Kama Mungu hayupo, maisha yana maana gani? Na kama yupo, kwanini Dunia inateseka hivi?

Kama Mungu hayupo, maisha yana maana gani? Na kama yupo, kwanini Dunia inateseka hivi?

Hakuna Mungu.

Maisha hayahitaji Mungu ili yapate maana.

Maadili na misingi ya binadamu yanaundwa na binadamu mwenyewe.
Ndugu hua unapinga sana.. Ni kua uliwahi kua dini flan ukaasi au umezaliwa familia isiyo na dini maana ake unapinga sana kuskia habari za Mungu
 
Maisha ni shobo zako mwenyewe ,kiufupi maisha ni biashara ya upatu tena pyramid schemes au ponzi scheme ..Mtu anazaa ili wengine wanaendelea kuzaani huko chini kama wajinga bila hata kufirikia yule anayemzaa atakumbana na mitihani ila mwisho wa siku atakufa tu haina ubishi.

Kiufupi Maisha yapo kwa sababu umeyapa maana ila maisha ni mateso na ujinga ,na aliyeleta huu mfumo wa maisha haya ya sasa ni Mthenge mkubwa kabisa ..
Hahahahahahah nani sasa???
 
Kama Mungu ni wa haki kwa nini anaruhusu kuteseka kwa mwanadamu? Swali linalotafutiwa majinu mpaka mwisho wa dunia
Mateso wameyataka binadamu wenyewe ; kwanza wanazaliana kwa kuhalalisha mateso kwa wengine wanaozaliwa ,wameweka mifumo migumu kama kupata pesa ili iweje , binadamu ni wabinafsi hawana hurumu hata awe mzazi wako ... Mafanikio ya binadamu ni kuwa juu ya mwingine hapo lazima dunia iwe chungu.
 
Duniani Kuna falme mbili; Giza na Mwanga, kila falme Ina kazi yake, Wakati Mungu anaumba ulimwengu hakutaka kumlimit mwanadamu kwenye namna ya Kuishi, kufikiri, na kuchagua. Kila unachokiona Leo kwako au familia yako ni matokeo ya maamuzi ambayo ulichukua, au familia yako ilichukua. Hakuna wa kumlaumu, Ingawa Ipo ahadi ya kuwa mshindi endapo utakuwa royal kwenye ufalme wa Mwanga, wa Giza sijui.
 
Wapo wanaoamini kuwa Mungu yupo – Muumba wa kila kitu, mwenye uwezo wa kubadilisha chochote.

Lakini wapo pia wanaoamini hakuna Mungu, na maisha haya ni matokeo ya mabadiliko ya asili, bahati, na akili ya binadamu.

Swali linakuja:

Kama Mungu yupo kweli, kwa nini kuna mateso, vita, magonjwa, vifo vya watoto wasio na hatia?
Na kwa upande mwingine:

Kama hakuna Mungu, binadamu anajiongoza kwa misingi gani? Maadili yanatoka wapi? Haki ni nini bila Mungu?


---

Maswali kwa mjadala:

Unaamini Mungu yupo au hakuna? Kwa nini?

Kama huamini, maisha yako yanapata maana wapi?

Kama unaamini, unawezaje kuelezea uwepo wa maovu na mateso?

Je, dini ni njia ya watu kutuliza hofu yao ya kifo au ni kweli kuna nguvu ya juu isiyoonekana?
Kuna jamaa siku moja alinihadithia jambo moja ambalo alikutana nalo huko posta.

Anasema wakati ametulia pahala anapunga upepo alitokea kijana mmoja ambae alikua kwenye nguo chafu chafu na nywele nyingi kichwani ambazo zilionesha ni siku nyingi pia hazijapata maji, na mguuni alikua na kidonda kibichi na alikua amekifunga kwa mfuko wa nylon, yaani inshort kijana alikua anatia huruma kwa kumuangalia.

Jamaa aoanieleza, yule kijana akasogea moja kwa moja hadi karibu ya jamaa na kuanza kujieleza ya kwamba yeye hajala tangu jana na anahitaji apate hata mia tano ili akapate chakula.

Kufupisha story ni kwamba jamaa anasema walipiga story kiasi na yule jamaa na baada ya story hizo akagundua jamaa hakuwa mwehu na kichwani kwake pia si haba, kwa maana alikua yuko exposed na mambo mengi ya kilimwengu, ila kwakua alikua na haraka sana hakuendelea kukaa nae sana so alichofanya nikumushikisha ten then akaachana nae.

