Kama Mungu hayupo, maisha yana maana gani? Na kama yupo, kwanini Dunia inateseka hivi?

Sijasema anayeuliza kuhusu Mungu ana confirmation bias.

Nimesema ukiuliza jani limewekwa na nani kwa kulenga kutafuta jibu la Mungu ulilokuja nalo mwenyewe mfukoni una confirmation bias.

Yani swali hujui jibu lake lakini ushalenga jibu lielekee kwa Mungu. Hiyo ndiyo confirmation bias yenyewe.
 
Free will bila consequences ni kama mtihani usio na alama—hakuna maana yake. Na kusema Mungu ni "mwehu" ilhali unamjadili kwa hasira zote hizo ni kama kumchukia Joker kwa kuwa kwenye movie ambayo hukuitazama.

By the way, kusema “God doesn’t exist” kwa ujasiri wote huo ni proof ya namna alivyo deep kwenye akili zako hadi unahangaika kumbishia mtu usiyemwamini. Irony much?

Kama Rais yupo kwa sababu anaonekana, basi akili yako pia haipo,, maana hatuioni. 🤷‍♂️
 
Mpaka sasa hujathibitisha Mungu yupo.

Umekuja na logical fallacy ya personal experience tu na habari za faith ambazo si proof na unaruhusiwa kuamini hata uongo.
 
Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe kimeundwa kwa mechanism, Hata huyo Mungu lazima awe ameundwa kwa mechanism.

Haiwezekani Mungu huyo atokee tu from nowhere.

Haiwezekani Mungu huyo azuke tu, from nowhere.
Ndio maana Mungu sifa sio za binadamu vau kitu ...🤣🤣Vingine vyote zina muundo ,ili mzaane lazima mpakuane na manii yaingie kwa mwanamke ...Ila Mungu ndiye kaweka ...Yeye hana chanzo wala Mwisho .
 
Mkuu hoja yako ina point, lakini kuna mchanganyiko wa concepts hapa. Personal experience siyo kila wakati,, logical fallacy—ni fallacy tu pale inapojaribu kutumika kama uthibitisho mkuu wa ukweli wa jumla (hasty generalization au anecdotal fallacy).

Lakini personal experience inaweza kuwa sehemu ya ushahidi au ikatumika kama kiashiria cha pattern, hasa kama inalingana na data au matukio mengine. Huwezi kuitupa kabisa kama haina thamani.

Mfano:
"Nimeshudia mvua ikianza kunyesha saa kumi kila siku wiki hii" — hiyo ni experience.
"Na imekuwa hivyo kwa wiki 4 mfululizo" — hapo una pattern.
Ukisema, “Mvua huanza kunyesha saa kumi kila siku,” bila data nyingine, hiyo ndiyo fallacy.

Kwa hiyo, kusema “personal experience = logical fallacy” ni overgeneralization pia.
Experience inaweza kuchangia kwenye kuona pattern, lakini haitoshi peke yake.

Personal experience pamoja na pattern = hoja yenye nguvu.
Personal experience peke yake kama uthibitisho wa ukweli wa jumla = logical fallacy.

Sijui hatuelewani wapi mkuu??
 
Ndio maana Mungu sifa sio za binadamu vau kitu ...🤣🤣Vingine vyote zina muundo ,ili mzaane lazima mpakuane na manii yaingie kwa mwanamke ...Ila Mungu ndiye kaweka ...Yeye hana chanzo wala Mwisho .
Mungu kaweka ulimuona?

Au unatetea habari za kiimani na kidini tu?
 
Mpaka sasa hujathibitisha Mungu yupo.

Umekuja na logical fallacy ya personal experience tu na habari za faith ambazo si proof na unaruhusiwa kuamini hata uongo.
Just because you haven’t personally confirmed God's existence doesn’t mean He doesn’t exist. Hii ni logical fallacy ya argumentum ad ignorantiam — kushindwa kuthibitisha jambo si uthibitisho kwamba halipo.

Faith si personal experience tu,, pia ni recognition of realities beyond human perception. You cannot dismiss something as non-existent simply because it’s beyond your current proof or understanding.
 
