Kama nyani alibadilika akawa binadamu ni kwanini nyani na sokwe wa sasa hawabadiliki tena kuwa binadamu?

Kama nyani alibadilika akawa binadamu ni kwanini nyani na sokwe wa sasa hawabadiliki tena kuwa binadamu?

jibu la swali lako hili hapa
 

Attachments

  • Screenshot_20241126-181704.png
    Screenshot_20241126-181704.png
    143.2 KB · Views: 3
  • Screenshot_20241126-181716.png
    Screenshot_20241126-181716.png
    161.1 KB · Views: 3
  • Screenshot_20241126-181724.png
    Screenshot_20241126-181724.png
    176.8 KB · Views: 2
  • Screenshot_20241126-181732.png
    Screenshot_20241126-181732.png
    151.6 KB · Views: 3
  • Screenshot_20241126-181742.png
    Screenshot_20241126-181742.png
    143.3 KB · Views: 3
  • Screenshot_20241126-181749.png
    Screenshot_20241126-181749.png
    150.3 KB · Views: 3
  • Screenshot_20241126-181749.png
    Screenshot_20241126-181749.png
    150.3 KB · Views: 3
  • Screenshot_20241126-181806.png
    Screenshot_20241126-181806.png
    148.4 KB · Views: 3
Wakati unajiuliza hilo sawali, ebu jiulize kwa nini leo mwanadamu haumbwi kwa udongo (refer creation theory).

All in all evolution and creation are just theories.
 
Ndugu zangu.

1: Tukiachana na maswala ya kidini, historia inatuambia binadamu wa kwanza alikua ni nyani / sokwe /chipanze,
binadamu hakua nyani ila alikua jamii ya nyani
sasa kama kweli binadamu tulikua ni manyani ni kwanini nyani / sokwe tunaowaona sasa hivi hawabadiliki kua binadamu na wala hawakatiki tena mikia na kua na mwili na utashi wa binadamu kama historia ilivyokua huko awali?
Evolution bado inaendelea na ipo enforced na mazingira vile vile inachukua muda mrefu sana kiasi kwamba hakuna kizazi kimoja kinaweza kuona mabadiliko kutoka hatua moja kwenda nyingine. Mfano kwa sasa hivi watu wanatumia muda mrefu sana kutumia smartphone sasa ile kukunja shingo wakati unatumia simu taratibu adaptation inaenda mpaka genes kwaiyo kuna uwezekano miaka milioni mbele binadamu akawa na shingo iliyojikunja nyuma hapo unaanzia mgongo.
 
Labda nikuulize,,,toka sokwe WA mwisho kubadilika na kuwa binadamu kuna mwengine ame undergone zile changes hata kukaribia stage ya homo habilis au hio process imepouse???
Process haijapause, process inabadilika jinsi dunia inavyobadilika. Hakuna mabadiliko yeyote makubwa yaliyotokea duniani kwa kipindi kirefu.
Pia, siyo sokwe hawa wa sasa hivi ndiyo walioevolve kuwa binadamu.
Kwani mbwa pitbulls walikuwepo msituni?
Je nyani wanaokula ndizi walikuwepo zamani?
Wamejuaje kufungua ndizi?
 
Samahani Kidogo Mkuu..
Hebu nipe Tofauti ya Mutation na Evolution..
Maana Katika maongezi yako ya Chini Paragraph ya Tano kutokea Chini Umeelzea Mutation badala ya Evolutiion
Mutation ni sehemu ya evolution. Ni agent ya evolution.

Random mutations huwa zinatokea kila kizazi.

Sasa, ikitokea random mutation fulani inatokea na kuipa species fulani feature fulani inayoipa specie advantage fulani, hiyo feature itaendelea kuwa dominant, dominance hiyo itapelekea vizazi vijavyo visivyo na hiyo mutation/feature kuwa vichache na hata kutoweka, na vilivyo na hiyo mutation/feature kuwa vingi, hatimaye hiyo mutation/feature inakuja ku dominate, na ikiwa na traits fulani tofauti kubwa, hapo ndipo species ina evolve.

Tukirudi kwenye mfano wetu wa bacteria na resistance. Kwa mfano bacteria wengi wakiwa wanauawa na dawa A, inayoshambulia plasma membrane zao za kawaida, wakatokea bacteria wengine wana mutation fulani kwenye DNA inayofanya plasma membrane zao kuwa ni nene zaidi, dawa haiwaiingii, hawa wachache hawatakufa kwa dawa, wataendelea kuzaana na kutawala kizazi kijacho, kizazi kinachofuata kitakuwa na hawa wenye mutation ya membrane nene wengi, hivyo, mutation hii itafanya wanaobakia kwenye species hii ya bacteria kuendelea kuwa ni wale wenye plasma membrane nene.

Hapo mutation ya wachache kuwa na plasma membrane nene imewapa advantage iliyofanya specie nzima i evolve kuwa ya wenye plasma membrane nene.

Mutation ni agent kubwa inayosababisha evolution.
 
