Kama Mungu hayupo, maisha yana maana gani? Na kama yupo, kwanini Dunia inateseka hivi?

Kama Mungu hayupo, maisha yana maana gani? Na kama yupo, kwanini Dunia inateseka hivi?

Nmezaliwa kwenye dini,
Mimi naamini Mungu yupo, ila kuna siku nilikaa nikajiuliza – kama kweli anatupenda, kwa nini wengine wanazaliwa kwenye vita, njaa, na mateso bila kosa?

Pia nimeshawahi kukutana na mtu ambaye ni Atheist lakini ana maadili kuliko mtu wa kanisani/msikitini. Hii inanifanya nijiulize sana, je kuwa wa Mungu ni kutamka tu au kuishi kwa mfano?
Upendo wa Mungu hauondoi uhuru wa binadamu. God gave humans free will, na kwa sababu hiyo, dunia imejaa matokeo ya chaguzi zetu, zikiwemo vita, uonevu, na ukosefu wa haki. Mungu yupo, anatupenda, lakini haingilii kila jambo kwa nguvu kwa sababu anatuheshimu pia. Suffering doesn't mean God's absence, sometimes it reveals how much we need Him.

Kuhusu mtu asiyeamini Mungu lakini ana maadili,, ni kweli kabisa. Morality is not exclusive to religion. Kuna watu wanachagua kuwa wema kwa sababu ya dhamiri, si imani ya kidini. Lakini kwa mtu wa Mungu, imani ya kweli haionekani kwa maneno tu, inaonekana kwa matendo.

Kama Yesu alivyosema, Mtawatambua kwa matunda yao (Mathayo 7:16), So yes, being godly is more about how you live than just what you say.

Kwa kifupi
Mungu yupo, upendo wake hauondoi maumivu yote, lakini umo nasi katikati ya hayo
 
Mtoto anaezaliwa na kansa au anazaliwa na matatizo, Ni upendo wa Mungu pia?
NDIYO, though it's hard to understand sometimes. Mungu haruhusu mambo kutokea bila sababu.

Mtoto kuzaliwa na kansa au matatizo si ushahidi wa chuki ya Mungu, bali ni sehemu ya ulimwengu uliopasuka (broken world) kutokana na dhambi.

Lakini upendo wa Mungu huonekana hata katikati ya mateso. God walks with us through pain, and often brings purpose, strength, and hope through even the most painful experiences.
 
Hakuna Mungu.

Maisha hayahitaji Mungu ili yapate maana.

Maadili na misingi ya binadamu yanaundwa na binadamu mwenyewe.
Hii ni humanistic worldview — inaamini kuwa binadamu anaweza kuishi maisha yenye maana bila imani ya Mungu.

swali la msingi si kama maisha yanaweza kuwa na maana bila Mungu, bali ni aina gani ya maana tunatafuta —ya muda mfupi au ya milele?
 
Wapo wanaoamini kuwa Mungu yupo – Muumba wa kila kitu, mwenye uwezo wa kubadilisha chochote.

Lakini wapo pia wanaoamini hakuna Mungu, na maisha haya ni matokeo ya mabadiliko ya asili, bahati, na akili ya binadamu.

Swali linakuja:

Kama Mungu yupo kweli, kwa nini kuna mateso, vita, magonjwa, vifo vya watoto wasio na hatia?
Na kwa upande mwingine:

Kama hakuna Mungu, binadamu anajiongoza kwa misingi gani? Maadili yanatoka wapi? Haki ni nini bila Mungu?


---

Maswali kwa mjadala:

Unaamini Mungu yupo au hakuna? Kwa nini?

Kama huamini, maisha yako yanapata maana wapi?

Kama unaamini, unawezaje kuelezea uwepo wa maovu na mateso?

Je, dini ni njia ya watu kutuliza hofu yao ya kifo au ni kweli kuna nguvu ya juu isiyoonekana?
Kuhusu existence ya MUNGU, hilo halina ubishi 100% yupo, the problem here ni jinsi dini zinapotray Mungu, apo kunaleta shida kidogo pia ukisoma kuhusu dini tafuti tafauti unaweza kuchanganyikiwa zaidi, kujibu swali kwanini watu wanateseka ni kwa sababu ndo utaratibu tuliojiwekea wenyewe binadam, mfano mfumo wa maisha, pesa ubaya na uzuri vyote viko defined na sheria kutokana sehem unapotoka ofwhich it makes sense

2) The main reason kwanini kuna maisha ni swali gumu sana ila cha muhimu ni kujifunza kuishi na maisha yenyewe yanavotaka
 
Harmony tu maisha yaendelee na kuondoa tabia za jungle! Wote sisi wanyama tu, ni lugha na utashi tu unatutofautisha na simba na fisi!
 
Suala la MUNGU kujidhihirisha kwenye maisha ya mtu ni kiwango chako cha imani. Maana pasipo imani ni vigumu kumpendeza MUNGU. Adamu alipewa amri na Mungu akaivunja akauza urithi kwa shetani mateso yakaanza. Ila Mungu kateuwa mwakilishi wake Yesu Kristo ukimwamini mateso yanakwisha.
 