1. Personal experience ni logical fallacy.
2. Jambo linaweza kuwa la personal experience halafu likawa na pattern zaidi ya personal experience.
3. Kama suala ni 2 hapo juu, kimantiki personal experience ni irrelevant (wa sababu ni logical fallacy kama tulivyoona kwenye 1 juu). Suala lililo relevant ni hiyo pattern ambayo imeshapita logical fallacy ya personal experience.

Yani ni hivi, kama nimeweza kuwasha taa kwa umeme, nina personal experience hiyo, halafu kuna patternnya ku validate hilo kwa watu wengi sana, hii personal experience yangu haitumiki kuthibitisha umeme unawasha taa, kwa sababu personal experience inaweza kuwa fluke tu.

Kinachotumika kuthibitisha umeme unawasha taa ni patternnya watu wengi na repeatable logically consistent experiments.

Sasa kwa nini unaweka hoja ya personal experience (a logical fallacy) kwenye suala lililokwisha vuka level ya personal experience na kuweka pattern kubwa zaidi?
 
Free will bila consequences ni kama mtihani usio na alama—hakuna maana yake. Na kusema Mungu ni "mwehu" ilhali unamjadili kwa hasira zote hizo ni kama kumchukia Joker kwa kuwa kwenye movie ambayo hukuitazama.
Na wewe kumtetea Mungu ambaye hata hujawahi kumuona na wala huwezi kuthibitisha uwepo wake ni sawa na kumtetea Abunuwasi wa kwenye vitabu.
By the way, kusema “God doesn’t exist” kwa ujasiri wote huo ni proof ya namna alivyo deep kwenye akili zako hadi unahangaika kumbishia mtu usiyemwamini. Irony much?
Sio proof bali ni kuonyesha kwamba huyo Mungu ni dhana ya kufikirika tu.

Huyo Mungu hana tofauti na Vibwengo, vampires, Mermaids, Dragons 🐉.

Vyote hivi ni fictions tu.

Fictional characters.

God is a fictional character.
Kama Rais yupo kwa sababu anaonekana, basi akili yako pia haipo,, maana hatuioni. 🤷‍♂️
Angalau kitu kinaweza kuwepo kwa namna mojawapo ya kuonekana, kusikika, kushikika, kuhisika na kupimika.

Akili ipo na inaweza kupimika.

Mungu hayupo kwa namna yoyote ile zaidi ya imani za kufikirika tu.
 
Sipingi uwepo wa Mungu kwa sababu sija confirm uwepo wake.

Napinga uwepo wa Mungu kwa sababu hata wanaosema Mungu yupo hawawezi kuthibitisha yupo na hoja zao zina internal contradictions zinazoonesha Mungu huyo hawezi kuwepo.

Hoja ya Mungu kuwepo ina internal contradictions.

Kwa mfano. The problem of evil/Epicurean paradox inaonesha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hawezi kuwepo.

Hujathibitisha Mungu yupo wala kuondoa hii paradox.
 
Personal experience inaweza kuwa logical fallacy kama inatumika kuthibitisha ukweli wa jumla bila data nyingine. Personal experience ni starting point au indication, lakini ili kuwa strong evidence inahitaji support ya pattern, data, au experiment repeatable.

Kwa mfano:

“Nimeshuhudia” ni personal experience tu (incomplete proof).

Lakini ukikusanya personal experiences nyingi zinazofanana na kuonyesha pattern, basi unapata ushahidi wenye nguvu zaidi.


So, personal experience si irrelevant, ni muhimu kama sehemu ya ushahidi lakini siyo standalone proof.
Kwa maneno mengine:
“Personal experience alone is weak proof, but combined with consistent pattern, it becomes relevant evidence.”

Hii ndiyo maana unapaswa kutambua tofauti kati ya personal experience kama indication na pattern kama uthibitisho.

Hivyo, personal experience si logical fallacy kwa sababu inachangia kwenye kuona pattern, lakini ni fallacy tu kama inatumika peke yake bila kuungwa mkono na data zaidi.

Huelewi wapi???
 
Uwepo wa uovu haupingani na uwepo wa Mungu, bali unaweza kueleweka kama sehemu ya uhuru wa mapenzi (free will) aliyowapa wanadamu. Mungu anaweza kuondoa uovu kwa nguvu, lakini kufanya hivyo kungeondoa uhuru wetu na kutufanya maroboti.

