Naamini Mbowe anaweza kushinda sababu ya kwamba viongozi wa chadema at least 90% wamekua kisiasa au kuingia chadema kwa invitation na mentorship ya Mbowe including Lissu.
Having said that, Mbowe akitumia incumbency, intimidation, threats na figisu kushinda ndio ataharibu ila akikeep his cool apige kampeni kwa wajumbe mbona atashinda tu na ndio demokrasia tunayotaka.
Tatizo ni hawa machawa, wanataka apite bila kupingwa au ashinde kwa kishindo na ndio wataharibu hata ushindi wake (in case atashinda).
Mimi ni Team Lissu ila nina uhakika hata Lissu akishinda itakua 50-55% hata Mbowe hawezi pata zaidi ya 60%. Kwa lissu itakua ni ushindi ila kwa mbowe 50-55% ya ushindi itakua imetia doa credibility yake na mandate. Kwahiyo hawa machawa ndio watataka wafanye figisu zote ili Mbowe ashinde kwa 90%!! Na hiki ndio kinafanya waanze rafu mapema sana licha ya Mbowe mwenyewe kuwa kimya.
Ushauri: Mbowe achague, agombee na ashindwe au ashinde kwa simple majority akose mandate au ajitoe ili watu wengi zaidi wachukue fomu na ndio tuone demokrasia ya kweli. Otherwise matokeo yotote yale yatakua damage kubwa kwa Mbowe na chadema