Unampaje mzazi mwenye uwezo ulio na kikomo, ujuzi ulio na kikomo na upendo ulio na kikomo wajibu mkubwa kuliko Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote?
Ukishaandika 1/2 = 10/x hapo x lazima iwe mara kumi ya mbili ili uwe na proportinality.
Sasa hesabu zako mbona zinaharibu proportionality, mwenye uwezo mdogo (mtu) unampa wajibu mkubwa na mwenye uwezo mkubwa (Mungu) unampa wajibu mdogo?
Unampaje lawama kubwa mzazi aliyefanya baya kwa sababu kajikuta kwenye dunia inayoruhusu mabaya kufanyika kuliko Mungu aliyeumba ulimwengu unaoruhusu mabaya kufanyika?
Kwani Mungu angeumba dunia mbayo mabaya hayawezekani kuwapo, watu wachague mazuri na mazuri tu, angepungukiwa nini? Kwa nini hakuumba hivyo?
Kwa nini unalazimisha mabaya yawepo ili huo uhuru uwepo? Uhuru unaoua, unaoharibu, unaotesa una maana gani?
Pia, Mungu alishindwa kuumba ulimwengu wenye uhuru wa maana bila ya mabaya kuwepo?
Kama alishindwa, kweli huyo ni Mungu muweza yote?
Kama hakushindwa, ila hakutaka tu, je, kweli huyo ni Mungu mwenye upendo wote? Mbona kaachoa mabaya yawepo yanatutesa sana? Mbona kuteseka huku kuna contradict habari ya kwamba Mungu ana upendo wote?
Kuhusu mzazi kupewa wajibu mkubwa kuliko Mungu mwenye uwezo wote. Hii ni kulinganisha visivyolinganishwa. Kwa sababu
Mzazi ana nafasi ya kushiriki na siyo kuamuru maisha ya mtoto.
Responsibility ya mzazi ni kushiriki katika malezi ya kimaadili na kimwili, lakini si kuamua maisha yote ya mtoto.
Mungu anatoa muongozo (kupitia dhamiri, dini, na maandiko), lakini binadamu wana uhuru wa kuchagua.
Kwa hiyo hoja ya kwamba mzazi anapewa jukumu kubwa kuliko Mungu haina msingi, kwa sababu mzazi hana uwezo wa ki-Mungu, na Mungu hana nafasi ya mzazi ya kibinadamu. Ni ngazi tofauti kabisa.
Unauliza kama Mungu angeumba dunia ambayo mabaya hayawezekani, angepungukiwa nini?
Hili swali lina mantiki , lakini lina presupposition inayodai
“Dunia nzuri ni dunia isiyo na mabaya.”
Kwa mtazamo wa falsafa ya dini (haswa kutoka kwa thinkers kama Alvin Plantinga), uhuru wa kimaadili (moral freedom) ni wa thamani kuu kuliko dunia ya roboti wanaotii tu bila hiari.
Ikiwa Mungu angeumba ulimwengu ambao hatuwezi kufanya mabaya, basi sisi tusingekuwa binadamu wa kweli bali maroboti wa kimaadili.
True love, true kindness, true courage haviwezi kuwapo pasipo uwepo wa uwezekano wa chuki, ubaya na woga.
Mungu hakutaka kuumba dunia perfect in programming bali perfect in potential.
Kwa hiyo, uhuru wenye uwezekano wa mabaya ni bora kuliko kutokuwepo kwa mabaya lakini pia kutokuwepo kwa upendo wa kweli.
Kwa Nini Uhuru wa Kuchagua Unaruhusu Mabaya?
Swali la msingi kabisa.
Uhuru unaoua, unaoharibu, unaotesa una maana gani?”
Kwa mtazamo wa kiroho, uhuru si tu uwezo wa kuchagua, bali uwezo wa kuonyesha upendo wa kweli kwa hiari.
Upendo wa lazima si upendo.
Ushujaa wa kweli ni ule unaochagua wema mbele ya uwezekano wa mabaya.
Hata Yesu aliteseka. Hata mitume waliteseka. Lakini mateso yao yalikuwa na maana,, si mateso yasiyo na sababu.
Hii inarejesha thamani ya suffering kama chombo cha mafunzo, ukomavu na hata ukombozi.
No cross, no crown.
Hakuna taji bila msalaba.
“
Kama alishindwa kuumba dunia bora, basi si muweza yote. Kama hakutaka, basi si mwenye upendo wote.”
Omnipotence haimaanishi kufanya yasiyo na mantiki. Mungu hawezi kuumba square circle, au mtu huru asiye na uhuru.
Kwa hiyo, kuumba dunia ya binadamu huru lakini wasioweza kuchagua mabaya, ni contradiction, si ukosefu wa uwezo.
Na kama Mungu aliona dunia ya uhuru yenye mateso ina thamani zaidi kuliko dunia isiyo na uhuru isiyo na mateso, basi ni kwa sababu sababu ya upendo na hekima, si ukatili.
Mbona Mungu Anaonekana Hayuko Wazi na Hayasaidii Wakati Mabaya Yanatokea?
Hapa umetoa hoja ya kihisia zaidi kuliko ya ki mantiki.
Mungu amejifunua kwa watu, kupitia dhamiri, kupitia historia ya wokovu, kupitia mitume, kupitia watu wema.
Siyo kwamba Mungu hayupo, ni kwamba huonekana kwa macho ya imani, si kwa macho ya kimwili tu.
Pia, mabaya mengi unayoyalaumu kwa Mungu ni matokeo ya matendo ya kibinadamu, si amri za ki-Mungu.
Hoja ya Mabaya Haibatilishi Uwepo wa Mungu, Inaonyesha Thamani ya Uhuru
The existence of evil is not evidence against God, but evidence of the value God places on human freedom.
A God who forces good removes the dignity of man.
A God who allows choice, even when it hurts, shows trust and the desire for authentic relationship.
Mungu hakutuumba tufanye mazuri kwa lazima, bali kwa hiari. Bila hiari, hakuna upendo wa kweli. Bila uwezekano wa mabaya, hakuna ushindi wa wema."
Na huo ndio ushahidi wa uwezo na upendo wa Mungu, kwamba aliweza kuumba binadamu wenye uhuru halisi, si maroboti, ili tuweze kumpenda kwa hiari, hata kama kuna hatari ya kupotoka.