Hoja ya kwamba Mungu hawezi kuwepo kwa sababu ya contradictions ina assume kwamba tunamwelewa Mungu kikamilifu kwa akili zetu finyu. Lakini kama Mungu ni wa kipekee, mwenye sifa zisizo za kawaida, basi ni dhahiri kuwa some attributes may appear contradictory to our logic, but not necessarily in reality.

Kwa hiyo, kutothibitisha Mungu kwa njia za kisayansi si ushahidi wa kutokuwepo kwake — ni ushahidi wa mipaka ya njia hizo, si mipaka ya Mungu.
 
kujua kuna Mungu si lazima uwe na microscope, unahitaji kitu ambacho pengine wewe umekosa: introspection na humility.

"proof" unayoitaka, unataka aje afanye interview CNN ama? au aje apige selfie na wewe kwa Instagram? Mambo ya kiroho hayaendi kwa logic za TikTok mkuu.

Kwa kifupi, kuwa na akili haimaanishi kuitumia ku-discredit aliyekupa hiyo akili.

God is not fictional. But your argument... definitely sounds like satire.
 
Kama pattern inathibitisha mambo zaidi ya personal experience, kwa nini unataka kutumia personal experience ambayo inaweza kuwa logical fallacy sehemu ambayo ina pattern?
 
Kama pattern inathibitisha mambo zaidi ya personal experience, kwa nini unataka kutumia personal experience?
Facts can inform, but experience transforms. Kama pattern inaonyesha ukweli objectively, basi personal experience inaonyesha jinsi huo ukweli unavyoishi ndani ya mtu.

Ni kama kusema Sijasikia tu kuhusu Mungu, nimemwona akifanya kazi ndani yangu. Hii inasaidia kuonyesha kuwa Mungu si theory tu—He’s real, present, and active.
 
Kwa nini Mungu aweke mabaya wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayapo kabisa?

Freewill si jibu. Freewill ni uwezo wa kuchagua mazuri au mabaya.

Kwa nini kusiwe na freewill ya kuchagua mazuri na mazuri tu, bila mabaya kuwepo?

Kama unasema hatuwezi kumuelewa Mungu kwa akili zetu finyu, unajuaje kuwa Mungu yupo at all?

Unajuaje kuwa akili zetu finyu hizi hazijapigiwa hadithi tu ya Mungu kuwepo zikakubali, kwa sababu zina maswali mengi ambayo hazina majibu yake, na hazitaki kukubali kuwa hazina majibu, zinataka kuwa na jibu jepesi la Mungu tu?
 
Hiyo kumuona tu Mungu ndani yako utajuaje si ugonjwa wa akili tu umekupa delusions of grandeur?
 
Mungu hakuumba uovu, bali aliumba viumbe wenye freewill (uhuru wa kuchagua).,,freewill halisi lazima iwe na uwezekano wa kuchagua jema au baya—kama hakuna baya, hakuna maana ya uchaguzi. Kuamua mazuri kati ya mazuri si choice, ni preference tu. Without the contrast, virtue loses meaning.

Kutokuelewa kila kitu kuhusu Mungu si kwa sababu Mungu hayupo, bali kwa sababu capacity ya akili zetu ni finyu—kama mtoto mdogo hawezi kuelewa maamuzi ya mzazi. That limitation doesn't prove the parent doesn’t exist.

Na kuhusu hoja kuwa akili zetu "zinadanganywa" na hadithi ya Mungu—inawezekana. Lakini pia akili hizo hizo zinatambua uzuri, upendo, haki, na tumaini—ambavyo havina maelezo ya kutosha bila source ya juu. Sometimes, the longing for meaning itself is the fingerprint of something greater.

Uwepo wa mabaya hauondoi uwezekano wa Mungu, bali unaibua haja ya Mungu zaidi.
 
Hiyo kumuona tu Mungu ndani yako utajuaje si ugonjwa wa akili tu umekupa delusions of grandeur?
Kumuona Mungu ndani yako si lazima iwe pathological—inaweza kuwa deep spiritual awareness. Tofautisha kati ya delusions na mystical insight: moja huleta kiburi na kuchanganyikiwa, nyingine huzaa upendo, amani, na selflessness.

Si kila kitu kisichoeleweka na akili ya kawaida ni ugonjwa.
 
Kwa mujibu wako, Mungu hakuumba ulimwengu ambao uovu unaweza kutokea?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…