Kama mfalme Zumaridi sio Mungu basi jeshi la polisi limpeleke Mungu halisi mahakamani kuthibitisha uongo wa mfalme Zumaridi

Akiwaua watu kama Kibwetere au Mckenzie bado mtaandika uzi wa kuilaumu serikali. Mleta uzi jua kwamba serikali ya Tanzania iko macho muda kupitia vyombo vya dola. Ukivuka mstari lazima utulizwe. Kuna mambo mengi sana serikali hutumia busara sana... ikisema ianze kamata kamata magereza hazitatosha. Kinachofanyika ni ku-control tu mambo.. wanaovuka mstari wa ustaarabu kama Zumaridi hukutana na kibano.
 
Kondoo najua hujui hunenalo!

Ila leo nakupa zawadi ya bora maishani mwako na ukitumia Akili itakusaidia sana wewe na kondoo wenzio.

Chukua Bible nenda Yohana 7:14-28
Utapata kujua kitu ambacho hakuna mchungaji amewahi kukusomea andiko hilo.

Ningekuwekea hapa ila naogopa utasema nime edit.
 
Aisee
 
Hizo ni hisia zako zilizochanganyika na wivu
 
Sio Kila mungu haonekani ni huyo wako tu ndie mmemuweka kwenye makanisa ,nenda nchi za ufilipino,Indonesia,India, utaona kuna mungu ng'ombe ,na wanamshika na hata kumuogesha
 
Sio Kila mungu haonekani ni huyo wako tu ndie mmemuweka kwenye makanisa ,nenda nchi za ufilipino,Indonesia,India, utaona kuna mungu ng'ombe ,na wanamshika na hata kumuogesha
Kwa hiyo mungu hata kuoga mwenyewe hawezi sasa hapo mbona kama anaemuogesha mungu ndo mungu?

vijana mmeshahalibiwa na hakuna cha kufanya tena juu yenu!
 
Kwani mkuu kikawaida binaadamu hadi kufikia kifo chake si anapitia hizo hatua?
Hatua ninazo zungumzia si hatua za kuzaliwa ,kuzaa na kuzeeka Kisha kufa .

Wao wanajiita miungu .Mungu hawezi kupitia hatua za kuzaliwa , kuzaa na kuzeeka Kisha ndo mauti ya mkute .


Yesu alijua kuwa atapitia hatua za mateso na hatimaye kuuwawa .Yesu hakupitia hatua ya kuzeeka hata kufa.
 
Kama Yesu wa Tongolani tu walishindwa kumleta Yesu ili wathibitishe kuwa Yeye is Yesu,basi mahakama ikabariki yeye ni Yesu wa TONGOLANI ,
 
Sijakusudia kupitia uzee ila nimekusudia kuwa watu wote wanaokufa hupitia hizo hatua, yote kwa yote kinachozungumziwa ni kifo kama kifo ambacho kila binaadamu hukipitia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…