Kuna jamaa siku moja alinihadithia jambo moja ambalo alikutana nalo huko posta.
Anasema wakati ametulia pahala anapunga upepo alitokea kijana mmoja ambae alikua kwenye nguo chafu chafu na nywele nyingi kichwani ambazo zilionesha ni siku nyingi pia hazijapata maji, na mguuni alikua na kidonda kibichi na alikua amekifunga kwa mfuko wa nylon, yaani inshort kijana alikua anatia huruma kwa kumuangalia.
Jamaa aoanieleza, yule kijana akasogea moja kwa moja hadi karibu ya jamaa na kuanza kujieleza ya kwamba yeye hajala tangu jana na anahitaji apate hata mia tano ili akapate chakula.
Kufupisha story ni kwamba jamaa anasema walipiga story kiasi na yule jamaa na baada ya story hizo akagundua jamaa hakuwa mwehu na kichwani kwake pia si haba, kwa maana alikua yuko exposed na mambo mengi ya kilimwengu, ila kwakua alikua na haraka sana hakuendelea kukaa nae sana so alichofanya nikumushikisha ten then akaachana nae.
Baada ya kumaliza mishe zake anasema alirudi nyumbani ila alikaa siku tatu huku ile picha ikiwa inamrudia kichwani mwake na jambo kubwa ambalo lilikua likimjia mara kwa mara ni why mtu kama yule ambae Hana utofauti na vijana wengi ambao yeye anafahamiana nao linapokuja swala la kupanga maneno kwenda kwenye hoja aishi maisha ya namna ile, na hapa ndio akaona arudi tena sehemu ile.
Aliporudi alikaa pale hakukutana na yule jamaa ila anasema katika lile eneo huwa kuna wadada watatu ambao wanakujaga na makapu yao ya chakula na kuwauzia watu wa pale, jamaa alishikwa na hamu ya kuulizia kama labda yule kijana anafahamika pale, na baada ya kufanya hivyo ikabidi apewe story ya kwamba yule sio chizi na wala Hana shida kama ambavyo yeye alikua anadhani ila ni vile tu ameingia kwenye uraibu wa madawa wa kulevya.
Taarifa zinasema yule kijana alikua ni kijana ambae anatokea kwenye familia ya watu wa kati kiuchumi na alikua na ndugu zake kadhaa ambao wako na maisha yao mazuri tu ila shida ni kwamba yeye alikua ni mtukutu mbele za baba yake na hii ikafanya baba yake amuache ajiongoze mwenyewe baada ya kumpa njia zimpasazo kupita kijana kugoma kuzifuata njia hizo na kuamua kufuata njia zake mwenyewe basi akajikuta ameangukia kwenye ulimwengu huo mbaya.
Wanasema mara kadhaa ndugu zake waliamua kumkalisha chini na kumpa jema hili na lile ila aliwaitikia tu kwa maneno kwa vitendo ikawa sifuri, aliweza kudumu kwenye kuyaishi hayo maneno yenye wema mkuu wa namna ya kuishi kwa angalau mwezi ila baada ya hapo anakengeuka na kurudi kwenye njia zake na hapo ndipo walipoamua kuachana nae mazima.
Sasa hivi hawamzingatii kwenye kumpa njia za kupita ila akienda kulia shida ya chakula anapewa anakula na hata fedha huwa anapewa ila ndio hivyo hazijawahi kudumu mikononi mwake kwa maana zote akizipata zinaenda kuishia kwenye madawa ya kulevya na hili ndilo jambo ambalo limefanya hata nduguze waone iko haja ya kutokumpatia pesa bali apewe mahitaji ya muhimu kwa maana pesa itakuja imuue.
Mwisho wa story.