Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sasaivi wanasema wana Wanachama Milioni 12. Na bado mnawaamini.Hata hili la kuaminishwa kuwa CCM ni chama Cha siasa na ilisajiliwa katika mfumo wa vyama vingi 1992 ni uongo mkuu.
Msajili wa vyama nchini ukimuomba hati ya CCM kusajiliwa kama chama mojawapo Cha siasa nchini katika mfumo wa vyama vingi,hatia hiyo Hana, na hajiulizi kwann yupo ofisini!Sasaivi wanasema wana Wanachama Milioni 12. Na bado mnawaamini.
We umesahau Lissu alipoibua issue ya Hati ya Muungano kwenye Bunge la Katiba hadi watu wakaenda kuitengeneza?Msajili wa vyama nchini ukimuomba hati ya CCM kusajiliwa kama chama mojawapo Cha siasa nchini katika mfumo wa vyama vingi,hatia hiyo Hana, na hajiulizi kwann yupo ofisini!
CCM kwa hakika wana allergy na kuongea ukweli.Tunajenga SGR Kwa fedha ZETU za ndani.... Tunajenga bwawa la Nyerere Kwa fedha ZETU za ndani, tumenunua ndege Kwa fedha ZETU za ndani,...n.k
Kumbe anang'ata na kupuliza?Wewe Mayor Quimby una sifa za kusifia unachokiponda, nakumbuka kuna nyuzi ulimsema sana Saa100 ukakaa siku 3 nyingi ukaja na nyuzi nyingine ya kumsifia saa100 najiuliza hivi huyu kichwa chake kina matatizo gaani? Lord denning ukimsoma nyuzi zake za kitambo humu ni kuisifia CCM mwanzo mwisho sasa hivi kajivika mabomu anailipua CCM, sasa atakapobadirisha upepo lazima niruke nae maana mnazengua
Hapana. Sehemu nilipowahi kuwatetea niliwatetea kwa hoja. Sehemu nilipowakosoa nimewakosoa kwa hoja.Kumbe anang'ata na kupuliza?
Soma hapa utaelewa👇Kumbe anang'ata na kupuliza?
Afu Mayalla alikuwa muandishi mzuri sana. Sijui kazeeka? Coz kwa mwafrika ukizeeka unakuwa mjingaWenda hili ni andiko bora kabisa jf kwa mwaka 2025, mkuu umenyooka kama rula, hii ndo jf sasa ,
Mayalla aje ajifunze kitu cha msingi
Huyu mtoa mada kuna mada moja nilikuwa najibishana naye alikiri kuwa ni mwana CCM ila ni mfuasi wa No reforms no elections .
Kumbe una kumbukumbu ndio maana nikasema wewe na Mayor Quimby ni watoto wa Baba mmoja kabisa mnavyofanya havina tofauti
Wewe Mayor Quimby una sifa za kusifia unachokiponda, nakumbuka kuna nyuzi ulimsema sana Saa100 ukakaa siku 3 nyingi ukaja na nyuzi nyingine ya kumsifia saa100 najiuliza hivi huyu kichwa chake kina matatizo gaani? Lord denning ukimsoma nyuzi zake za kitambo humu ni kuisifia CCM mwanzo mwisho sasa hivi kajivika mabomu anailipua CCM, sasa atakapobadirisha upepo lazima niruke nae maana mnazengua
Ungeanza kupambana ndani ya chama au ungehama chama. Lissu ambaye ni mtu unayekubali sera zake ameanza mapambano ndani ya chama.Niliacha kumuunga mkono magufuli na kujitenga na CCM baada ya jaribio na kumuua Tundu Lissu
Amani iwe nanyi wanabodi. Mwaka huu naenda kutimiza miaka 10 ya membership kwenye jukwaa hili kwa Id hii. Hata hivyo, kwa ujumla nina miaka mingine 4 nyuma ya 2015 ya membership nikiwa na id nyingine ambayo kwa sasa siitumii. Mimi ni mwanachama wa CHAMA CHA MAPINDUZI ninayependa Demokrasia...www.jamiiforums.com
Umeridhika na maelezo? Au ndo ushafanya ligi ya mabishano?Ungeanza kupambana ndani ya chama au ungehama chama. Lissu ambaye ni mtu unayekubali sera zake ameanza mapambano ndani ya chama.
Uliacha au umeacha? Mboni km huelewekiHapana. Sehemu nilipowahi kuwatetea niliwatetea kwa hoja. Sehemu nilipowakosoa nimewakosoa kwa hoja.
Upo uzi kabisa niliwahi andika humu kuhusu Kwa nini niliacha kuwaunga mkono CCM.
Tafsiri yako tu ila ujumbe unaeleweka.Uliacha au umeacha? Mboni km hueleweki
Duuh kama yanaingia vile!Ni vile tu Watanzania wengi ni wajinga na sio wasomaji sana wa vitabu na wafuatiliaji wa masuala ya nchi yao.
Mlioshtuka leo kuhusu habari ya Tanzania kununua umeme nje kwa ajili ya matumizi ya mikoa ya Kaskazini wakati Serikali imekuwa ikijisifu kuzalisha umeme kuzidi matumizi yetu nawashangaa sana.
Kwa wale msiofahamu hakuna Chama cha siasa Afrika hii na nadhani duniani kinachoishi kwa uongo kama CCM. Na uongo wa CCM haujaanza leo, ulianza tangu ikiwa TANU na uliasisiwa na aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Tanganyika na Tanzania , Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Vitabu vya dini vinasema Shetani ni Baba wa Uongo ila kwa hapa Tanzania, baba wa uongo ni CCM.