Nyani na sokwe walibadilika na kuwa Binadamu kwa Muda Usiopungua Miaka Milioni ..
kwa sasa hawawezi Kwa sababu hakuna Nyani anayeishi Miaka zaidi ya Milioni kwa Sasa
1: Unajuaje kama hawafiki miaka milion kutokana na mabadiliko ya kalenda kurudisha miaka nyuma?

2: Kwa hiyo sisi binadamu ni manyani waliobadilika miaka mingi iliopita zamani ?
Wakati unajiuliza hilo sawali, ebu jiulize kwa nini leo mwanadamu haumbwi kwa udongo (refer creation theory).

All in all evolution and creation are just theories.
wewe una uhakika gani kama binadamu aliumbwa kwa udongo ?
 
Ndugu zangu.

1: Tukiachana na maswala ya kidini, historia inatuambia binadamu wa kwanza alikua ni nyani / sokwe /chipanze, sasa kama kweli binadamu tulikua ni manyani ni kwanini nyani / sokwe tunaowaona sasa hivi hawabadiliki kua binadamu na wala hawakatiki tena mikia na kua na mwili na utashi wa binadamu kama historia ilivyokua huko awali?

2: Je, kama kweli tulikua nyani na tukabadilika kua binadamu ni kwanini sahivi haiwezekani tena binadamu kubadikika na kurudia kua nyani kama wanasayansi wanavyodai?
Unaambiwa itachukua miaka mamilioni wao kubadilika wakati hawamalizi hata miaka 50
 
Labda nikuulize,,,toka sokwe WA mwisho kubadilika na kuwa binadamu kuna mwengine ame undergone zile changes hata kukaribia stage ya homo habilis au hio process imepouse???
Kutaka sokwe abadilike kuwa binadamu ni sawa na kutaka pundamilia abadilike kuwa farasi. Au ng'ombe abadilike kuwa nyati. Au Chui kuwa Simba.
 
Jiulize kwanza wewe unafahamu generations ngapi kwenda nyuma na kupata differences kubwa unahitaji generations ngapi... (in that token ni kama wewe na mababu zako wenye uwezo wa kuishi kwa dakika mtake kushuhudia mambo yanayotumia miaka miaka moja)

Kuweza kuelewa evolution inabidi ufanye utafiti kwa kupitia kitu kinachobadilika kwa muda mfupi sana kulinganisha na wewe unayefanya utafiti (mfano dakika au sekunde)...

Vilevile ukisema urudi nyuma uplan kila kilichotokea kitokee tena huenda kisitokee kama kilivyotokea (kuna a lot of happenstances)
 
Kwanza kabisa hatukuwaacha nyani ambao hawakubadilika.

Watu wengi wanafanya makosa ya kufikiri kuwa evolution inasema zamani tulikuwa sawa na hawa nyani wa sasa, sisi tumebadilika wao hawajabadilika.

Hivyo si evolution inavyosema. Wote tumebadilika. Ila tulikuwa na a common ancestor ambaye alikuwa more ape like, maana yake sisi tumebadilika zaidi.

Kwa mujibu wa evolution.

Evolution inakwenda kwa natural selection. Kuna mazingira fulani yanafanya species fulani zife, nyingine ziendelee kuwapo, nyingine zibadilike.

Kwa mfano, kwenye mazingira ya misitu, wanyama wanaofanana na misitu ile wanaweza kupata advantage ya kuwa camouflaged wakaendelea kuwapo, na wasio na rangi ya hiyo misitu kuwindwa kirahisi na kutoweka, matokeo yake baada ya vizazi vingi wanyama wenye rangi isiyo na advantage ya camouflage watatoweka na wale wanaofanana na msitu wataongezeka na kuwa ndiyo watawala.

Kitu kingine ambacho ni kigumu kuelewa ni kuwa, kwa mujibu wa theory ya evolution, evolution inatokea katika mamilioni na malaki ya miaka, mabadiliko madogo madogo yanalimbikizana na kusababisha mabadiliko makubwa.

Sasa watu wengi wanaohoji evolution wanahoji kama vike wanataka kuona mabadiliko katika umri wao, miaka 30, miaka 50.

Ukitaka kuona evolution katika muda nfupi usiangakie wanyama wakubwa kama sokwe, nyani au watu. Ukitaka kuangalia evolution katika muda nfupi angalia vidudu kama bacteria, virus.

Angalia kitu kinaitwa anti-biotic resistance na jinsi bacteria wanavyojenga resistance dhidi ya dawa.

Unajua kwa nini hospitali hawatumii tetracycline tena? Unajua kwa nini madawa ya zamani ya malaria hayatibu tena malaria inabidi tutumie madawa mapya?

Hiyo ni evolution. Vidudu vimejipanga kuweza kujikinga na dawa, vime evolve.

Ukitaka kuelewa evolution usiangakie nyani na watu, angalia jinsi bactwria na microorganism nyingine zinavyojenga resistance dhidi ya dawa, na kwa nini tunahitaji dawa mpya, kwa nini zamani magonjwa kama gono yalikuwa yanatibiwa na tetracycline lakini siku hizi kuna gononsugu halisikii dawa.

Vidudu vya gono vimefanya evolution.
We jamaa uko vizuri sana,hii ndio jf ya kipindi kile sasa
 
Back
Top Bottom