Mimi sio mfuasi wa mfalme zumaridi na simjui na sijawahi kuonana nae ! Nachokipenda kwa zumaridi ni shepu yake safi 👏tatizo langu ni jeshi la polisi mara zote wanamkamata kwa kosa hasa la yeye kujiita MUNGU !!
Si mara moja bali ni mara zote zumaridi amekuwa akijiita mungu na wafuasi wake maelfu ya watu wenye akili timamu ,wasomi na wasio wasomi wamekubali kwamba yeye ni mungu wao !! Ikiwa jeshi la polisi linamashaka na uungu wake ama polisi wao wanae mungu halisi ambae sio mfalme zumaridi itakuwa zumaridi anapotosha watu ,kwa hivyo nalishauri jeshi la polisi pasi na shaka yoyote wamlete huyo mungu wa kweli mahakamani ili kuthibitisha uongo wa mfalme zumaridi ,
Soma Pia: Mfalme Zumaridi akamatwa na Polisi Mwanza
Na kama polisi watashindwa kumleta Mungu halisi mahakamani basi mfalme zumaridi hana hatia yoyote !!! Kwa habari ya kelele waanze nà makanisa yote nchi nzima wachungaji wote wawekwe ndani kwa sababu hakuna kanisa kwa Sasa ambalo Lina soundproof na kwa habari ya kwamba kanisa lake halijasaliwa ukweli ni kwamba asilimia 75 ya makanisa ya kiroho hayajasajiliwa kabisa !!
Mtu tu anaamka anasema hili ni kanisa linaitwa mganguzi basi iyena iyena ! Wakamatwe wachungaji wote ambao hawajasajili makanisa wawekwe korokoroni !! Hapo mtakuwa mmefanya kwa usawa lakini kumlenga zumaridi pekee ni kumuonea !!!