Kama mlikuwa hamjui: CCM imeliongoza hili Taifa kwa uongo tangu ikiwa TANU hadi sasa.

Mkuuuu umechelewa mpaka tumeshibishwa matango pori ya kutosha? Sas mkuu vijana wa kileo tuanzie wapi? Maana Hoja zako ni rafiki kwa mustakabali wa vizazi vijavyo! Nimeshiba Sana kwa sauti yako ya maandishi
 
Tulia soma uelewe ndo utoe maoni yako. Mada inasema kuhusu CCM kuongoza hili Taifa kwa kutumia uongo. Na hili limeanzia tangu kipindi cha TANU.
Nini kinachokufanya unione kuwa sielewi ninacho kisoama hadi unihimize?
Mada ni mbovu kwa kujumuisha kijumlajumla kama ulivyo fanya.

Inawezekana hujui maana ya "kusema uongo"; lakini unajisikia kuwa mtaalam wa kutufundisha hayo unayo dhani wewe tuyaone yote kuwa ni uongo!
 
Sasa kama mada ni mbovu kwa nini umepoteza muda wako kuja kusoma na ku comment kwenye mada mbovu? Au ndo sindano imegusa mfupa?
 
Tena kuna wakati wakatoa taarifa kuwa watu wanaiba miundombinu kumbe ukweli ni kwamba kulikuwa na shida ya umeme kwenye njia zao kulikotokana na kutoweka umeme wa kutosha kwenye njia na ku u balance vizuri kwenye njia zao.
Noma sana!
 
Tulia soma uelewe ndo utoe maoni yako. Mada inasema kuhusu CCM kuongoza hili Taifa kwa kutumia uongo. Na hili limeanzia tangu kipindi cha TANU.
Mada ni mbovu, usitake kulazimisha kitu kibovu kiwe bora.
Nani ataamini kuwa CCM ya viongozi laghai kama hawa waliopo sasa ni ile ile ya wakati ilipo anzishwa; au hata TANU iliyo ongoza juhudi za kupata uhuru!
Unapo andika kwa mihemkohemko bila ya kuweka tafakuri kwenye hoja unazo andika, wasomaji wataona kuwa huna umakini wowote.
Na udhaifu huu unajionyesha wazi katika maandishi yako toka enzi zile ulipokuwa umekomalia mfumo wa ubepari.
Inaonyesha akili yako ni "one track", inaposhikilia jambo; basi haina muda wa 'moderation' kwenye jambo hilo.
 
Au ndo sindano imegusa mfupa?
Unaelewa maana ya "sindano kugusa mfupa", lakini?

Sindano ikigusa mfupa kuna athari zipi unazozijuwa wewe?
Ni mwendelezo wa yaleyale niliyo kueleza toka mwanzo, enzi zile ukiimba nyimbo za "ubepari" humu JF.
Unayo tabia ya ku'exagerate' kwa kila jambo unalo lisemea. Sasa unajigaragaza kabisa juu ya "uongo" wakati wa TANU!
 
Hoja upingwa kwa hoja. Ni vizuri kuonesha lipi lililosemwa hapo ni uongo?

CCM ilizaliwa mwaka 1977, na before kikikuwepo TANU. Sasa ni vizuri ukasema huo uongo hapo ulikuwa unaenezwa na kina nani ambao hawakuwa TANU!

Punguza obsession kijana!
 
Punguza obsession kijana!
Naona hujifunzi kitu. Ninakueleza lakini huwezi kuelewa. Kila unacho andika humu unatunga tu kichwani mwako, kama ulivyo tunga huo mstari hapo juu. Huo u-"kijana" umeutoa wapi?
Hiyo 'obsession' ni ya jambo gani? Ninapo sema wewe unayo 'obsession' ya ku-'exagerate' kwenye kila jambo unalolijengea hoja, bado huoni ukweli huo?
 
Jifunze kujibu hoja kwa hoja. Unachokifanya hapa ni kupiga mdomo tu bila facts.

Great thinker anapinga hoja kwa kutoa hoja. Wengine wanafanya kama unavyofanya wewe! Maneno matupu!
 
Hoja
Jifunze kujibu hoja kwa hoja. Unachokifanya hapa ni kupiga mdomo tu bila facts.

Great thinker anapinga hoja kwa kutoa hoja. Wengine wanafanya kama unavyofanya wewe! Maneno matupu!
Hoja zipi?
Hivi kwa nini hutaki kuelewa?
Hivi unajichukulia hapa wewe kuwa "Great Thinker" kwa kuleta mada za aina hii humu?
 
Endelea kupiga mdomo ndugu.
'Factually', "sipigi mdomo", natumia vidole!
Naona kupindisha mambo ni tabia yako ya kudumu; kama hivyo unavyo dai humu kuwa CCM ya Samia, yenye ulaghai mwingi ni CCM ileile ya Mwalimu Nyerere na TANU ya enzi zile!
 
Toa hoja zako ninapindisha kivipi? Toa hoja zako mambo niliyosema humu ni ya uongo au yamepindishwa kwa namna gani?
 
Toa hoja zako ninapindisha kivipi? Toa hoja zako mambo niliyosema humu ni ya uongo au yamepindishwa kwa namna gani?
Unapotoa maelezo kijumla jumla kama ulivyo fanya kwenye mada yako hii; ukaifananisha CCM ya ulaghai iliyopo sasa na CCM ya miaka ya 80, au TANU; halafu unajihisi umetoa hoja zinazotakiwa kujibiwa? Seriously, unaona hoja hapo ya kujibiwa?
 
Kofia na t-shirt zinatuponza!Ndio maana mdau mmoja humu alianzisha mada Moja,ili sm iondoke,watu waliozaliwa miaka ya 1960_1977,Wanatakiwa waondoke ili kizazi kipya kitawale,ila alituonea sio wote wenye mawazo ya kiesm!
Mwashambwa tatlaan sozani kama ni WA miaka ya sabini huko Hawa ni uchawa TU unawasumbua
 
Unapotoa maelezo kijumla jumla kama ulivyo fanya kwenye mada yako hii; ukaifananisha CCM ya ulaghai iliyopo sasa na CCM ya miaka ya 80, au TANU; halafu unajihisi umetoa hoja zinazotakiwa kujibiwa? Seriously, unaona hoja hapo ya kujibiwa?
Kwa hiyo hizi ndo hoja zako?

Kakojoe tu ukalale! Huu uzi umekuzidi sana uwezo!
 
Mpaka vitukuu vyako hilo halitatokea, kwa mbadala upi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…