Kama Mungu angekupa nafasi ya kuamua uishi miaka uipendayo je ungechagua mingapi? (Sharti muda lazima)

Kama Mungu angekupa nafasi ya kuamua uishi miaka uipendayo je ungechagua mingapi? (Sharti muda lazima)

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
Toa sababu pia kwanini umechagua miaka hiyo.

Mimi 1000 sababu ningependa kuona tabia ya nchi inavyobadilikabadilika.
 
Moderator heading isomeke kufa lazima na sio muda lazima.
 
Miaka 150 ,napenda sana safari na pia napenda niwe nakaa na watu wadogo wa umri wangu niwapange hata ambayo hayajawahi kuwepo kikubwa ni socialize nao
 
Aaaa pale mwili na akili tu vitakapochoka nitwaliwe..Sitaki kusumbua watu
 
hii suprise tunayo ishi nayo ndo nzuri inafanya unaishi kwa ukamilifu .....mapenzi ya mungu yakitimia anichukue
 
Mkuu mbona michache
Mingi ukiwa na mikakati.

Mimi nataka niishi maisha ya ukamilifu, nimalize kilichonileta duniani halafu niondoke chap. Sitaki kukawia sana.

Sasa hivi nina 30, bado miaka 15 tu. Nikizidisha sana 50 inatosha kabisa nitakuwa nimekamilisha kila kitu.

Nikiona bado nahitaji muda wa kuwepo naweza kuongeza mkataba kidogo nirefushe angalau miaka mitano, ila sitaki kuvuka 60 kwa namna yoyote ile.

Uzuri mimi ndiye ninayeamua. I am in TOTAL CONTROL.

Hata ukija na mauchawi ya Congo au bunduki huwezi kuniondoa kabla ya wakati wangu. KAMWE.

Hata Mungu mwenyewe hawezi kuniondoa bila RIDHAA yangu kwa sababu HATA HIVYO mimi ndiye Mungu mwenyewe.

Cc: DR Mambo Jambo NAMBA MOJA AJAYE NCHINI Rabbon
 
Mbona tayari tumeshapewa nafasi hiyo ya kuchagua, na tumefanya uamuzi wetu kama wanadamu?

Wazazi wetu Adamu na Hawa walipochagua dhambi walichagua pia mauti.

Kwa mujibu wa Biblia, mimi na wewe tumejichagulia miaka 70 au 80 kama tuna nguvu.

Zaburi 90:10.

Maandiko hayadanganyi.
 
Mingi ukiwa na mikakati.

Mimi nataka niishi maisha ya ukamilifu, nimalize kilichonileta duniani halafu niondoke chap. Sitaki kukawia sana.

Sasa hivi nina 30, bado miaka 15 tu. Nikizidisha sana 50 inatosha kabisa nitakuwa nimekamilisha kila kitu...]
Points tupu👏
 
Back
Top Bottom