Mzee Kinana nikama vile psychologically hayuko vizuri. Kinana ni mtu aliyeamini kabisa kuwa kwa umri alionao na kwa kazi kubwa aliyoifanya na kuifanyia ccm huu ungekuwa muda mzuri kwake kupumzika.
Kupumzika ambako aliakutamani na kuona kazi aliyotumwa na kujituma ameikamilisha na ameweza kuandaa damu changa ambayo kwa mikono yake ameilea na kuipa uzoefu wakutosha. Hivyo ni muda sasa wakuiacha hiyo damu changa ifanye kazi na yeye na wengine waliowakongwe wawe washauri wa mipango na mikakati yakuendeleza chama.
Hata akafikia wakati kutaja kupumzika lakini ghafla akaambiwa hapana subiri kwanza. Hali hii imemstua sana. Pengine ndio chanzo cha kudhoofu kwa siha yake na 'kutumwa' kutibiwa huko alikotumwa.
Hii nikama hali ya mtu tajiri sana na aliyedumu katika maisha yake yote kuitengeneza familia yake kwa muda mrefu, akaiwekea misingi imara na madhubuti yakumudu maisha na maisha ya ushindani wakibiashara na miamalati ya maisha ya kawaida kwa hadhi ileile ya asili.
Lakini ghafla ikiwa umri umeenda sana, tajiri huyo akajikuta katika familia ile aliyoijenga na kuacha vijana wake wakiwa imara na akiwa na imani kuwa wataendeleza tunu za familia kwa pamoja na msikizano, anaiona familia inaanza kuparaganyika na kushikana mashati, pengine watoto wengine wanaambiwa hawahusiki na mali za mzee, tajiri yule anachanganyikiwa na pengine anaweza kuumwa ghafla na hata kupoteza maisha kwa hiyari au kwa kulazimishwa.
Watu waliopoteza umri wao mrefu katika kujenga jambo fulani nankuweka misingi bora ya aidha familia, kampuni, shirika, chama au hata nchi. Huwa wanapata huzuni sana pale wanapoona jitihada zao za miaka na miaka zinaweza kuharibiwa kwa sekunde tu na kuacha mvurugano usiokuwa na maana.
Hali hiyo pia ilimtokea baba wa taifa hili, mwalimu Nyerere pale alipoona misingi ya utawala bora na uchumi inaharibiwa na watu aliowaamini na kuwapeleka kwa jamii ili waaminiwe, wanaharibu nchi kwa sera za hovyo kama ubinafsishaji au utandawazi. Nyerere aliumizwa sana na kuona mashirika ya umma yakiuzwa kama njugu kwa bei za hovyo. Ilimuuma kwani alitumia umri wake wote kuyajenga mema hayo leo kufumba na kufumbua wanakuja watu wanaharibu machoni pake akiwa hai.
Mungu mbariki Mzee Kinana- zama zinabadilika.