Mbona huyaorodheshi hayo mabaya nami nikuorodheshee yale mazuri? Msitafute pa kujifichia, mlianza kwa kusingizia covid 19, ikaja vita ya Ucraine na sasa mmekuja na sababu za mabadiliko ya tabia nchi.
1.Mauaji ya kutisha na ya mara kwa mara
2.Mbunge kupigwa risasi mchana kweupe kwenye eneo la ulinzi wa kila namna.
3.Kuibuka kwa viongozi uchwara na watekaji mfano:-Makonda,Sabaya,Mnyeti na wengineo
4.Uharibifu wa Demokrasia nchini mfano kuzuia mikutano ya hadhara na kufungia ovyo baadhi ya vyombo vya habari.
5.Ukabila:- Ndiyo awamu ambayo Wasukuma kwa asilimia kubwa wamepata mtelezo wa mambo mengi
6.Ukanda,awamu hiyo iliamini kuwa Wachapakazi bora Tanzania wanapatikana kanda ya ziwa na si vinginevyo
7.Kunvunjika kwa Umoja na mshikamano wa Watanzania
8.Ongezeko la deni la Taifa
9.Kujenga Chato kuwa jiji kwa sababu tu rais alizaliwa huko.
10.Nchi kuingia kwenye takwimu za uongo kwa sababu ya ukosefu wa uwazi na ukweli
11.Kuhujumu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020
12.Kuingilia Uhuru na maamuzi ya baadhi ya Vyama vya Upinzani mfano Chadema na Cuf.
13.Kupeleka Wabunge Bungeni ambao hawakustahili kuwepo kwa mujibu wa sheria mfano Covid 19