Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Kujenga chama siyo lelemama,siyo kazi nyepesi wala rahisi wala kazi ya Mzaha mzaha.kujenga chama na kuwafikia wanachama na kutafuta wanachama wapya na kueneza sera ,itikadi ,misimamo na ajenda za chama Ni kazi Ngumu sana.
Ni kazi ya jasho na Damu,ni kazi ya kujitoa na kujitolea,ni kazi ya suruba lakini kubwa kuliko yote ni kuwa kujenga chama ni gharama kubwa sana tena sana inayohitaji rasilimali fedha za kutosha pamoja na watu wa kutosha na wenye weledi,ushawishi na kukubalika kwa watu.
Ndio Maana kuna vyama vinajitokezaga katika kutoa matamko tu au kuchukua Fomu ya Urais na kwenda kujifungia makabatini bila kwenda kufanya kampeni walau hata kata moja tu ndani ya wilaya moja tu. Ndio maana vipo vyama vingi tu hapa Nchini havina uwezo wala ubavu wa kuandaa mkutano au mawakala au kuweka mawakala katika kila kituo au kusimamisha wagombea katika kila nafasi na maeneo mbalimbali.
Hii ni kwa kuwa havina pesa wala watu wa kuvisaidia wala kuvichangia hata mafuta ya gari la kukodi wala hata pesa ya kukodi meza ya kuweka vitabu na makabrasha yao.
Chama kama CHADEMA kinahitaji kuwa na Mwenyekiti aina ya Mwamba na Jabali la siasa Mheshimiwa Mbowe mwenye Uwezo binafsi wa kiuchumi,marafiki kibao wenye pesa na uwezo mzuri wa kiuchumi,ushawishi wa jumuiya mbalimbali kuanzia wafanyabiashara wakubwa ,baadhi ya watumishi wa umma,wadau mbalimbali ndani na nje ya Nchi n.k.ambao wanaweza kukichangia chama hadharani na gizani kama ilivyokuwa kwa watu kama SABODO.
Ifahamike ya kuwa Ruzuku pekee ya chama haitoshi na ni kidogo sana kuweza kuendesha shughuli zote za chama kuanzia makao Makuu mpaka huku chini kabisa.kuzunguka nchi nzima na kufanya mikutano Maeneo mbalimbali ni gharama kubwa sana.hapo bado kipindi cha uchaguzi ambacho kinahitai pesa za kutosha kwa ajili ya zoezi hilo gumu,zito na lenye gharama kubwa sana katika kukamilisha mchakato wake wa kuhakikisha chama kinakuwa na uwezo wa kutoa ushindani wa kutosha.
Mbowe alijitahidi sana kukiwezesha chama kupata ufadhili kutoka kwa watu mbalimbali kutokana na ushawishi alio nao.
Lakini Leo hii CHADEMA ijiroge impatie Lissu uenyekiti wa chama Taifa ni wakati imesaini hati ya Kifo.Kwa sababu lissu hana ushawishi kwa watu kuweza kukichangia na kukiwezesha chama katika shughuli za kichama,lissu hana ushawishi kwa makundi muhimu yenye uwezo wa kukichangia chama mfano wafanyabiashara na matajiri wakubwa wakubwa.
Kwa sababu watu hao hawawezi na hawataki ukaribu na lissu kwa sababu wanajua lissu ni mropokaji , mkurupukaji na mwenye Mihemuko sana.ikumbukwe watu aina hiyo wanapenda kusaidia pasipo kujulikana au kutaka hata kutajwa hadharani.lakini kwa Mdomo wa lissu wanajua kuwa haujawahi kuwa na utulivu wala kutulia.ndio maana hawawezi kamwe kuwa karibu naye na kutaka mazoea naye iwe hadharani au gizani.
Hivyo basi chama kinaweza kukosa misaada na hivyo kushindwa kabisa kufanya lolote lile la maana la kujijenga .ikumbukwe ya kuwa uhai wa chama ni kuwepo midomoni mwa watu muda wote.na ili kufanikiwa katika hili ni kukipeleka kwa watu kila siku kwa ajenda,sera,n.k.
Sasa huyu lissu ameshindwa hata kupata na kutimiza michango ya kununulia gari la kutembelea. karibu mwaka sasa anahangaika tu kukusanya na bado haitoshi .ni vipi sasa atapata misaada kwa ajili ya kukijenga chama? Kama Ameshindwa kuwa na ushawishi kwa watu ndani na nje ya Nchi kumsaidia kupata gari mpya ni vipi ataiwezesha CHADEMA kupata uungwaji mkono kutoka kwa watu wenye uwezo na ushawishi? Hamuoni kuwa lissu amezungukwa na watu wababaishaji na wasio na misaada na mchango wowote ule? Sasa watu kama akina SATIVA ndio watasaidia nini kwa CHADEMA? Watu kama akina Maria Sarungi wataisaidia nini CHADEMA zaidi ya kuimaliza na kuingamiza?
CHADEMA ni wakati wenu wa kumpigia kura za ndio Mheshimiwa Mbowe Mwamba na Jabali la siasa za Upinzani kwa kishindo kikuu kitakacho itetemesha Dunia nzima .Msikosee wala kufanya majaribio katika jambo hilo nyeti na lenye kubeba Uhai wa chama.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.