Hii ni humanistic worldview — inaamini kuwa binadamu anaweza kuishi maisha yenye maana bila imani ya Mungu.

swali la msingi si kama maisha yanaweza kuwa na maana bila Mungu, bali ni aina gani ya maana tunatafuta —ya muda mfupi au ya milele?
Maisha ni ya muda mfupi tu.

Hakuna maisha ya milele.

Kifo ndio cha milele.
 
"Mfumo wa asili" hapa ndo mzizi wa maswali ya wengi
Mfumo wa asili huu tuna uhakika gani nje ya mafundisho ya dini zetu? Sijui umelielewa swali
Ngoja nikusaidie kuelewa kitu hapa mkuu.

Mfumo wa asili unaonekana kupitia nature, akili ya kawaida (common sense), na maadili ya kijamii (universal moral instincts). Hata bila dini, binadamu wengi hutambua kuwa kuna mambo yanafaa na mengine hayafai kama vile kuua bila sababu au kuiba.

Mfano mdogo tu, watu wa tamaduni tofauti duniani walikuwa na sheria za msingi za kuheshimu uhai na mali hata kabla ya dini zilizoandikwa.

Hii inaonyesha kuwa kuna conscious moral order ndani ya mwanadamu,, ambayo wengi huitafsiri kama mfumo wa asili.

Kwa hiyo, hata bila dini, tunaweza kuona mfumo wa asili kupitia:

Human conscience
Observation of nature
Universal moral patterns

Kwahiyo dini imekuja kuupa mfumo huo sura kamili na mwelekeo wa kiroho.
 
Wapo wanaoamini kuwa Mungu yupo – Muumba wa kila kitu, mwenye uwezo wa kubadilisha chochote.

Lakini wapo pia wanaoamini hakuna Mungu, na maisha haya ni matokeo ya mabadiliko ya asili, bahati, na akili ya binadamu.

Swali linakuja:

Kama Mungu yupo kweli, kwa nini kuna mateso, vita, magonjwa, vifo vya watoto wasio na hatia?
Na kwa upande mwingine:

Kama hakuna Mungu, binadamu anajiongoza kwa misingi gani? Maadili yanatoka wapi? Haki ni nini bila Mungu?


---

Maswali kwa mjadala:

Unaamini Mungu yupo au hakuna? Kwa nini?

Kama huamini, maisha yako yanapata maana wapi?

Kama unaamini, unawezaje kuelezea uwepo wa maovu na mateso?

Je, dini ni njia ya watu kutuliza hofu yao ya kifo au ni kweli kuna nguvu ya juu isiyoonekana?
Mungu hayupo.

Maisha yanapata maana kutokana na sisi wenyewe tunavyojiongoza.

Kwa mfano, kama dunia ina udhalimu mwingi na mtu anayatoa maisha yake kupambana na udhalimu huo, maisha yake yanapata maana sana kwa kazi yake ya kupingana na udhalimu.

Kama kupambana na ubaguzi wa rangi ni jambo lenye maana na kupunguza udhalimu, basi maisha ya mtu kama Nelson Mandela yatakuwa yana maana bila kutegemea uwepo wa Mungu.
 
Kama Mungu ni wa haki kwa nini anaruhusu kuteseka kwa mwanadamu? Swali linalotafutiwa majinu mpaka mwisho wa dunia
Injustice doesn't cancel God's justice. Mateso yapo kwa sababu ya uhuru wa mwanadamu (free will), dhambi, na pia kama sehemu ya majaribio ya kiimani.

God allows suffering not because He is unjust, but because through suffering, character is shaped, imani inaimarika, na watu hujifunza rehema, upendo, na uvumilivu.

"Maana mateso ya sasa si kitu kama tutakayofunuliwa baadaye." Warumi 8

Kwa hivyo, Mungu huruhusu mateso kwa sababu ana mpango mkuu unaopita uelewa wetu wa sasa, na kwa kila maumivu, kuna kusudi.
 
Mimi nimezaliwa kwenye familia ya kikristo katoliki. Nimepata ubatizo, Ekaristi na kipaimara.

Habari za Mungu ni habari za kurithishana na kuaminishwa tu na wazazi au walezi wako.

Lakini kiuhalisia hazina ukweli wowote ule zaidi ya imani za kusadikika tu.

It's only humans who speak on behalf of God.

Ni binadamu tu, wanahangaika kumuelezea huyo Mungu.

Mungu huyo hajawahi kuwepo na hayupo kujiongelea mwenyewe na kujidhihirisha mwenyewe.

Hakuna Mungu.
So unataka Mungu ajithibitishe kama nani? CRB? Au unadhani kwa sababu hujamwona basi hayupo,, wewe hujawahi kuiona akili yako, but here you are, defending it passionately!

Unasikitisha.
 
