Kama Saudi Arabia na Vatican wameweza kufanya ibada majumbani sisi tuliopokea dini toka kwao tunashindwa nini?

Unaelewa tofauti ya kupokea na kuanzisha?
Ni lazima upokee kutoka kwa walioanzisha?
Saudi Arabia hawakuanzisha dini yoyote. Saudi Arabia ni nchi iliyoanzishwa juzi juzi tu 1932, na wale wale walioianzisha Israel.

Kama vitu huvijuwi ni heri ukafanya japo utafiti kwa kutumia Google tu kabla hujakurupuka na ku "offend' dini zisizo kuhusu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiona wameshindwa kufunga sehemu za kuabudu acha kwenda kusali/ Kuswali.
 
Saudi Arabia hawakuanzisha dini yoyote. Saudi Arabia ni nchi iliyoanzishwa juzi juzi tu 1932, na wale wale walioianzisha Israel.

Kama vitu huvijuwi ni heri ukafanya japo utafiti kwa kutumia Google tu kabla hujakurupuka na ku "offend' dini zisizo kuhusu.
Samahani ajuza nilidhani Maka na Madina ziko Saudia.

Pale Iran wanaswalia majumbani pia ila wenyewe wanamwogopa Trump siyo Covid 19!
 
Unaelewa tofauti ya kupokea na kuanzisha?
Ni lazima upokee kutoka kwa walioanzisha?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata kupokea, hatukupokea dini yoyote nkutoka Saudi Arabia.

Saudi Arabia imeanza 1932. Dini zote zilizopo Tanzania zipo kwa miaka mingi sana kabla ya Saudi Arabia.a

Sifahamu Ukristo ulipokelewa kutoka wapi lakini Uislam hapa kwetu haukupokelewa kutoka Saudi Arabia.
 
Samahani ajuza nilidhani Maka na Madina ziko Saudia.

Pale Iran wanaswalia majumbani pia ila wenyewe wanamwogopa Trump siyo Covid 19!
Makkah na Madina kwa sasa zipo Saudi Arabia lakini sisi hatukupokea dini kutoka Saudi Arabia. Saudi Arabia ni utawala wa kifalme ambao historia yake inaanzia 1932 tena haikuanzia Makkah na Madina.
 
Hata kupokea, hatukupokea dini yoyote nkutoka Saudi Arabia.

Saudi Arabia imeanza 1932. Dini zote zilizopo Tanzania zipo kwa miaka mingi sana kabla ya Saudi Arabia.a

Sifahamu Ukristo ulipokelewa kutoka wapi lakini Uislam hapa kwetu haukupokelewa kutoka Saudi Arabia.
Dini ya bakwata iliasisiwa miaka ya 60s!
 
Makkah na Madina Kwa sasa zipo Saudi Arabia laki Sisi hatukupokea dini kutoka Saudi Arabia. Saudi Arabia ni utawala wa kifalme ambao historia take inaanzia 1932 tena haikuanzia Makkah na Madina.
Wewe ni bakwata.....nilitolea mfano wa Prof Lipumba nikimaanisha wale waliopokea hiyo imani kutoka huko ilikoasisiwa.

Nashukuru kwa kunipa historia ya Saudi Arabia.
 
hatukupokea dini yoyote nkutoka Saudi Arabia.Dini zote zilizopo Tanzania zipo kwa miaka mingi sana kabla ya Saudi Arabia.a
Uislam hapa kwetu haukupokelewa kutoka Saudi Arabia.
upo sahihi bmkubwa.
kiukweli uislamu ulianzia pwani ya afrika mashariki karne nyingi zilizopita katika kitongoji cha kariakoo kinachopatikana mkoa wa dar es salaam, baadaye ukasambaa mpaka mashariki ya kati na duniani kwa ujumla.
takbirrrrrr.
 
Wewe ni bakwata.....nilitolea mfano wa Prof Lipumba nikimaanisha wale waliopokea hiyo imani kutoka huko ilikoasisiwa.

Nashukuru kwa kunipa historia ya Saudi Arabia.
Imani ipi na imeasisiwa wapi? Kumbuka Tu, Imani sio dini. Unaweza kuwa na dini lakini huna Imani.
 
kiukweli uisalamu ulianzia pwani ya afrika mashariki karne nyingi zilizopita katika kitongoji cha kariakoo kinachopatikana mkoa wa dar es salaam, baadaye ukasambaa mpaka mashariki ya kati na duniani kwa ujumla.

takbirrrrrr.
Kila mtu ana mawazo yake lakini mengine huwa ni porojo zisizo na maana. Majamvi haya yana wengi.

Ukiwa unamaanisha Dar Es Salaam kwa maana ya jina lake basi haupo mbali na kuwa sahihi. Itakuwa umesahau, si Kariakoo, ilikuwa ni tunayoiita sasa Ikulu. Rejesha kumbukumbu zako.
 
Jana nilimsikia Prof Lipumba akisema yeye ameanza kuswalia nyumbani ili kuepuka misongamano inayoweza kusababisha maambukizi ya Covid 19.

Binafsi nikawa nimemwelewa vilivyo.

Ndipo nikaanza kutafakari, kama Waislamu kule Saudia wanaswalia nyumbani Bakwata wanashindwa nini?

