mbuga katika mioyo ya watanzania,ambao wanaendelea kupaza sauti zao kutaka apokee Urais kutoka kwa Mh Rais Samia Mwaka 2030.
Si ni wewe ulikuja na uzushi wako humu kuwa makamu mwenyekiti wa CCM mh kinana anataka kujiuzulu kwa sababu hakubaliani na uteuzi wa Mh Makonda? Yapo wapi sasa uliyozusha ewe mnafiki mkubwa usiye na haya wala soni.?
Wewe ni mnafiki na unayeteseka sana kuona mh Makonda akikubalika kwa watanzania.lengo lako limeshindwa na utaendelea kushindwa siku zote ,.maombi yako mabaya kwa mh makonda yatakurudia mwenyewe na uzao wako.
Huwezi kushindana na mheshimiwa Makonda kwa namna yoyote ile,hutaweza kumzuia Mheshimiwa Makonda kwa njia yoyote ile. Makonda ni mpango wa Mungu katika kumuandaa kwa nafasi za juu kuongoza Taifa letu.hivyo vita yoyote ile na silaha yoyote ile utakayo iinua kamwe haitafanikiwa maana itakutana na mkono wa Mungu ulio imara na hodari.
Fanya uwezavyo lakini huwezi kuzuia wala kuondoa kibali cha Mwenyezi Mungu kilichowekwa kwa Makonda.hujiuliza kwanini anakubalika kiasi hiki? Hujiulizi kwanini anapokelewa kwa kishindo huko mikoani? Hujiulizi kwa nini Taifa limekuwa na matumaini makubwa juu yake na kumtabilia makubwa huko mbele?
Ungekuwa na akili japo kidogo tu ungetambua ya kuwa Mheshimiwa Makonda ni mpango wa Mungu Mwenyewe