Kwa nini huyo Mungu aliumba binadamu wasiotii neno lake?

Huyo Mungu, Alishindwaje kuumba binadamu watakao tii neno lake?

Kama huyo Mungu ana makusudi ya kufanya mambo magumu kutokea, Basi hajielewi na anaendeshwa kwa mihemko ya kihisia.
Mungu hakuumba binadamu kama mashine zisizo na hiari. He gave humans free will, uwezo wa kuchagua mema au mabaya. Bila hiari, obedience ingekuwa meaningless.

Utii wa kweli hutoka kwa moyo unaochagua kumpenda Mungu, not by force.

Kama kila kitu kingekuwa rahisi au perfect, then there would be no space for growth, responsibility, or real relationship with God.

So, God allows difficulty and disobedience not because He is emotional or confused, but because through them, character, love, and true faith are revealed.
 
So unataka Mungu ajithibitishe kama nani?
Kwa nini unahangaika kumuelezea na kumtetea huyo Mungu?

Huyo Mungu anashindwa nini kujielezea na kujitetea mwenyewe?
CRB? Au unadhani kwa sababu hujamwona basi hayupo,, wewe hujawahi kuiona akili yako, but here you are, defending it passionately!
Thibitisha uwepo wa huyo Mungu na si imani na mawazo yako ya kufikirika uliyoaminishwa.
Unasikitisha.
 
Maisha ni ya muda mfupi tu.

Hakuna maisha ya milele.

Kifo ndio cha milele.
Yes, physical death comes lakini si mwisho wa maisha. According to scripture, "Na hii ndiyo ahadi aliyotuahidia, yaani, uzima wa milele" (1 Yohana 2:25).

Kwa hiyo, kifo si cha milele, ni kiingilio tu kuelekea maisha ya milele, either in the presence of God or away from Him. The real question is not if we live forever, but where.??
 
Kwa nini unahangaika kumuelezea na kumtetea huyo Mungu?

Huyo Mungu anashindwa nini kujielezea na kujitetea mwenyewe?

Thibitisha uwepo wa huyo Mungu na si imani na mawazo yako ya kufikirika uliyoaminishwa.
Kama mtu ameona mwanga wa jua, ataulizwa kwa nini anazungumzia jua? We speak not because God is weak, but because His greatness compels us to.
 
Injustice doesn't cancel God's justice. Mateso yapo kwa sababu ya uhuru wa mwanadamu (free will), dhambi, na pia kama sehemu ya majaribio ya kiimani.

God allows suffering not because He is unjust, but because through suffering, character is shaped, imani inaimarika, na watu hujifunza rehema, upendo, na uvumilivu.

"Maana mateso ya sasa si kitu kama tutakayofunuliwa baadaye." Warumi 8

Kwa hivyo, Mungu huruhusu mateso kwa sababu ana mpango mkuu unaopita uelewa wetu wa sasa, na kwa kila maumivu, kuna kusudi.
Ebu weka kwa maelezo ya backbencher mzeya...naona kama unataka kufungua pfc yangu...elaborate
 
Ebu weka kwa maelezo ya backbencher mzeya...naona kama unataka kufungua pfc yangu...elaborate
Maelezo yanajitosheleza sana hayo, soma kwa kuyatafakari mkuu, nadhani utanielewa na utaelewa ukuu wa Mungu.
 
Mungu hakuumba binadamu kama mashine zisizo na hiari. He gave humans free will, uwezo wa kuchagua mema au mabaya. Bila hiari, obedience ingekuwa meaningless.
Kama huyo Mungu alitupa freewill ya kuchagua mema au mabaya, Kwa nini hataki na hapendi tuchague kufanya mabaya?
Utii wa kweli hutoka kwa moyo unaochagua kumpenda Mungu, not by force.
Huyo Mungu akipendwa anafaidika nini?

Kama tuna freewill ya kumchukia, kwa nini huyo Mungu anataka tumtii na tumpende?
Kama kila kitu kingekuwa rahisi au perfect, then there would be no space for growth, responsibility, or real relationship with God.
Mungu muweza wa vyote, Alishindwaje kuumba dunia isiyo na uovu wala mabaya?
So, God allows difficulty and disobedience not because He is emotional or confused, but because through them, character, love, and true faith are revealed.
Kwani ili "love" iwe revealed ni mpaka watu wapitie difficulties?
 
Mungu hayupo.

Maisha yanapata maana kutokana na sisi wenyewe tunavyojiongoza.

Kwa mfano, kama dunia ina udhalimu mwingi na mtu anayatoa maisha yake kupambana na udhalimu huo, maisha yake yanapata maana sana kwa kazi yake ya kupingana na udhalimu.

Kama kupambana na ubaguzi wa rangi ni jambo lenye maana na kupunguza udhalimu, basi maisha ya mtu kama Nelson Mandela yatakuwa yana maana bila kutegemea uwepo wa Mungu.
Duuuh ili jibu limekaa kimkakati sana
 
Back
Top Bottom