Baada ya kumaliza mishe zake anasema alirudi nyumbani ila alikaa siku tatu huku ile picha ikiwa inamrudia kichwani mwake na jambo kubwa ambalo lilikua likimjia mara kwa mara ni why mtu kama yule ambae Hana utofauti na vijana wengi ambao yeye anafahamiana nao linapokuja swala la kupanga maneno kwenda kwenye hoja aishi maisha ya namna ile, na hapa ndio akaona arudi tena sehemu ile.

Aliporudi alikaa pale hakukutana na yule jamaa ila anasema katika lile eneo huwa kuna wadada watatu ambao wanakujaga na makapu yao ya chakula na kuwauzia watu wa pale, jamaa alishikwa na hamu ya kuulizia kama labda yule kijana anafahamika pale, na baada ya kufanya hivyo ikabidi apewe story ya kwamba yule sio chizi na wala Hana shida kama ambavyo yeye alikua anadhani ila ni vile tu ameingia kwenye uraibu wa madawa wa kulevya.

Taarifa zinasema yule kijana alikua ni kijana ambae anatokea kwenye familia ya watu wa kati kiuchumi na alikua na ndugu zake kadhaa ambao wako na maisha yao mazuri tu ila shida ni kwamba yeye alikua ni mtukutu mbele za baba yake na hii ikafanya baba yake amuache ajiongoze mwenyewe baada ya kumpa njia zimpasazo kupita kijana kugoma kuzifuata njia hizo na kuamua kufuata njia zake mwenyewe basi akajikuta ameangukia kwenye ulimwengu huo mbaya.

Wanasema mara kadhaa ndugu zake waliamua kumkalisha chini na kumpa jema hili na lile ila aliwaitikia tu kwa maneno kwa vitendo ikawa sifuri, aliweza kudumu kwenye kuyaishi hayo maneno yenye wema mkuu wa namna ya kuishi kwa angalau mwezi ila baada ya hapo anakengeuka na kurudi kwenye njia zake na hapo ndipo walipoamua kuachana nae mazima.

Sasa hivi hawamzingatii kwenye kumpa njia za kupita ila akienda kulia shida ya chakula anapewa anakula na hata fedha huwa anapewa ila ndio hivyo hazijawahi kudumu mikononi mwake kwa maana zote akizipata zinaenda kuishia kwenye madawa ya kulevya na hili ndilo jambo ambalo limefanya hata nduguze waone iko haja ya kutokumpatia pesa bali apewe mahitaji ya muhimu kwa maana pesa itakuja imuue.

Mwisho wa story.
 
Unapoanza kijiuliza maswali ya aina hii, mwanzoni utaanza kujihisi mchanganyiko wa hofu, mfadhaiko, na kushtushwa pale unapoona umetumia sehemu kubwa ya maisha yako katika Imani ya Mungu.

Baadae taratibu utaanza kukaa sawa. Utaona Sheria ya kweli imejengwa katika misingi ya Humanity.

Nitamsaidia mwenye uhitaji, sitamuonea mtu, sitamlaghai mtu, etc. kwa sababu ninaongozwa na misingi ya Utu, na siyo kwa sababu naogopa nitachomwa moto na Mungu

Ukienda mbali utatunza mazingira hasa ya asili, kwa sababu Dunia ni nyumba ya wote
 
Ndugu hua unapinga sana.. Ni kua uliwahi kua dini flan ukaasi au umezaliwa familia isiyo na dini maana ake unapinga sana kuskia habari za Mungu
Mimi nimezaliwa kwenye familia ya kikristo katoliki. Nimepata ubatizo, Ekaristi na kipaimara.

Habari za Mungu ni habari za kurithishana na kuaminishwa tu na wazazi au walezi wako.

Lakini kiuhalisia hazina ukweli wowote ule zaidi ya imani za kusadikika tu.

It's only humans who speak on behalf of God.

Ni binadamu tu, wanahangaika kumuelezea huyo Mungu.

Mungu huyo hajawahi kuwepo na hayupo kujiongelea mwenyewe na kujidhihirisha mwenyewe.

Hakuna Mungu.
 
Mungu yupo, mambo magumu yanayotokea mengine ni kwa sababu ya kutotii neno lake, na mengine yanaruhusiwa na Yeye kwa makusudi maalumu.
Kwa nini huyo Mungu aliumba binadamu wasiotii neno lake?

Huyo Mungu, Alishindwaje kuumba binadamu watakao tii neno lake?

Kama huyo Mungu ana makusudi ya kufanya mambo magumu kutokea, Basi hajielewi na anaendeshwa kwa mihemko ya kihisia.
 
Back
Top Bottom