Yafuatayo ni maeneo ambayo TANU na CCM waliwadanganya/Wamewadanganya Watanzania na wao wakaamini.
1. Suala la Oscar Kambona kutangazwa kuwa mhaini na ameolewa Uingereza. Jambo hili lilitangazwa na Serikali ya Nyerere mwaka 1967 baada ya Kambona kuamua kujiuzuru nafasi zote za Uongozi ndani ya Serikali na Chama baada ya kupingana na Nyerere kuhusu sera za Ujamaa. Watanzania kama mazuzu tuliamini huu uongo wa Nyerere na hadi tukatungishwa nyimbo mashuleni kuwa kambona Kaolewa Uingereza. Huu ulikuwa uongo wa Nyerere ili kuwarubuni Watanzania na kuwa label vibaya wanaompinga.
2. Suala la Nyerere kung'atuka kutangazwa ni kwa sababu eti ni Kiongozi mzuri na hataki kung'ang'ania madaraka. Mwaka 1985 CCM walitangaza na kueneza uongo unaoaminika hadi leo kuwa Nyerere aling'atuka kwa sababu hakuwa na tamaa ya madaraka wakati kiukweli kilichomkimbiza Nyerere ikulu ni mfululizo wa majaribio ya mapinduzi dhidi yake hasa ya mwaka 1981/1982 na lile la kutekwa kwa ndege ya ATCL kutokana na kushinikiza aondoke madarakani kwa sababu ya hali mbaya ya kimaisha/ kiuchumi iliyotokana na kufeli kwa sera zake za ujamaa.
3. Suala la kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 kuwa ni busara za Nyerere wakati ukweli ni kwamba baada ya kuanguka kwa Shirikisho la Kikokumunisti (USSR) nchi zote zilizokuwa zinaitegemea Urusi ziliamua kuchukua sera zinazofanana na za kimagharibi ili kuendelea kupata misaada kutoka Mataifa ya Magharibi.
4. Suala la Nyerere kuwa alikuwa kiongozi bora na hakuwa dikteta wakati kiuhalisia hakuna Kiongozi aliyekuwa dikteta nchi hii kama Mwalimu Nyerere. Kipindi cha Uongozi wake ndipo Watanzania wengi waliotofautiana nae kimawazo kama kina Bibi Titi Mohamed na Oscar Kambona walifunguliwa kesi za Uhaini na wengine wengi kuwekwa vizuizini chini ya Sheria ya kuweka watu kizuizini. Waliopona wachache walikimbia nje ya nchi na kurudi baada ya Nyerere kuondoka madarakani.
5. Suala la vita vya Uganda kuwa ilitokana na Iddi Amini kutaka kuuchukua mkoa wa Kagera wakati ukweli ni kwamba ugomvi wa Iddi Amini na Nyerere ulitokana na Nyerere kumpa hifadhi Obote aliyepinduliwa na Iddi Amini. Amini aliamini vikundi vinavyompinga ambavyo vingi vilikuwa vinashambulia Uganda kutokea Mkoa wa Kagera nchini Tanzania vinakuwa supported na Nyerere hivyo kuanza kuleta chokochoko mpakani na kuivamia Tanzania.
6. Suala la Corona kutokuwepo Tanzania kipindi cha awamu ya 5 (mwaka 2020/21) wakati kipindi hicho maelfu kama sio mamia ya watanzania walikuwa wanakufa kwenye hospitali zetu kwa ugonjwa wa Corona.
Kutokana na mifano hii michache, napenda kuwaambia Watanzania, CCM hawajawahi kuongoza hii nchi kwa ukweli. Kama wanashangaa leo kuambiwa tutanunua umeme Ethiopia wakati waliambiwa tunazalisha umeme unaozidi matumizi yetu basi watakuwa hawaijui CCM vizuri.
Ukweli uliopo kwenye suala la umeme ni kwamba matumizi yetu yanazidi kuongezeka kila kukicha hivyo hata huo Umeme wa Bwawa la Nyerere hautoshi. Pia pamoja na kuanza kazi kwa Bwawa la Nyerere, mabwawa mengine yanazidi kupunguza uzalishaji kila siku kutokana na kujaa matope na mabadiliko ya tabia nchi yaliyopunguza uwezo wa mabwawa hayo kuzalisha umeme kwa kiwango kinachopaswa. Ila ukweli huu kamwe Watanzania hamtaambiwa mtaletewa uongo wa kila na post za watu mbalimbali kutengeneza hoja uchwara kuutetea huo Uongo (Spinning)
Ikitokea CCM ikaanguka kwenye taifa letu jambo la kwanza watakalotakiwa kulifanya Viongozi wapya wa Tanzania ni kufanya maombi ya toba kwa Taifa kutokana na nchi hii kuendeshwa kwa uongo kwa miongo mingi sana.
Lord denning.
Huu ndo ukweli na uhalisia. CCM ni baba wa uongo hapa Africa na watanzania tulivyo mazuzu hatupendi kuhoji ndo wanatupeleka kweli.Duuh kama yanaingia vile!
Kwa hiyo no reform,no Elections ni sahihi?!!Hata siku moja usije kuamini data au takwimu zozote zile zinazotolewa na Serikali ya Tanzania iliyo chini ya CCM.
Amini maneno yangu. HATA SIKU MOJA USIZIAMINI, maana almost 99.9% ni za kupika, kutengenezea kwa nia na maslahi wanayojua wao.
Ni zaidi ya Sahihi. Haya mambo yote hayawezi kutokea kwenye nchi yenye mifumo imara ya checks and balance.Kwa hiyo no reform,no Elections ni sahihi?!!