Kama ni kweli, basi comrade Kinana amepuuzwa!

Kama ni kweli, basi comrade Kinana amepuuzwa!

lini ashawahi kupokewa? weka picha za nyuma kama hizo, halafu kanuni zao zinasamaje? ibara gani?

ukijibu haya unakuwa umeondoa dhana ya umbea
Ndio maana Mungu alituumba na akili ili tuzitumie katika mambo madogomadogo ya kila siku. Hivi unategemea kumjulia hali mgonjwa ielekezwe kwenye KATIBA? Kumpokea mgeni atuelekeze Mungu? Au huwa huwaoni watu wamejipanga kumpookea Magufuli hata kama ametoka Dodoma tu? Au hilo limeandikwa kwenye KATIBA?
 
Alikuaga wakati anaondoka?

Alikuwa anakutaarifu yanayojiri huko alipokuwepo?

Katibu mkuu wa CHADEMA huwa anakuaga wakati akisafiri na huwa anakutaarifu anaporejea?

Kama Kinana alikuwa huko alikokuwa kama mtu binafsi na si kama katibu mkuu wa chama wewe inakuhusu nini kujua kama karejea au la?

Yaani mnatafuta kila aina ya vijisababu tu ili mumseme rais Magufuli.....


Btw, mpiga picha Woody hajatoa tu tweet ingine?
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
Tangu utudanganye ile guest house ya 'Nzagamba ya Migato' iliyoko Bariadi ni yako na umeijenga wewe wakati mwenyewe namjua ni marehemu nilikudharau sana.
 
Mbona sioni tatizo lolote....

Mmeumbuka kwenye ndege na huyo mpiga picha wenu sasa mmeibuka na non issue kuhusu mzee Kinana....

Bado nacheka kuhusu mpiga picha Woody....😀
Mbona hayahusiani hayo? Umekuwa kiranja wa kupangia watu hisia za kuleta JF toka lini?
 
Nyani Ngabu,
Lete hoja acha kutetea ubashite hapa!
Kinana ni KM wa CCM ni mtu mkubwa ndani ya chama, baada ya M/kiti Magufuli ni yeye! Haiwezekani Kinana aende na kurudi India kwa matibabu kimyakimya!
Ukweli lazima usemwe, kwamba ndani ya CCM kwa sasa kuna uasi na kumsusia Mwenyekiti hasa baada ya sakata la Bashite la kuvamia Clouds Media hadi kupelekea Nape Nnauye kuondolewa madarakani kwa kudhalilishwa!
Ikumbukwe kwamba Kinana na Nape ndo waliopigania kwa nguvu zote nchi nzima ili kuhakikisha Magufuli na CCM yake wanaingia Ikulu!
Kitendo cha Magufuli kumfuta kazi Nape huku akitishiwa kwa bastola na huku akiendelea kumlinda Paul Makonda kimewaudhi wana CCM wengi akiwemo KM Bwana Kinana! Hakuna siri na majibu yake ni 2020 ndipo mtajua kama huu ni umbeya au ukweli!

Hahaaaa nyie watu bana!

Kumbe mnawapenda CCM eeh?

Manake si kwa kujali huko...😀😀
 
We mtoa mada ungetoka hospital hujarecover completely ungetaka makamera kwako?. Msipende kudandiadandia mambo bhana. Au basi mtumeni Woody akapige picha kwa juu pale kwa comrade
mbona rais mstaafu JK aliporudi kutoka US kwenye matibabu aliongea na vyombo vya habari pale airport?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kwa hyo wanaolazwaga kule ujeruman kila baada ya miez mitatu akirud mnampokeaga?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Alikuaga wakati anaondoka?

Alikuwa anakutaarifu yanayojiri huko alipokuwepo?

Katibu mkuu wa CHADEMA huwa anakuaga wakati akisafiri na huwa anakutaarifu anaporejea?

Kama Kinana alikuwa huko alikokuwa kama mtu binafsi na si kama katibu mkuu wa chama wewe inakuhusu nini kujua kama karejea au la?