Kama Wakristo kule Vatican, UK na Germany wanasalia majumbani hawa Katoliki, Anglican na KKKT wanafeli wapi?

Kama Walokole huko USA wanasalia majumbani hawa kina Kakobe, Gamanywa, Gwajima, Mwingira wanashindwa nini?

Kuna wakati yatupasa kutumia busara hata kama mamlaka za juu zimewaachia hiyo fursa bado mnatakiwa kutumia hekima ya Mungu kutenda jambo sahihi.
Serikali haiwezi kuwakataza directly lakini nyie mmebarikiwa macho ya rohoni na mwilini na hata hao wagonjwa 88 waliotangazwa hadi sasa ni waumini wenu.

Hekima ya Mungu wa mbinguni na iwe juu yenu!
Rais amesema kagonjwa ni kadogo mbele ya Yesu hivyo hakuna haja ya kutishika tuenderee kwenda kwenye nyumba za ibada. Shida ya viongozi wetu mpaka tatizo liwe kubwa ndipo akili huwa zinawarudia.

Ugonjwa ulipoingia akatokea kiongozi mmoja mpumbavu wa chama akasema wapinzani ni sawa na korona. Hapo ndio kaanza kuupiga vita ugonjwa huo. Hatuja kaa sawa akatokea mjinga mwingine bwana masifuri gavana wa jimbo kuu. Yeye akasema anamshukuru Mungu kuwa mtoto wa kiongozi wa upinzani naye kapata korona.

Wapinzani waliposhauri kuwa tuzuie wageni viongozi wakajibu tupo vizuri tunahitaji pesa za watalii. Tukaendelea kupokea watalii kutoka China ulipoanzia ugonjwa. Baada ya mambo kuzidi wamefuata ushauri ule ule walioukataa

Wagonjwa walipoanza kuongezeka kiongozi mmoja wa upinzani akashauri badala ya kuwaweka karantini kwenye hoteli za gharama wanaotoka nje wawekwe kwenye mabweni kwani siyo wote wanauwezo wa kulipa gharama za hoteli. Wakatokea wabwatukaji wa chama wakamzodoa kiongozi. Hali ilipo zidi wakaanza kuwapeleka watu kwenye hostels za chuo wakati mwanzo walijia vichwa maji.

Wapinzani wameshauri tena tufunge makanisa na misikiti watu wasali nyumbani ili kuepuka maambuzi. Baba mkubwa amesema hapana huko ndiko kuna uponyani. Wakati wa Pasaka tumeona wenzetu waliotuletea hizi dini wakiendesha misa bila waumini kwa kutumia video. Sisi tunaojifanya tuko karibu sana na Mungu kuliko wao tukajazana makanisani. Sasa wagonjwa wanaongezeka na vifo vinaongezeka. Je wataendelea kusisitiza kutofunga makanisa na misikiti au akili zitawarudia baada ya tatizo kuongezeka? Baadhi ya makanisa yamesitisha huduma mbali mbali za shamra shara kama ndoa na vipaimara. Sasa hivi hata Sunday Schools zinaambiwa siyo sehemu ya kujaza wanafunzi waliopo likizo ya korona. Nini kinashindikana watu kumwomba Mungu wakiwa makwao mpaka waende makanisani na misikitini?
 
Rais hajalazimisha mtu kuendelea au kutokuendelea kwenda kanisani au msikitini. Kawaachia wenyewe mtumie akili zenu.
 
Ukimpa mtoto wako madafu ampelekee kitukuu chako bado ni sahihi kusema Uledi amepokea madafu kutoka kwa nyanya yake.
Dhana ya kupokea kitu ni pana sana.
Hata kupokea, hatukupokea dini yoyote nkutoka Saudi Arabia.

Saudi Arabia imeanza 1932. Dini zote zilizopo Tanzania zipo kwa miaka mingi sana kabla ya Saudi Arabia.a

Sifahamu Ukristo ulipokelewa kutoka wapi lakini Uislam hapa kwetu haukupokelewa kutoka Saudi Arabia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jana nilimsikia Prof Lipumba akisema yeye ameanza kuswalia nyumbani ili kuepuka misongamano inayoweza kusababisha maambukizi ya Covid 19.

Binafsi nikawa nimemwelewa vilivyo.

Ndipo nikaanza kutafakari, kama Waislamu kule Saudia wanaswalia nyumbani Bakwata wanashindwa nini?

Kama Wakristo kule Vatican, UK na Germany wanasalia majumbani hawa Katoliki, Anglican na KKKT wanafeli wapi?

Kama Walokole huko USA wanasalia majumbani hawa kina Kakobe, Gamanywa, Gwajima, Mwingira wanashindwa nini?

Kuna wakati yatupasa kutumia busara hata kama mamlaka za juu zimewaachia hiyo fursa bado mnatakiwa kutumia hekima ya Mungu kutenda jambo sahihi.
Serikali haiwezi kuwakataza directly lakini nyie mmebarikiwa macho ya rohoni na mwilini na hata hao wagonjwa 88 waliotangazwa hadi sasa ni waumini wenu.

Hekima ya Mungu wa mbinguni na iwe juu yenu!
Usiige kila unachoona kwa jirani
 
Back
Top Bottom