Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 89,019
- 156,726
Wewe una distinction gani ya kukuhalalishia wewe kusema mimi sijui ninachojadili? Kipi kinakupa haki hiyo, hususan ikiwa umesema hata wewe hujui?Labda swali halikutakiwa liwe nani ana credentials hiyo itakua ni Ad hominem.
Kwani hapa tunajadili hoja au sifa za watoa hoja?
Kama huwezi kuelezea unachosema, kuelezea Mungu ni nani, yukoje, anapatikanaje, na yuko katika hali ipi yaani anaonekana? anasikika? anashikika? ananusika? anaonjeka? au hata kuthibitika kwa njia yoyote ya uhalisia basi unajichanganya unapodai unajua unachokijadili.
Unapodai kitu kipo au hakipo bila uwezo wa kukieleza kwa kina wala kukionyesha kwa njia yoyote halisi, kimsingi unapinga hewa yaani hakuna kilichotokea.
Hoja ya Mungu, kwa msingi kama huo imebaki kuwa wazo tu na kuendelea kulazimisha kuijadili bila hata kuelewa hali ya hicho unachokijadili je, hiyo siyo dalili wazi ya kutokujua unachokijadili?
Mimi nikisema sijui, shida iko wapi? Ni msimamo sahihi wenye uelekeo wa kutaka kufundishwa, kwanini niseme najua kitu wakati sikijui?
Kama wewe unajua na una credentials za kutosha basi fafanua ili wote tuelewe vinginevyo hoja yako inavunjika huku ikifunikwa na jazba.
Hiyo superiority unaitoa wapi?