Kama Mungu hayupo, maisha yana maana gani? Na kama yupo, kwanini Dunia inateseka hivi?

Kama Mungu hayupo, maisha yana maana gani? Na kama yupo, kwanini Dunia inateseka hivi?

Friji la mtumba

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2024
Posts
277
Reaction score
434
Wapo wanaoamini kuwa Mungu yupo – Muumba wa kila kitu, mwenye uwezo wa kubadilisha chochote.

Lakini wapo pia wanaoamini hakuna Mungu, na maisha haya ni matokeo ya mabadiliko ya asili, bahati, na akili ya binadamu.

Swali linakuja:

Kama Mungu yupo kweli, kwa nini kuna mateso, vita, magonjwa, vifo vya watoto wasio na hatia?
Na kwa upande mwingine:

Kama hakuna Mungu, binadamu anajiongoza kwa misingi gani? Maadili yanatoka wapi? Haki ni nini bila Mungu?


---

Maswali kwa mjadala:

Unaamini Mungu yupo au hakuna? Kwa nini?

Kama huamini, maisha yako yanapata maana wapi?

Kama unaamini, unawezaje kuelezea uwepo wa maovu na mateso?

Je, dini ni njia ya watu kutuliza hofu yao ya kifo au ni kweli kuna nguvu ya juu isiyoonekana?
 
Nmezaliwa kwenye dini,
Mimi naamini Mungu yupo, ila kuna siku nilikaa nikajiuliza – kama kweli anatupenda, kwa nini wengine wanazaliwa kwenye vita, njaa, na mateso bila kosa?

Pia nimeshawahi kukutana na mtu ambaye ni Atheist lakini ana maadili kuliko mtu wa kanisani/msikitini. Hii inanifanya nijiulize sana, je kuwa wa Mungu ni kutamka tu au kuishi kwa mfano?
 
Ukiweza kung'amua lile andiko la siku 1 inaweza kugeuka miaka 1000 na miaka 1000 inaweza kuwa siku 1 utakua mtulivu.

Unaweza kulaani na kukata tamaa ukaja kushtuka kwenye usingizi wako ukakuta kumbe maisha uliyoishi hapa duniani ni ndoto ya sekunde 2 ndani ya usingizi wa siku moja.
Hajawahi kuota ndoto isiyokupendeza hadi ukaamka na jasho ukashukuru?😁
 
Nmezaliwa kwenye dini,
Mimi naamini Mungu yupo, ila kuna siku nilikaa nikajiuliza – kama kweli anatupenda, kwa nini wengine wanazaliwa kwenye vita, njaa, na mateso bila kosa?

Pia nimeshawahi kukutana na mtu ambaye ni Atheist lakini ana maadili kuliko mtu wa kanisani/msikitini. Hii inanifanya nijiulize sana, je kuwa wa Mungu ni kutamka tu au kuishi kwa mfano?
Mimi nililia kwanini nilizaliwa kwenye familia masikini lakini cha ajabu hata mimi nilipata watoto wakati napambana na maisha niliendekeza
migodi badala ya kujiimarisha

Kumbe matatizo mengi tunayo kabiliana naya husababishwa na binadamu
 
Ukiweza kung'amua lile andiko la siku 1 inaweza kugeuka miaka 1000 na miaka 1000 inaweza kuwa siku 1 utakua mtulivu.

Unaweza kulaani na kukata tamaa ukaja kushtuka kwenye usingizi wako ukakuta kumbe maisha uliyoishi hapa duniani ni ndoto ya sekunde 2 ndani ya usingizi wa siku moja.
Nadharia
 
Maisha ni shobo zako mwenyewe ,kiufupi maisha ni biashara ya upatu tena pyramid schemes au ponzi scheme ..Mtu anazaa ili wengine wanaendelea kuzaani huko chini kama wajinga bila hata kufirikia yule anayemzaa atakumbana na mitihani ila mwisho wa siku atakufa tu haina ubishi.

Kiufupi dunia kote hata kwa wanyama ni matatizo ,kuna jamii kama nyumbu kazi yao kuliwa ila bado wanazaa tena wako wengi zaidi hapa utajua hata binadamu ni wajinga ...Bado maisha ni magumu ila bado wanazaana kama wathenge.

Kiufupi Maisha yapo kwa sababu umeyapa maana ila maisha ni mateso na ujinga ,na aliyeleta huu mfumo wa maisha haya ya sasa ni Mthenge mkubwa kabisa ..
 
Back
Top Bottom