Yaani mnatafuta kila aina ya vijisababu tu ili mumseme rais Magufuli.....


Btw, mpiga picha Woody hajatoa tu tweet ingine?[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Alienda kibinafsi au alitumwa na rais kwenda kwenye matibabu? Au alitumwa arudi kabla hajapona kwamaana bajeti ilikwisha kwahiyo anaugulia nyumbani?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kama aliondoka bila kuagwa na viongozi wa chama chake na amerudi bila kupokelewa na kiongozi hata mmoja wa chama chake basi amepuuzwa ! Ndio nimeamini Duniani tenda wema uende zako! Kawatengenezea njia wamemwacha anajiuguza peke yake.

Jifunzeni kitu kwa CHADEMA, angalia Lema alivyo kuwa anafarijiwa alipo kuwa gerezani, angalia Mheshimiwa Mbatia alivyokuwa anafarijiwa wakati anaumwa! Mheshimiwa Heche kila Wakati ana wabunge na wanachama kibao pembeni ya kitanda chake wakimfariji.
Hata JK alipolazwa watanzania na wanaccm walionyesha kuguswa na walimfariji kwa uwazi, vipi mpambanaji wa chama hakuna ajuaye utadhani katibu wa tawi?
 
Jibu hoja ni kawaida kwa kiongozi wa ngazi ya juu kama KATIBU MKUU wa chama kurudi kimyakimya? Imeanza lini? Au nako ni kubana matumizi?
Kwwni alipoondoka kwenda huko alikokwenda kulikuwapo waandishi wa habari na shamra shamra airport? Aliondoka kimya kimya na atarudi kimya kimya. Tena inawezekana akwa alisharudi zamani. Maana huko India situliambitu atakaa siku 12 tu. Si kila kitu ni siasa. Yaani hata ugonjwa nao imekuwa siasa. Ugonjwa unahusu yeye na watu wake wa karibu.
 
Kuna Uzi uliorushwa kwamba alipotaka kuhutubia tu wanahabari alikamatwa na kutiwa vitasa vya kutosha coz ilionekana anataka kumuunga mkono nape
Dhambi ya uchaguzi inawatesa
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Habari wanajamvi!

Sijaamini maneno ya msemaji wa chama cha Mapinduzi labda nitaaminishwa baadae. Kwa maneno yake Katibu mwenezi anasema ni kweli mwanasiasa nguli na Katibu Mkuu wa chama cha mapinduzi comrade Alhajji Abdulrahman Kinana alikuwa anaumwa, na alipelekwa nje ya Nchi kwaajili ya matibabu,lakini kwa sasa amerudi yupo Nchini anapumzika nyumbani kwake! Hajafafanua kama ni Dar es salaam au Arusha. Nikajiuliza maswali yafuatayo;

- Hivi inawezekana kweli Katibu Mkuu wa chama arudi kutoka kwenye matibabu halafu asipokelewe na Mtu yeyote pale Airport? Hata ndugu zake hawakwenda kumlaki? Yaani asionekane na mwandishi wa habari hata mmoja?

- Tuseme yupo nyumbani kweli anaendelea kupumzika baada ya matibabu na huenda ana ED za miezi miwili au mitatu, lakini hakuna hata mtu mmoja alie kwenda kumpa pole? Yaani hata katibu mwenezi Naibu katibu mkuu hawajaenda kumpa pole!

- Yaani hata viongozi wote wanao julikana kwa uungwana wao wa asili kama Mbowe, Maalimu Seif, n.k Hawajaenda kumjulia hali? Nini kimetokea?

Ndio maana nikaishia kusema kama ni kweli kuwa Comrade Alhajji Abdulrahmani Kinana amerudi yuko nyumbani na hakuna mtu hasa wanao penda kuonekana kwenye vyombo vya habari, basi ni dhahiri ndugu yetu amedharauliwa na kupuuzwa.

Binafsi naomba wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kampeni pole kwa niaba yangu.
Mange kimambe anayomajibu,jamaa haumwi walichomfanyia ni kama alivyofanyiwa marehemu abdu jumbe baada ya sakata la nape
 
Back
Top Bottom