Unajuaje hizo ishara zinathibitisha Mungu yupo na si kabobo tu?
Tukiangazia upande wa dhamira (conscience), si tu hisia ya ndani, bali ni uwezo wa kutofautisha jema na baya hata kabla ya kufundishwa.
Mfano: Mtoto mdogo anaweza kuhisi kuwa amekosea hata kabla hajafundishwa kwa kina kuhusu sheria. Why would a child, who has not been fully socialized, feel guilt or shame? That deep inner sense of right and wrong-suggests there is a moral law, and if there is a moral law, there must be a Moral Lawgiver.
Hii ndiyo hoja ambayo C.S. Lewis aliitumia katika kitabu chake Mere Christianity akisema
"If there was a controlling power outside the universe, it could not show itself to us as one of the facts inside the univers. But it could show itself inside ourselves as an influence or a command trying to get us to behave in a certain way."
Kwahiyo, dhamira inakuwa ni kama sauti ya sheria ya maadili ambayo haijatungwa na sisi,, na hilo linaashiria kuwepo kwa Muumba mwenye akili na maadili ya juu.
Mawazo na uwezo wa kutafakari mambo ya kiroho ni kiashiria cha nafsi – na nafsi si kitu cha kimwili
Labda unijibu hili swali mkuu
👇
If thoughts are just brain chemicals, why do we have the capacity to question our existence, morality, or purpose? Why would evolution produce beings who contemplate God?
Hii inatuonyesha kuwa kuna kitu zaidi ya mwili – kuna nafsi (soul/spirit) – na hilo ni kiashiria cha kuwa kuna Chanzo cha kiroho kilichotuumba.
Uumbaji unaoendana na akili unatuonyesha kuwa kuna Muumbaji mwenye akili kubwa
Mawazo yenye mpangilio, mantiki, na sayansi hutegemea dunia iliyo na kanuni za kueleweka. Kwa nini kuna "logic" au "laws of nature" ambazo akili yetu inaweza kuelewa?
Einstein aliwahi kusema:
"
The most incomprehensible thing about the universe is that it is comprehensible."
Kwahiyo uwezo wa akili ya binadamu kuelewa dunia ni ushahidi kwamba dunia iliumbwa na Akili kuu – na hiyo ni ishara kuwa Mungu yupo.
Kwa hiyo, kusema kwamba dhamira na mawazo si ushahidi wa kuwepo kwa Mungu ni kupuuza hoja ya ndani (inward evidence) ambayo hata sayansi haiwezi kuelezea kikamilifu. Hizo ishara ni vitu vinavyoonyesha:
Kuna sheria ya maadili.
Kuna Nafsi iliyo juu ya mwili.
Kuna Akili kuu iliyoasisi uumbaji unaoeleweka.
Na hii ni sababu ya msingi ya kuamini kuwa Mungu yupo – sio kwa imani potofu, bali kwa akili yenye kufikiri.